Jkt iwe lazima kwa kila mtanzania?

pembe

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,067
2,000
Kwa wale waliopitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanajua fika faida ya jeshi hilo kwa nchi yetu.
Nina mawazo kuwa kuwe na kipengele katika katiba mpya ikisisitiza kuwa ni wajibu kwa kila mtanzania aliyefikisha miaka kumi na minane na kuendelea awe amepata mafunzo haya.
Hii itasaidia sana kwa vijana kuwa na fikra za kizalendo na pia kila mtanzania atakuwa tayari kujihami kwa lolote lile kwani kumkabili adui si lazima uwe na silaha, na hata katika kujiokoa kwahitaji mbinu za medani.

Huenda hii mada imeshaletwa jamvini kama tayari mnisamehe bure!
 
TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,785
2,000
Hii itasaidia sana kwa vijana kuwa na fikra za kizalendo !
It is wastage of time kama issue ni kujenga uzalendo,kwani hii tayari imeshaonyesha kushindwa kwa kuwa mafisadi wengi tunaolia nao sasa wamepitia huko JKT!
 
HOMOSAPIEN

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
724
225
Kwa wale waliopitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanajua fika faida ya jeshi hilo kwa nchi yetu.
Nina mawazo kuwa kuwe na kipengele katika katiba mpya ikisisitiza kuwa ni wajibu kwa kila mtanzania aliyefikisha miaka kumi na minane na kuendelea awe amepata mafunzo haya.
Hii itasaidia sana kwa vijana kuwa na fikra za kizalendo na pia kila mtanzania atakuwa tayari kujihami kwa lolote lile kwani kumkabili adui si lazima uwe na silaha, na hata katika kujiokoa kwahitaji mbinu za medani.

Huenda hii mada imeshaletwa jamvini kama tayari mnisamehe bure!

Kwa usalama wetu jambo hilo la miaka 18 must kupita JKT siafiki kabisa mafunzo ya kijeshi kwa raia wote baadae uwaache bila kazi wanaweza kugeuka akitokea mwehu mmoja akawapa silaha nchi hii na huu ufisadi patachimbika,bora JKT ikirudi ianze na wale kuanzia form iv na kozi ya mwaka 1 ambao hawakupata mfunzo hayo baada ya kusitishwa mafunzo popote pale walipo ndiyo waanze.na wachache wa kujitolea kama zamani.
 
snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,286
2,000
labda wale waliomaliza form four na kwenda tertiary education(vyuo vya ufundi),ndio wadahiliwe kwa wingi jeshini.maana sikuhizi mafundi hawana maadili kabisa,wengine wamelegealegea tu.....ni mawazo yangu tu
 
Straddler

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
722
195
Kwa wale waliopitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanajua fika faida ya jeshi hilo kwa nchi yetu.
Nina mawazo kuwa kuwe na kipengele katika katiba mpya ikisisitiza kuwa ni wajibu kwa kila mtanzania aliyefikisha miaka kumi na minane na kuendelea awe amepata mafunzo haya.
Hii itasaidia sana kwa vijana kuwa na fikra za kizalendo na pia kila mtanzania atakuwa tayari kujihami kwa lolote lile kwani kumkabili adui si lazima uwe na silaha, na hata katika kujiokoa kwahitaji mbinu za medani.

Huenda hii mada imeshaletwa jamvini kama tayari mnisamehe bure!
Sio fikra za kizalendo tu... Jeshi linasaidia kujenga nidhamu kwa vijana. Ndio maana vijana wengi wa siku hizi hawana adabu.
 
pembe

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,067
2,000
It is wastage of time kama issue ni kujenga uzalendo,kwani hii tayari imeshaonyesha kushindwa kwa kuwa mafisadi wengi tunaolia nao sasa wamepitia huko JKT!
Sasa kama itabidi kwenda mpakani na Malawi tutapeleka nani? Wakati wa Idd Amin JKT iliokoa jahazi. Hawa mafisadi bomu likilipuka tu ndio wa kwanza kulala kifudifudi na kupanua midomo kwani wanazijua hizo mbinu. Ufisadi ni kipindi cha mpito tuu na 2015 wakae chonjo kwani watajuta kuzaliwa bongo.
 
TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,785
2,000
Sasa kama itabidi kwenda mpakani na Malawi tutapeleka nani? Wakati wa Idd Amin JKT iliokoa jahazi. Hawa mafisadi bomu likilipuka tu ndio wa kwanza kulala kifudifudi na kupanua midomo kwani wanazijua hizo mbinu. Ufisadi ni kipindi cha mpito tuu na 2015 wakae chonjo kwani watajuta kuzaliwa bongo.
Ikitokea vita watakwenda wanajeshi kwa kuwa hiyo ndiyo kazi walioajiliwa kuifanya!kwani sasa hivi tauna wanajeshi?na kama hawatoshi hatuwezi kuwaongeza?ninachokikataa mimi ni kulazimisha kila mmoja aende JKT kwa sababu ya kujenga uzalendo,hii sikubaliani nayo kwa kuwa hatutaweza kufikia malengo tunayokusudia!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom