Jogoo Aliyesema... Mnamkumbuka?!

Jogoo Aliyesema... Mnamkumbuka?!

hili jogoo nalikumbuka sana kwa kuwa lilitoa funzo kubwa kwa binadamu wote wanaowatesa wanyama. Ukitaka kujua alitoa funzo gani kamuulize PAZI aliyening'inizwa kichwa chini na miguu juu kama alivyokuwa akiwaning'iniza kuku wenzake na lile jogoo. Tungepata kiongozi mwenye kutoa discipline ya namna hii nadhani tugeheshimiana kwenye matumizi ya raslimali za Taifa letu. Eeeeeh Mola twaomba twaomba utushuhshie katika nchi yetu viongozi wenye kariba ya jogoo lililosema kwa kuwaadhibu wote wasiopenda mnaendeleo ya wananchi wote wa TZ
 
Kwa yeyote mwenye nakala ya kitabu hiki please nijulishe nimuonyeshe mwanangu tulosoma zamani za hapo kitambo kiasi
 
platozoom sungura ngoja nikumbuke ubeti walke mmoja ila pokea kwanza huu wa sikiri

sikiri mimi masikini narudi tena nyumbani
nikiwa huku porini napata shida jamani
sadiki sasa ashiba chakula kingi nyumbani .....................duh nimechemka asiee! sijui ma chemistry yamenipumbaza lol!
 
Last edited by a moderator:
platozoom sungura ngoja nikumbuke ubeti walke mmoja ila pokea kwanza huu wa sikiri

sikiri mimi masikini narudi tena nyumbani
nikiwa huku porini napata shida jamani
sadiki sasa ashiba chakula kingi nyumbani .....................duh nimechemka asiee! sijui ma chemistry yamenipumbaza lol!

Kwa nini umeishia njiani?..............hebu rekebisha memory kidogo au ulisoma inglish akademi ndio maana umesahau
 
haya tukumbuke na hii


600229_10150912220548581_1085862619_n.jpg
mandawa na manenge.
 
Safari yenye mkosi; Kapulya mdadisi; Mwampelwa the tax collector.
 
Nganenepa ang'atwa na nyoka; Ahadi 10 za mwana TANU; Kiburi si Maungwana, Mwenge kijiji cha Mahurunga (kijana Dadi); Kana kansungu, umwelu (Kalegesye); Bwana matata; Lyamba lya mfipa.

mh. we ni noma,really u made ma day. na hapa je:
Lindu amwokoa kapilima
watoto wageuka mawe.
pamela na kipini
kutengeneza kichanja.
matete na mpapai
 
Kwa nini umeishia njiani?..............hebu rekebisha memory kidogo au ulisoma inglish akademi ndio maana umesahau

Alitakiwa aandike hivi.
Sikiri mimi masikini
uvivu wangu nyumbani
ukiwa huu njiani
Nakufa hapa kwa nini?
Sadiki sasa ashiba
chakula kingi kwa baba...
 
Heri mimi sijasema.
Manenge na Mandawa.
Kalume kenge.
Togolo na mavazi ya kijerumani.
Kipofu Msese.
 
Safari ya Unguja
Siku ya ya gulio Katerero
Juma na Roza
Chopeko na mnofu
. . .
 
Watu wenye majina ya Pazi wana matatizo sana. Hapa JF kuna Mzaramo mmoja anaitwa hivyo, yaani anaichukia Yanga kiasi alifanya ule uharibifu kwenye basi letu pale Kabuku.

Namtafuta kitambo simuoni, nataka nimwalike Ikwiriri aje kula maboga na kambale labda akili yake itatulia. Pazi uko wapi wewe Mzaramo, ina maana hunisikii? Kweli simba kufungwa ndio hata tusisalimiane, mweh!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom