JK; "Wanahatarisha Maisha Yao..." | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK; "Wanahatarisha Maisha Yao..."

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MgungaMiba, Jul 2, 2012.

 1. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 891
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 80
  Katika hotuba yake jana, kama nilimsikia vizuri, alisema kuwa Wale "Intern Doctors watakaogoma wanahatarisha Maisha yao..." kwani hivi kweli mtu akikosa ajira ya Serikali ndio maisha yake yako hatarini? Kwani hivi sasa kuna Watanzania wangapi ambao wamesoma na hawana ajira serikalini, ina maana hao wote "Maisha yao yapo Hatarini?" Au alikuwa na maana ya "Hatari" kama iliyompata Dr Ulimboka? (which is the most probable meaning) Au aliteleza ulimi? Kama aliteleza ulimi, basi ni dhahiri kuwa Mind Set yake iko kwenye Kuhatarisha Maisha ya Watakaogoma, bahati mbaya ulimi uliponyoka ukareveal kilichomo kichwani mwake, ni kama siku ile Spika Makinda alipoponyokwa na ulimi wake na kumuita Kiongozi wa Upinzani Bungeni "Mh Mbowe na Majambazi Wenzako!" ingawa alisahihisha baadae lakini tayari imeonesha kilichomo kichwani mwake anavyomuwazia Mh Mbowe.

  Ni dhahiri Mh Rais anayo mawazo ya kuhatarisha maisha ya Madaktari watakaogoma. Just look at this, for Food of Thought, na kubuild Premises kwa hoja ya Rais kuwawazia uovu Drs hao, amekiri kuwa Serikali inatuhumiwa kwa "Hatari" aliyofanyiwa Dr Ulimboka, and yet, badala ya kuunda Tume Huru kuchunguza, ameagiza kundi la Watuhumiwa, (wa Serikali) waende wakajichunguze Kisha wampe taarifa Kama wamehusika ili awachukulie hatua. 2nd Premise ni kuwa ametamka kuwa suala liko Mahakamani na Mahakama ina adhabu zake (ndo maana yule Bibi kule Bungeni kakataza katakata suala hilo lisijadiliwe Bungeni na wala taarifa ya Tume ya Bunge iliyofuatilua suala hilo isisomwe kwa sababu suala liko mahakamani) sasa kilichofanya serikali ipeleke suala hili ni kipi na kilichomfanya yeye aongelee na atoe hukumu ya suala hilo kabla Mahakama haijaamua ni kipi? Kama Madaktari hawakutii amri ya Mahakama ya kuacha mgomo, Mahakama si ina taratibu zake kuwashughulikia wanaopuuza amri zake, yeye kiherehere cha kutoa maamuzi kilimpataje?

  Tukumbuke, Pinda aliwahi kutoa maamuzi Kama haya, matokeo yalikuwa ni nini? Je, na yeye kuamua hivyo ndio maisha ya wagonjwa yatanusuriwa? Hivi kweli serikali ilisha exhaust options zote mpaka kufikia uamuzi huo wake? Mbona ile tume ya Bunge ambayo inaelekea kufanya vizuri pale mwanzo haikushirikishwa safari hii? Au ni kwa vile ameambiwa DHAIFU ndio maana anataka kujitutumua ili aonekane Mbabe? Maamuzi Kama haya mbona hakuyachukua kwa Mawaziri wake waliousambaratisha uchumi wa nchi, mpaka aliposhinikizwa na Wabunge na Waziri Mkuu wake kutishiwa kutimuliwa kwa kura kukosa Imani? Is he Really Serious?
   
Loading...