JK: Watakaofanya fujo tume ya katiba kukiona | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Watakaofanya fujo tume ya katiba kukiona

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kikulacho, Apr 13, 2012.

 1. K

  Kikulacho Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  RAIS Jakaya Kikwete, amewaonya watu watakao fanya fujo watashughulikiwa na vyombo vya sheria ikiwemo kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya Katiba.
  Kauli ameitoa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwaapisha wajumbe wa tume ya kuratibu mabadiliko ya Katiba ya nchi, ambapo alisema kutokana na umuhimu wa kazi hiyo Serikali itahakikisha itatoa ulinzi wa kutosha mara tume hiyo itakapo anza kazi rasmi ya kuratibu maoni kwa wananchi kwa kuhakikisha ina imarisha ulinzi kwa wajumbe wa tume hiyo ikiwemo kupambana na watakaofanya fujo kwa kuchukuliwa hatua na vyombo vya dola.
  Rais Kikwete, alisema pamoja na kazi hiyo wamewataka Watanzania kutambua kuwa kazi ya tume hiyo ni kuratibu maoni ya Katiba mpya, na sio ya kujadili kuwepo au kutokuwepo Muungano ila ni mchakato wa kupata katiba bora itakayoendesha Taifa la Tanzania.

  Wajumbe hao wa tume ya mabadiliko ya Katiba walioapishwa na Rais Kikwete ni pamoja na Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba, Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Augustino Ramkadhani pamoja na wajumbe wake ambao ni Profesa Mwesiga Baregu, Riziki Shahari Mngwali, Dk. Sengodo Mvungi, Richard Lyimo , John Nkolo, Alhaj Said EL- Maamry, Jesca Mkuchu, na Profesa Palamagamba Kabudi.

  Wengine ni Humphrey Polepole, Yahya Msulwa, Esther Mkwizu, Maria Kasonda, Al-Shaymaa Kwegyir na Mwantumu Malale pamoja na Joseph Butiku.

  Wengine ni Dk.Salim Ahmed Salim, Fatma Said Ali, Omar Sheha Mussa, Raya Suleiman Hamad, Awadh Ali Said, Ussi Khamis Haji, Salma Maoulid, Nassor Khamis Mohammed, Simai Mohamed Said, Muhammed Yussuf Mshamba, Kibibi Mwinyi Hassan, Suleiman Omar Ali, Salama Kombo Ahmed, Abubakar Mohammed Ali, Ally Abdullah Ally Saleh.

  Pamoja na Katibu wa tume hiyo Assaa Ahmad Rashid na Naibu Katibu wake Casmir Sumba Kyuki.
  Rais Kikwete, alisema kutokana na kazi hiyo Tume hiyo inayoongozwa na Jaji mstaafu Joseph Warioba, itafanya kazi ya kukusanya maoni kuhusu katiba na maslahi ya Wananchi wa pande mbili zinazounda muungano.

  Alisema kwa muda mrefu kumekuwepo na hali ya kutoaminiana kati ya Serikali na wadau hasa mara ulipotangazwa muswada wa mabadiliko ya katiba huku baadhi ya vyama vya siasa kuona havina uwezo wa kukishinda Chama Cha Mapinduzi (CCM), na hata kuibua hoja mra kwa mara ya kuhitaji mabadiliko ya katiba ya nchi.

  "Kuzinduliwa rasmi kwa tume hii ya kuratibu maoni ya kupata katiba mpya ya nchi ni ishara tosha ya Taifa letu kuingilia katika historia iliyotukuka kwa kuanza safari mpya ya kuelekea kuzaliwa kwa Katiba mpya itakayotokana na maoni ya Watanzania wenyewe.

  "Pamoja na hili kwetu sisi upande wa Serikali tutahakikisha tunatoa ulinzi wa kutosha kwa tume hii mara itakapoa anza kazi ya kuratibu maoni kwa wananchi na tunajua wapo wale wakorofi ikiwa wataleta fujo watashughulikiwa na vyombo vya dola kwa mujibu wa sheria.
  "Mbali na hilo tutawawezesha kikamilifu ikiwemo vitendea kazi pamoja ikiwemo usafiri pamoja na fedha ili mfanye kazi hii ya Watanzania kwa ufanisi wa hali ya juu kama ilivyokusudiwa.
  "Tangu nilipotangaza uteuzi wenu kwa kweli Watanzania wengi wameupokea vizuri, nanyi mna wajibu wa kufanya kazii kwa niaba ya Watanzania wote na sio kuteta misimamo ya vyama vyenu au taasisi zenu. Kuwepo kwenu katika tume hii hakika mmekuwa wawakilishi kwa kila Mtanzania katika kuifanya kazi hii ambayo nina aamini italeta mafanikio makubwa kwa Taifa letu," alisema Rais Kikwete.

