Jobless-Graduates Association Press conference

Jobless-Graduates Association Press conference

PSPA Pure'12 udsm

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2013
Posts
834
Reaction score
450
Ndugu Wana-bodi

Nawasalim sana!
Kutokana na hali ya ajira nchini kuwa mbaya kiasi cha kutisha, huku serikali kama mwajiri mkuu na chombo pekee nchini cha kuzalisha fursa za ajira nchini kutokua na chembe ya dalili za kufanya jitihada za makusudi za kupunguza kama sio kumaliza kabisa janga hili, binafsi nimepata wazo la kujikusanya wahanga wa janga hili, yaani wahitimu wa vyuo vikuu,diploma,cheti ufundi na mafunzo mbalimbali wasiokua na ajira na kufanya yafuatayo;

1. Kuunganisha nguvu za pamoja na kuwa na sauti moja yenye nguvu na kuunda umoja wetu (Association). Hii itaakisi majitaji ya wahanga wa ajira popote Tanzania walipo kwa nia ya ku-pressurise serikali ifanye juhudi za kupunguza janga hili.

2. Kufanya Press Conference ya vyombo mbalimbali vya habari. Wote tunajua kwamba hiki ni kipindi cha bunge la bajeti. Press conference yetu ipaze sauti kwa serikali kuhusu tatizo la ajira, hivyo bajeti ilenge zaidi namna ya kutatua kero hii kwani na sisi tuna haki ya kulitumikia taifa hili kupitia fursa za ajira zinazoendana na ujuzi wetu.

3. Tunatambua kwamba mwaka huu 2014 na 2015 kutafanyika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu. Tuwaambie kabisa, kama hali itaendelea kuwa hivi hivi, wategee ushiriki wetu utakua wa kutosha sana unaolenga zaidi kuwaelimisha wananchi kuhusu utendaji mzuri wa serikali yao sikivu. Hivyo cha kinachoongoza serikali kisijisumbue hata kupiga kampeni maana kitakuwa kimepita bila kupingwa.

NB: Naomba hoja za maboresho na mapendekezo.
0718-257680

UPDATES
....................................

Kuhusu kujiunga.

1. Nimetoa namba ya simu hapo, naomba walio tayari tupange kukutana tarehe 18/5 2015 Napendekeza iwe pale mabibo hostel .

2. Nasikia kundi kikundi chenye mrengo na welekeo kama huu,nomba nao wanitafute kupitia namba hapo juu. Tutaungana nao ili kuwa na sauti ya pamoja.

3. Nitoe wito kwa wadau wote wahanga na wale waliopo makazini na media pia kutuunga mkono katika kufikisha sauti zetu kwa serikali. Mwalimu Nyrerere ashawahi kusema "No one is free if others are oppressed".
 
Yeah, ni Idea nzuri sana, nimeipenda, it needs people willingness hapa, sio kuongea tu humu but live press conference will be great!!!!, Akina Ridhione sio wenzetu, wao ni vimemo tu!!!!!
 
Sawa ila kuna harakati km hiyo inaendelea na thread ipo humu,unganisheni nguvu
 
Kaka kwa budget ya mwaka wa fedha huu ulishapita mi naona tufanye mapema na tujisajili kabisa then tuwafuate hukohuko bungeni tena kwa train,fusso au lori tukawambie na tuutangazie umma wa taifa na kimataifa
 
Mimi mbona tiyari, nilishaga toa wazo kama hili, ila nikaona vijana sisi wenyewe tuna matatizo makubwa sana kama kutaka kuona matokeo ya kitu kabla ya kitendo, kutaka mafanikio ya haraka*2 vitu ambavyo vinatugharimu kweli! ila namshukuru Mungu mpaka sasa nina kikundi changu na nilishasajiri kama CBO Morogoro ni vijana! Kama vipi tujoin coz mimi pia ni mwanaharakati sana tu wa maendeleo! (0763863919)
 
Mkiunda hicho kikundi kutakua na mchanganyiko wa professional mbalimbali ingesaidia zaidi mngeunganisha nguvu,resources,network na hata ideas ili mjiajiri. OR

Hiyo association iwe na business plan on the table asking for financial assistance; mkililia serikali kuhusu ajiri sidhani kama itawork out besides utumishi wanatoa ajira everyday and then zinapojitokeza
 
Yeah, ni Idea nzuri sana, nimeipenda, it needs people willingness hapa, sio kuongea tu humu but live press conference will be great!!!!, Akina Ridhione sio wenzetu, wao ni vimemo tu!!!!!

