JKT zaidi ya 300 waandamana sababu ya ajira

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,798


1:01 AM HABARI KITAIFA

VIJANA zaidi ya 300 waliopata mafunzo kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wameandamana kwenda Ikulu kumwona Rais Jakaya Kikwete ili asikilize kilio chao na kupinga upendeleo wa ajira ndani ya jeshi.


Maandamano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam jana kwa saa mbili asubuhi kwa vijana hao kujikusanya katika eneo la Jangwani huku wakiwa wameshika bendera nyekundu kupita barabara ya Morogoro, Umoja wa Mataifa hadi Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).


Vijana hao baada ya kufikia katika eneo hilo walizuiwa na askari polisi waliokuwa wameweka ulinzi maalumu huku wakiwataka kueleza matatizo yao kwani si kila jambo linapaswa kufanywa maandamano, mengine yanaweza kuzungumzwa.
Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Magesa Masatu, alisema lengo la maandamano hayo ni kupeleka kilio chao kwa Rais Kikwete baada ya kukosa ajira kwa muda mrefu ndani ya jeshi.


Alisema walifikia uamuzi huo baada ya kupeleka barua za maombi ya kazi Wizara ya Kazi na Ajira, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ulinzi bila kupatiwa ufumbuzi wowote.


“Vijana wengi wamekuwa wakipelekwa JKT na kuahidiwa kupatiwa ajira, lakini toka mwaka 2000 hadi 2014 wameajiriwa vijana wachache na wengine tumekuwa tukiachwa. “Kama Serikali haina uwezo wa kuajiri vijana kwanini wanatupeleka JKT na kutupatia mafunzo ambayo wanajua kuwa baadaye tunaweza tukayatumia vibaya kutokana tatizo la ukosefu wa ajira?


“Wengi hatuna kazi tunaishia kuzurura mitaani bila kazi yoyote, kutokana na hali hii mafunzo tuliyopewa yanaweza yakasababisha vijana wengi kufanya mambo ambayo baadaye yataleta adhari kwa taifa,” alisema Masatu.


Kwa upande wake Fabian Mashauri alisema wasipopata majibu mazuri kutoka kwa Rais Kikwete wataendelea kupigania haki yao hadi pale itakapopatikana. Pia alisema Serikali isipoangalia suala hilo la vijana, watakuwa wanatengeneza makundi hatari ambayo yatakuja kuliathiri taifa.MutalemwaBlog
 
Labda waandamane after 2015. Sasa hivi mkulu yupo busy kuchanganya Maazimio ya Bunge na za kwake.
 
Huko JKT wamekuwa wakifundishwa kazi za mikono, inakuwaje sasa wanashindwa kujua malengo ya JKT? Kwani ni nani aliwadanganya kuwa ukienda JKT sharti uajiriwe hata kama hauna sifa za kuajiriwa?
 
Wamefundishwa silaha alafu wanaandamana kama sie mambumbumbu wa silaha! Kweli ujinga wa mtu upo damuni mwake.
 
Labda waandamane after 2015. Sasa hivi mkulu yupo busy kuchanganya Maazimio ya Bunge na za kwake.
nadhani mchanganyiko huu ni mgumu, lazima kuna moja inaelea juujuu haitaki kuchanganyika.Mbona anachukua muda mrefu?.
 
Uzuri hao ni wapiga kura wanangoja tu wakati ufike watoe adhabu kwa wabaya wao kupitia sanduku la kura.

Ni kweli tatizo la ajira ni la dunia nzima lakini sisi hata viwanda tumeu, sasa hili tatizo tunalikabili vipi kama sio kuwatekeleza hawa vijana maana hata viwanda vipya vimetushinda kuvianzisha?
 
Huko JKT wamekuwa wakifundishwa kazi za mikono, inakuwaje sasa wanashindwa kujua malengo ya JKT? Kwani ni nani aliwadanganya kuwa ukienda JKT sharti uajiriwe hata kama hauna sifa za kuajiriwa?
Bwabwaja hivyo hivyo, subiri matokeo yaja. Omba uzima tu
 
Rais kachoka mara huku mara kule mara xkroo, mara nani agombee kupitia ccm, familia aargrr
 
Mkuu hicho kichwa cha habari wengine nusura turudi kambini toka maeneo ya starehe tukifikiri kuna uasi. Manake mwanajeshi haruhusiwi kuandamana, akiandamana ni uasi na uasi hukumu yake ipo wazi.

tuwe tunaangalia vichwa vya habari tusije kuleta sintofahamu
 
Mkuu hicho kichwa cha habari wengine nusura turudi kambini toka maeneo ya starehe tukifikiri kuna uasi. Manake mwanajeshi haruhusiwi kuandamana, akiandamana ni uasi na uasi hukumu yake ipo wazi.

tuwe tunaangalia vichwa vya habari tusije kuleta sintofahamu

..hao ni "wanajeshi."

..ukiachilia hilo tujiulize kwanini wameandamana.

..je, kuna kitu waliahidiwa na sasa wanafuatilia utekelezaji wake?

..serikali iache kutoa ahadi kwa mambo ambayo hawana uhakika wa kuyatekeleza.

cc Lizaboni, Salary Slip
 
Last edited by a moderator:
Kweli kabisa.
nyie wajinga wa Lumumba na hizo genye zetu mnapanukwa tu ! hivi hamuioni hiyo threat ya hao vijana kwa Taifa? kuweni kidogo basi hata na staha post ambazo hamna uwezo nazo kuzijibu embu ziacheni! makende yenu
 
..hao ni "wanajeshi."

..ukiachilia hilo tujiulize kwanini wameandamana.

..je, kuna kitu waliahidiwa na sasa wanafuatilia utekelezaji wake?

..serikali iache kutoa ahadi kwa mambo ambayo hawana uhakika wa kuyatekeleza.

cc Lizaboni, Salary Slip
mkuu nilichowahi kusikia ni Rais kutoa maagizo kwamba kukiwa na ajira kwenye vyombo vya ulinzi na usalama basi wale waliopitia JKT waajiriwe. Hivyo siyo kwamba wote waliopitia JKT wanatakiwa kuajiriwa. Inategemea nafasi za kazi zilizopo. Labda hapa kuwe na issue kwamba hakuna uwazi na kuna watu wanaajiriwa ambao hawakupitia JKT ama hata kama wamepitia lakini kuna upendeleo. Hilo linatakiwa liangaliwe na kuchunguzwa hasa tukikumbuka yaliyotokea Uhamiaji.
 
Hivi ni kweli waandamanaji tajwa wote ni wahitibu wa JKT! au ni msafara wa mamba na kenge wanaweza wakawemo?
 
Back
Top Bottom