John Heche aitwa Polisi kwa tuhuma za kufanya mkutano jimbo lisilo lake - Kilombero

Sheria gani inakataza mtu kufanya mkutanowa siasa jimbo lisilo lake?

Na sheria hiyo inakosaje kupingana na sheria mama, katiba, inayoruhusu uhuru wa mikutano ya siasa bila kuangalia mipaka ya majimbo?
 
Wewe endelea kupayuka hapa lakini huyo Heche kesho anaripoti polisi asubuhi na mapema bila kubisha.
Halafu baada ya hapo anakufa?
Huyo ni mwanaume vitu vya kawaida,hakuna tabu, hivi mbona huwa hamjiulizi nani amewahi kufungwa na kosa hilo.
 
Toka tarehe 8 April 2017 mpaka leo polisi walikuwa hawajui Heche yuko wapi? hili jeshi ni hatari kuliko kitu chochote.
Kutakuwa na sauti juu yao imehoji kulikoni Heche hajahojiwa, na au kuwekwa sero kabisa? Mkumbuke Heche akiwa bungeni wiki iliyopita alishusha nondo akihoji maamuzi ya kujenga uwanja wa ndege Chato wa kiwango hicho wakati makao makuu ya nchi hakuna uwanja wa maana. Na alihoji kikao kipi cha bunge kilichoidhinisha fedha kwa ajili hiyo!
 
Kila jambo Lina mwisho!kipimo wanachowapimia mkihifafhi Kama si kesho kesho kutwa nikutumie hicho hicho kuwapimia!
 
Ndio maana nasema Mhe. Lowassa anawazidi wote ndio mgombea wao hafanyi huo ujinga ila wao kwa kujifanya wakaidi na wafia chama wanakaidi mamlaka halali acha akione cha moto
 
Back
Top Bottom