Job ndugae ni mfuasi wao (mafisadi)???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Job ndugae ni mfuasi wao (mafisadi)????

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jethro, Nov 9, 2010.

 1. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Katika kutafakari saaana na kuangalia ndani ya CCM kwa wale walio chukua form kuwania nafasi ya USPIKA wa Bunge(10). Nimepatwa na wasiwasi saana, kwani naonavyombo vyote vya Habari(Magazeti,TV,Radio), Taasisi za Elimu, Na Raia, Wanao tumia mitandao ya Internet wamekuwa wakiangaza macho yao kwa Andrew Chenge na ninamashaka makubwa sana CCM kumpitisha Chenge kwani ita kuwa ni ndoto ya mchana kweuuupee nadhani twapigwa changa la macho hapo.

  Lakini tukirudi nyuma tutafakali katika hawa wagombea USPIKA tokea CCM kama JOB NDUGAE nadhani ni mmoja wa mafisadi kwani yeye yupo kama vile ni mmoja wetu sie tunaopinga vita ya mafisadi lakini kavaa ngozi ya Chui huyi mtu nina mashaka sana nae kuwa CCM yaweza mpitisha maana yeye yupo yupo machoni pa raia anaonekana yuko safi na hana upande.

  Wana JF hili ndolo duku duku langu.
  Mwageni nanyi hoja zenu karibuni uwanja ni wenu huu wa maoni
   
 2. k

  kiche JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  tetesi zilizopo toka kwa wabunge wateule Job ndiye chaguo la chama!na kwa wale wabunge wa ndiyo mzee wameshapewa taarifa mtu wa kuchagua ni yeye,na inasemekana si mtu safi!kwa vile ni tetesi subiri tuone
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ni mtetezi sana wa chama chake hata kama ni kwa gharama ya watanzania. Sidhani kama anafaa kuwa spika. Spika mzuri ni yule anayejali maslahi ya taifa na siyo chama. Ndg zangu lazima tuwe wakweli mzee sita bado anaonekana kuwa kinara ktk orodha ya wana ccm waliochukua fomu za kugombea uspika.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Piga ua CCM wataweka mtu wao... kinachotakiwa ki huyo mtu kuwekwa kwenye hali ngumu kila siku kama ataendelea kutetea upande mmoja tu wabunge
   
 5. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #5
  Nov 10, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  CCM waumizane tu wenyewe. Napenda kuwahakikishia kuwa kwa kikosi cha CHADEMA kilichoshuka bungeni mwaka huu, no way hata awekwe makamba pale, hataweza kuwazuiya kuichachafya ngome ya serikali. Ni sawa na timu ina Drogba, Messi na Ronaldo, alafu unamwambia Paulsen asuke ngome ya Taifa Stars kuwazuia! Atamweka nani...
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  No way kwamba safari hii uadilifu utashinda. Sitta atapewa uwaziri wa Marmo - Bunge na Katiba na kuachia uspika, Andrew Chenge atapeta kama kawa
   
 7. t

  tumwe273us Member

  #7
  Nov 10, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugai sio m2 mzuri,kunakipindi nilitembelea wilaya ya Kongwa ambapo mzee huyu ndie mbunge wao.ukiwa unaenda dodoma mbele kidogo soko kubwa la kibaigwa kuna rachi ya NARCO ambayo alidai kuwa anataka imegwd wagaiwe wananchi wa jimbo lake,lakini kumbe alikua ameshajiandaa kununua heka 100 ndani ya hy ranchi.hvy is not a gud person na ni fisadi pia.
   
 8. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Hili la Spika sisi tusio na kura tunalichukulia jambo jepesi tu!!!Lakini ni kweli kabisa mambo mengi ya kitaifa yanamtegemea mtu huyu Spika jinsi gani atayapika huko bungeni !!Ni dhahiri zaidi kwamba nafasi hiyo inahitaji mtu makini na mwenye mtizamo mpana zaidi ya maslahi ya Chama chake.Tunamhitaji mtu anayeweza ku balance issues na kuja na suluhisho la uhakika.Mtu mbabaishaji ni hatari hata kuliko fisadi!!Chama Tawala kinayo nafasi kubwa ya kumchagua Spika ukizingatia wingi wao bungeni pia na Uzoefu.Sitarajii CCM kumchagua mtu ambaye kazi yake ni kuukandamiza upinzani na hoja zake pale bungeni.Watanzania siyo wale wa karne iliyopita tena,Wanaelewa mambo yote yanayowazunguka leo.Kwa hiyo kuwachagulia Spika wa Bunge mwenye dhamira ya kufunika Upinzani watakuwa wamejimaliza wenyewe kwani ukweli nusu ya population ya wananchi wako Upizani na wanavumilia matendo maovu yanayofanywa na chama tawala.
   
 9. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Naomba kuuliza kumilikisha mtu vijishamba vya eka tatu tatu na mwingine kumiliki eka 100 ni lipi lenye faida kwa uchumi wa Taifa? Mimi nadhani huyu wa Eka 100 atakuwa anakuza uchumi wa Taifa kwani yuko kibiashara zaidi. Yule wa eka tatu ni kwa ajili ya kulisha familia yake tuu na ziada labda kwa ajili ya ngoma
   
 10. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2010
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  If he is not one of you be sure he is not against them
   
 11. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Surname Ndugai
  First Names Job Yustino
  Country of Birth Tanzania
  Positions
  Date of Birth 21 Jan 1960
  From To Organisation Position
  2005 Kongwa Constituency MP for Kongwa
  Political Affiliation CCM

  Notes EDUCATION
  School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
  Open University of Tanzania LLB 2000 To date NOT COMPLETED
  University of Norway MSc. in Mgt. Natural Resources & Sustainable Agric. 1995 1996 MASTERS DEGREE
  University of Norway PG Diploma in Mgt of Natural Resources 1994 1995 POSTGRADUTE University of Dar es Salaam BSc. (Zoology Wildlife Ecology) 1989 1993 GRADUATE MWEKA Wildlife College Diploma in Wildlife Management 1986 1988 DIPLOMA
  Old Moshi High School A-Level Education 1982 1984 HIGH SCHOOL
  Kibaha Secondary School O-Level Education 1978 1981 SECONDARY
  Matare Primary School Primary Education 1971 1977 PRIMARY
  --------------------------------------------------------------------------------
  CERTIFICATIONS
  Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
  No items on list
  --------------------------------------------------------------------------------
  EMPLOYMENT HISTORY
  Company Name Position From Date To Date
  Frankfurt Zoological Society Technical Officer 2000 2000
  Serengeti Regional Conservation Project Manager 1997 1999
  Ministry of Natural Resources and Tourism Coordination Officer 1996 1996
  Selous Game Reserve Manager 1993 1999
  Ministry of Natural Resources & Tourism-Liwale District Wildlife Officer 1988 1989
  --------------------------------------------------------------------------------
  POLITICAL EXPERIENCE
  Ministry/Political Party/Location Position From To
  CCM-Chama Cha Mapinduzi Member of Parliament(Kongwa District) 2000 Todate
  CCM-Chama Cha Mapinduzi Ward Youth Commander 1996 1999
  CCM-Chama Cha Mapinduzi Chairman(Work Place) 1996 1999
  CCM-Chama Cha Mapinduzi Member 1981 Todate
  [ Retrieved on 1/7/2006 - Parliament of Tanzania ]
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  Nov 10, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kwangu mimi nadhani sita ndio kinara kwa ubora pamoja na madhaifu yake, napata tabu kumlinganisha sita na chenge,job au makinda
   
Loading...