Jobless tunadhaurika sana

karibu chanika tulime mihogo mkuu.....haitaji mbolea wala umwagiliaji mkuu...
 
Nina dogo anajiona kama dunia imemuangukia mwenye balaa nimemshauri biashara hataki hata kusikia mwaka wa tano huu toka a graduate sasa hivi anamwambia mama atakunywa sumu ushauri wanajamvi
Sasa kama hata ushauri hataki uta msaidia je?
Mana ajira ndio kama hvyo finyu, akubali kuhamisha hayo mawazo yake ya Shule.
Asifikirie kuajiriwa tena a jaribu njia nyingine
 
Mkuu wasikusumbue,
Ukiona bahasha imechafuka tupa kule na weka cv kwenye bahasha mpya.
 
Hakika
 
Binadamu wameumbwa na kasumba flani. Wanaweza kukuheshimu au kukudharau kutokana na kazi unayofanya (hasa watanzania). Lakini pia usipokuwa na kazi wanakudharau vilevile.
[HASHTAG]#heshima[/HASHTAG] kazi #
Mungu atajalia neema na Baraka katika mihangaiko ya kila siku.
 
Hakuna fedhea kubwa dunia kama umesoma umri unaenda afu huna kazi kila mmoja atakudharau ila naamini Mungu ni wakwetu sote wakati wangu utafika tu.
Shida mnachagua kazi una degree huna uzoefu umekaa nyumbani unasubiri ajira itangazwe. Wenzio tulimaliza vyuo kwakua hatuonagi aibu bila kuchelewa tukaingia makampuni ya ulinzi kwa mishahara ya lakimbili na sabini baada ya muda tukaitwa kwenye interview za promotion tukiwa walinzi wa kawaida lakini tulikua tumeambatanisha na vyeti vyetu faster tukachukuliwa tukavua gwanda za ulinzi saizi tunapokea laki sita baada ya makato ingawaje si kikibwa sana lakini naridhika nacho maana wenzangu walionicheka mpaka sasa wanasota na mabahasha . Mdogo wangu nilimpa ujanja huo nae akaingia kwa ulinzi lindo alilo pangiwa akazoeana na boss wa pale faster kapata nafasi kaanza kula parefu zaidi yangu walio mcheka bado wanahangaika na ma interview. Na huo ujanja alinifundisha rafiki yangu yeye yupo bank ya Stanibic arusha alisota sana akaamua kuingia kwenye kazi za ulinzi aligundua kua kule kuna chance nyingi maana unaingia kulinda kwenye makampuni na mashirika tofauti hivyo inakua rahisi kujuana na wahusika maana kazi za sasa hivi 90% kujuana na undugu.hivyo kijana jichanganye
 
Hakuna fedhea kubwa dunia kama umesoma umri unaenda afu huna kazi kila mmoja atakudharau ila naamini Mungu ni wakwetu sote wakati wangu utafika tu.

Ipo fedheha.... Kwa single woman, single mother na mwanamke ambae ameolewa lakini ni tasa (hana mtoto) ...... kila mmoja atakudharau ila aamini Mungu ni wakwetu sote wakati wako utafika tu
 
Good spirit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…