Very sure, naamini utakuwepo pale Mabibo hostel siku iliyopangwa.
 
apo kwenye uchaguzi wa serekali za mitaa....unaweza hatarisha naisha yako binafsi, siasa za tanzania ya leo ni za uhasama na uuwaji!!!
 
Kaka kwa budget ya mwaka wa fedha huu ulishapita mi naona tufanye mapema na tujisajili kabisa then tuwafuate hukohuko bungeni tena kwa train,fusso au lori tukawambie na tuutangazie umma wa taifa na kimataifa

Tulishawahi kushuhudia bajeti ya uchukuzi ikigomewa pale bungeni, kwahiyo nikutoe wasiwasi kwamba hatujachelewa.

Nimependa sana wazo lako la kuwafata bungeni. I need committed persons like you in action. Tukutane pale hostel, tupange lini tumaenda bungeni dodoma.
 
Mimi mbona tiyari, nilishaga toa wazo kama hili, ila nikaona vijana sisi wenyewe tuna matatizo makubwa sana kama kutaka kuona matokeo ya kitu kabla ya kitendo, kutaka mafanikio ya haraka*2 vitu ambavyo vinatugharimu kweli! ila namshukuru Mungu mpaka sasa nina kikundi changu na nilishasajiri kama CBO Morogoro ni vijana! Kama vipi tujoin coz mimi pia ni mwanaharakati sana tu wa maendeleo! (0763863919)

Asante mwanaharakati. Wote tusiokua na ajira tumajishughulisha kwa namna moja au nyingine lkn matokeo ni madogo ukilinganisha na ujuzi tulioubeba vichwani. Tunataka serikali ituwezeshe tutumie ujuzi wetu in full utilization.
Na hii sio kutaka mafanikio ya haraka.
 
Mkiunda hicho kikundi kutakua na mchanganyiko wa professional mbalimbali ingesaidia zaidi mngeunganisha nguvu,resources,network na hata ideas ili mjiajiri. OR

Hiyo association iwe na business plan on the table asking for financial assistance; mkililia serikali kuhusu ajiri sidhani kama itawork out besides utumishi wanatoa ajira everyday and then zinapojitokeza

Hiyo ni long term plan, kuteam up with business plan is a good idea. Hayo tumeshafanya bila chembe ya support ya serikali.

Nilikua mmoja wa waanzishi wa kinondon saccos
mwaka jana. Business plan zetu zinatekelezwa na vigogo pale manispaa huku sisi tukikosa hata mia ya maji ya kandoro. Ikibidi haki yetu itapatikana hata barabarani.
 
Hyo ndo udsm haki mbele heshima nyumbn kwakp.
Hawa wanasiasa ss bac kwnz wakilipuliw wote kwn kuna hasar gn?!
Hpa watu wanakaz ya kupean idea mgando tu za kujiajiri fursa zenyew zimekaa kisiasa siasa ukisem ufanye export unakutan na mianya yao.wanaomwagiw tindikal na kuham nchi sio bure.
Tujiajiri wametengenez mfumo gn wa kijan alotok chuo aweze kujiajir km sio kutak watu wakae mtaan mpk umri wa kustaafu uwakute?!
Idea nzur sn ya kuwafuat hko mjengoni naamin udsm kwny maswla ya haki na kujenga hoja.
Ila mleta uzi nawacwac wanawez kukutafut wakakup kitengo utulize munkari ss ole wao watakaokengeuka na kupotosh umma kucha zitahusika hpo.
 
Mkuu,naomba nikutoe hofu. Ninaongozwa sana na falsafa ya "Others first, me latet". sio hao mafisadi,ni wale watoto wa wakulima kama mimi.
 
mkuu mbona namba uliyotoa haipatikaniiii...hebu rekebisha,maana nataka tuunganishe nguvu.......umoja ndo nguvu yenyewe hiyo!
 
Back
Top Bottom