  "Mwalimu Julius K. Nyerere, alisema mawazo hayapingwi kwa rungu bali hujibiwa kwa mawazon yaliyobora zaidi. Ni vema mtambue kuhamaki si jibu ila jambo jema ni kutoa mawazo yako yaliyobora zaidi. Kama Watanzania tutaifanya kazi hii kwa moyo tutafanikiwa kupata katiba iliyo bora itakalolilea Taifa letu katika miaka 50 ijayo," alisema

  Rais Kikwete, alisema tangu mwaka 1984, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haikuwa na haki nyingi za raia ambapo kutokana na hali hiyo hivi sasa Taifa linahitaji kuwa na katiba ambayo itaingizwa haki nyingi za msingi za Watanzania kutokana na rasilimali zilizopo nchini na zinazoendana na matamko ya umoja wa mataifa.
   
 2. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,750
  Likes Received: 17,828
  Trophy Points: 280
  Kama katuandalia utaratibu mzuri uliojaa kila aina ya ushirikishwaji na wenye kachumbari ya uwazi sasa fujo zitoke wapi. Kinyume na hapo utasikia tu kwenye news ''OKW BOBAN SUNZU amteka nyara mjumbe-mnoko wa katiba katekwa na haijulikani alipo''
   
 3. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Wazanzibari pamoja na harakati zenu zote za kutaka kufanyike kura ya maoni kuhusu muungano mmekwama!

  Sheria ya katiba mpya inawataka mjadili namna ya kuboresha muungano na si vinginevyo. Hivyo kama hamuuhitaji muungano andaeni hoja zenu baada ya kupitishwa kwa katiba mpya kwa sasa mtaonekana wahaini na mtachukuliwa hatua kali za kisheria!

  ZANZIBAR ITABAKI KAMA SEHEMU YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MIAKA MINGI IJAYO INGAWA MIMI BINAFI SIPENDI. POLE SANA WAZANZIBARI!
   
 4. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Vyombo vya habari vimekariri Kikwete akisema kuwa tume mpya ya katiba haitashughulikia kukusanya na uhalali au uharamu wa muungano. Je kwa wale hasa ndugu zetu wa Zanzibar huu siyo mwisho wa ndoto zao za kujitenga? Je huu si msaada mkubwa kwao?
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Alikuwa anatania tu for sure, huwezi kujadili Katiba bila kujadili muungano. Muungano ni sehemu ya Katiba.

  Kama alikuwa serious aliposema hayo basi inabidi arudi kwenye drawing board na atafute jinsi ya kufuta sheria hiyo.
   
 6. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  SOURCE TZ DAIMA

  Rais jk kashatunga katiba anayoitaka kwani keshatoa mwongozo hakuna atakaye hojiwa juu ya swala la Muungano

  Sasa nini maana ya uhuru wa kutoa maoni mbona yale matwakwa mengine ya watu flani hakuyaweka wazi
   
 7. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  jk anapata tabu sana! Kanumba angekwepo tungemwomba atengeneze filamu iitwe JK empire!
   
 8. C Programming

  C Programming JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2,750
  Likes Received: 1,786
  Trophy Points: 280
  mkuu......unakumbuka mjadala wa katiba mpya.......karimjee hall zile vurugu hadi watu wakapigwa na kuumizwa na hakuna aliyekamatwaa
   
 9. l

  lum JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 343
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hahahaha namuheshimu sana rais kikwete lakini kwa WAZANZIBAR suala kuwa tusijadili kuukataa muungano ni kichekesho na hivyo vyombo vya dola ss tumezoeaaa. kwa tarifa yake yy na wote wenye mawazo km yake zanzibar inaondoka na atakee jaribu kutumia nguvu kuzuia anatia nchi katika mgogoro mkubwa na anaunda tanganyika na zanzibar zenye uhasama mkubwa huko mbele(majirani mmaadui).kashidwa mreno kaondoka,muuingireza kaondoka,muarabu kaondoka hee tanganyika kazidi nn asiondoke. we will never sale ZANZIBAR by any price. haturundi nyuma ng'o fikiri kabla kutenda
   
Loading...