JK: Waziri Mponda, Lucy hawang`oki

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
JK(53).jpg

Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick na kushoto ni Mwenyekiti wa Wazee mkoani Dar es Salaam, Idd Simba. (PICHA: SELEMANI MPOCHI)

Uwezekano wa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya, kujiuzulu au kuondolewa kwenye nafasi zao ni sawa na haupo kwa sasa kufuatia kauli ya Rais Jakaya Kikwete wakati akihutubia

taifa kupitia mkutano wa wazee wa Dar es salaam kwamba nafasi zao ni za kuteuliwa na zinaweza kubadilika wakati wowote na haziwezi kuathiri maamuzi ya kisheria ya serikali.

Madai ya kujiuzulu au kuondolewa kwa Dk. Mponda na Nkya yamekuwa ni muhimili wa kuendelea kwa mazungumzo baina ya madaktari na serikali ambayo yalikwama na kusababisha kuibuka kwa mgomo wa mara ya pili ya watumishi hao wa sekta ya afya kabla ya kuusitisha kufuatia amri ya mahakama na baada ya kukutana na Rais Kikwete Ijumaa iliyopita.

Akizungumza katika mkutano wa jana na wazee, Rais Kikwete alisema suala la kuondoka kwa mawaziri hao halina umuhimu sana kwa sababu ndani ya wizara hiyo kama ilivyo kwingine, wamepita mawaziri wengi ila jambo la msingi ni

kuweka mfumo wa kisheria juu ya madai ya madaktari ili yeyote atakayekuwa waziri asiwe na uwezo wa kuyagusa.
Alimtaja Dk. John Magufuli kuwa ni miongoni mwa mwaziri aliyeanza naye utawala wa awamu ya nne akiwa Wizara ya

Ardhi na Maendeleo ya Makazi, lakini baadaye akamuahamishia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kisha akarejea Wizara ya Ujenzi aliko sasa.

Dk. Magufuli chini ya awamu ya tatu alipata pia kuwa Waziri wa Ujenzi, alianza kama Naibu Waziri katika wizara hiyo mwaka 1995 na mwaka 2000 akawa waziri kamili.

Rais Kikwete alisema madaktari wanaamini kwamba mambo yao yamekwama kutokana na mawaziri waliopo na kwamba hata kama makubaliano yakifikiwa na serikali juu ya madai yao hawana imani kama mawaziri hao wanaweza kuyasimamia katika utekelezaji wake.

Alisema hakuwa amepata tuhuma au sababu za msingi za kuwaondoa viongozi hao wa wizara.
“Madaktari wamesema wanataka kuzungumza na watu wapya, lakini nimewaambia mawaziri hawa wanazunguka sana kwa hiyo kubwa hapa ni kutengeneza regulations (kanuni) au sheria ili akija waziri msiyempenda asicheze nayo,” alisema.

Alisema mgogoro baina ya madaktari na viongozi wa Wizara ya Afya unatokana na kutoaminiana baina ya pande hizo jambo alilosema ni kanuni au sheria ndizo zitakazoweza kulikomesha.

Hata hivyo, aliwapongeza madaktari kwa kukubali kusitisha mgomo baada ya kukutana naye na kueleza kwamba “nasema wameniamini na ninawasihi waendelee kuniamini, tutashughulikia madai yao na tutatengeneza mazingira mazuri.”

Rais Kikwete aliwaomba madaktari kutogoma tena kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha taaluma yao na pia ni kukiuka sheria inayoruhusu mgomo ambayo inazuia watumishi wa sekta ya afya hususani madaktari na wauguzi kutoshiriki mgomo.

Kada nyingine zinazozuia kugoma ni nishati ya umeme pamoja na maji.
“Nawaomba madaktari huu uwe mgomo wa mwisho, taaluma yenu inawataka iwe hivyo na sheria za nchi zinataka hivyo …serikali ipo tayari kuzungumza zaidi lakini tunapozungumza tusiwekeane sana masharti,” alisema Rais Kikwete.
Hata hivyo, alisema serikali itatimiza madai yote ya madaktari.

MADAI YA MADAKTARI

Akizungumzia madai ya nyongeza ya mishahara, posho mbalimbali za mazingira hatarishi, mazingira magumu, nyumba, usafiri na kuitwa kazini kwa dharura, alisema italazimu kila daktari kulipwa Sh. milioni 7.7 kwa mwezi wakati daktari bingwa atalipwa Sh. milioni 17 kwa mwezi.

Katika madai hayo, madaktari wanataka mshahara wa kuanzia uwe Sh. milioni 3.5, posho ya mazingira hatarishi (asilimia 30 ya mshahara wa mwezi).

Posho nyingine na nyongeza ya asilimia kwenye mabano ni mazingira magumu ya kazi (40); nyumba (30) usafiri (10); kuitwa kwa dharura (10) na kupewa kadi ya kijani ya bima ya afya.

Rais alisema madai kama hayo si rahisi kupatiwa majibu ya papo kwa papo, lakini serikali ina mpango wa kuboresha maslahi ya watumishi wa sekta ya afya na tayari imeanza mchakato wa kuyashughulikia.

Alisema serikali ina mpango wa kujenga nyumba 700 nchi nzima na kila wilaya itapewa nyumba 18 za madaktari.

Rais Kikwete aliwashangaa wanaharakati kwa kutokemea mgomo huo ambao ulikuwa unahatarisha uhai wa wananchi, na kuhoji wanasimamia nini katika haki za binadamu kama hawezi kutete haki ya msingi ya kuishi.

Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam, Iddi Simba, akimshukuru Rais Kikwete kwa niaba ya wazee wenzake alimshukuru kwa kumaliza mgomo huo na kusisitiza kuwa adha yake ilikuwa kubwa kwa wananchi na ilikuwa inatishia mfumo mzima wa utawala nchini.

Alisema wazee nchi nzima wanataka kuunga ili kutoa ushauri kuhusu masuala mbalimbali yanayokabili taifa kabla mambo hayaharibika.

CHANZO: NIPASHE
 
JK%2853%29.jpg

Kimsingi ni kweli kabisa katika hotuba ya JK hakuna mahali alipoonesha wazi kuwa atawaondoa kwenye nafasi zao mawaziri hao. Na naamini, alichokisema kwamba uandalaliwe utaratibu wa kisheria ambao utalenga kusimamia haki za madaktari na wala sio suala la nani yupo kwenye nyazifa hizo dio jambo la msingi kutokana na ukweli huo kwamba wanahama hama kila inapobidi.

Hatahivyo, kwa tuliofuatilia kwa umakini hotuba ile tumegundua kwamba sula la mawaziri hawa kuondolewa kwenye wizara hiyo liko njiani. Ni suala la muda tu. Na hili linatokana na ukweli kwamba, katika hotuba yake mh. Rais amegusia suala zima la mahusiano mema kazini karibu mara mbili.Kwamba ameliona hilo na kwamba ni wazi atalishughulikia. Kwahiyo nadhani tusubiri tu muda ukifika wataondolewa wizarani hapo.
 
Back
Top Bottom