John Cheyo kumfagilia JK ni kujikomba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Cheyo kumfagilia JK ni kujikomba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by amba.nkya, Jan 20, 2010.

 1. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Katika hali isiyo ya kawaida mpinzani mkongwe, John Momose Cheyo ametamka rasmi kuwa rais JK ametimiza ahadi zake kwa wapiga kura na anawaonea huruma watakaojitokeza kuwania kinyang'ilo cha urais, 2010. Hii anamaanisha kuwa maisha bora kwa watanzania wote yamepatikana. Binafsi sikubaliani na kauli za Cheyo maana bado ahadi za JK kwa wananchi wake hazijatekelezwa kama alivyoahidi. Naawachia wana JF hapa jamvini kwa hoja zenu makini....mnasemaje?
   
 2. O

  Omumura JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ukishangaa ya Cheyo utastaajabu ya Mrema!
   
 3. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tanzania hatuna opposition!wote ni pesa tu.
  Tuna udikteta wa chama tawala.na tutaendelea na mediocre ya hawa wabunge wetu ,
  wanakula taxpayers money for nothing.kamati ya bunge ya Cheyo is a joke
   
 4. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ukiangalia kwa jicho la tatu wote hawa wanataka ccm isiwabane kwenye majimbo yao kipindi cha uchaguzi ndo maaana wanaifagilia ccm wakati last year tu walikuwa wanaikandia.njaaaa jamani njaaaaaa shem on them wanatuchanganya.......
   
 5. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,686
  Likes Received: 21,951
  Trophy Points: 280
  Kazungumzia wapi maneno hayo?
   
 6. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Yamezungumzwa almost all media...!
   
 7. N

  Nanu JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hebu ainisha ni zipi hajatekeleza? Ni rahisi kutoa statement ya moja kwa moja, lakini tukitaka kuwa analytical tuorodheshe alichoahidi JK, alichotekeleza, na ambayo bado hakijatekelezwa. Ni kwa analysis ndiyo unaweza kuchallenge JK. Kwasababu JK atakuja na list ya vitu kibao ambayo serikali imefanya, lakini yale yote ambayo hawajafanya hazitatajwa kabisa. Nadhani kuna waandishi wa habari waliokuwa wanaandika kila ahadi ya JK kwa ajili ya kufuatilia, lakini baada ya uchaguzi JK akawapa vyeo ili wasije wakawakumbusha wananchi hizo ahadi, wengine inawezekana sasa hivi wanamsaidia huko state house. Naomba kwa wale ambao wanakumbukumbu za ahadi alizotoa waziweke hapa mtandaoni ili tuchangie.
   
 8. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mabilioni ya JK hatuoni yamefanya nini?
  Hali bora kwa kila mdanganyika bado ni kitendawili,..n.k,n.k
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Jan 20, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Unamshangaa Cheyo,mbona ndio kawaida yake?Cheyo sio mpinzani wa kweli,w e fuatilia hata nyendo zake Bungeni utagundua kwamba jamaa siyo.
   
 10. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  wapinzani wa bongo mi wala hata siwaelewagi
   
 11. bona

  bona JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  njaa mbaya inaweza ikakufanya uonekane ni mpumbavu kuliko watu wote pasipo mwenyewe kujali ilimradi tumbo lako lipate chochote!

  watanzania tumsamehe john cheyo ni njaa jamani!
   
 12. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Mzee Cheyo anazeeka vibaya. Tunataka Maisha bora aliyotuahidi JK yako wapi???????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
   
 13. T

  TANURU Senior Member

  #13
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wasiliana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi atakupatia. Aliahidi ofisi yake watachapa kitabu ambacho kitaelezea kwa undani kila ahadi ya Rais aliyoitoa.
   
 14. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wote ni Makanjanja ya kisiasa na pia hii ni mbaya sana hata siku zinapokwenda ndio tunazidi kuwajua watu vizuri
   
 15. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kwani Bongo kuna mpinzani?

  Mi sijawahi waona toka nizaliwe miaka 60 iliyopita!
   
 16. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Naanza kuamini kuwa huu ni mkakati wa CCM kumsafisha JK, kwa hiyo wenyeviti wa vyama pinzani wameambiwa wasaidie kumsafisha kuelekea uchaguzi Mkuu
  1. Agustine Mrema
  2. Cheyo
  3. tusibilie list itaongezeka

  .......Upinzani wa kweli tutapata hadi hapo CCM itakapogawanyika makundi mawili -----kwa sasa upinzani ni utata mtupu.
   
 17. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CCM wanaogopa tu kivuli chao wenyewe na wameamua kuyatumia haya MAFUVU YA KISIASA (political fossils) kujaribu kuficha mapambano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea;

  Cheyo na Mrema wamebeba Bango la CCM Bara

  Seif Shariff Hamad amebeba Bango la CCM Zanzibar (au la Karume?)

  You will see more fossils rise as internal squabling continues.
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  jamani hivi hamjuagi kuwa Cheyo ni best na mtani wa JK?safari zake zote za kujitambulisha kama Pres wa Tanzania alikuwa anaenda nae.....wakikutana wanataniana sana sanaa.....hakuna upinzaji ni maslahi tu...umeshawahi sikia Cheyo anampiga kijembe JK hata kama amechemsha???never...ni ma best ever.......hata akikosa ubunge atampa wa kumteua......tena ukizingatia Mapesa ameanza kuchoka kibiashara siku za karibuni........
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,481
  Trophy Points: 280
  Kwanza alikuwa Mrema sasa Cheyo wote wanamfagilia Kikwete wa CCM badala ya kufagilia vyama vyao, huko CHADEMA ikiwa imebaki miezi 9 kabla ya uchaguzi mkuu hali si shwari wanafukuzana na kuadhiriana hadharani. Vyama vya UPINZANI HOVYO! Huu ulikuwa ni mwaka wao wa kufanya vizuri kufuatia utendaji finyu wa Kikwete na hali ilivyo ndani ya CCM lakini kwa mara nyingine tena they drop the ball! aaaarrrrrgggghhhhh! Si bora tu wamsimike Kikwete madarakani na Wabunge wote wa CCM ili kufuta uchaguzi ujao na kusave mabilioni ya shilingi.
   
 20. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Inawezekana kuwa ndio uamuzi mgumu ambao labda chadema wanaufanya ambao haufanywi na vyama vingine. Kwani mtu akienda kinyume na chama, mnampaka mafuta na kumsifia?

  Angesema hivi katibu mkuu/mwenyekiti wa chadema ungesema je?

  Ofcourse akisema Zitto, inasemekana ni msimamo wake binafsi, au siyo?
   
Loading...