JK Vunja Baraza la Mawaziri-Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK Vunja Baraza la Mawaziri-Mbowe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, Dec 18, 2009.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Dec 18, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuvunja Baraza la Mawaziri kama njia ya kujipanga upya kukabiliana na ufisadi.
  Rai hiyo imetolewa juzi na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Kwale, Pangani, mkoani Tanga.
  Hata hivyo, Mbowe alisema haoni kama Rais Kikwete anaweza kuvunja baraza kwa nia hiyo kwani mafisadi wanaopaswa kushughulikiwa ni watu wake wa karibu, na ndio walifadhili kampeni zake za urais.
  Mbowe alisema rais anapaswa kuwa mkali na kuwaondoa serikalini baadhi ya mafisadi ambao wamo katika Baraza la Mawaziri. Hata hivyo, hakuwataja majina mafisadi hao.
  Alisema kosa kubwa la Rais Kikwete ni “kucheka na mafisadi”. Aliwataka Watanzania kukasirika na kuchukua hatua wakati wa uchaguzi mkuu ujao mwakani.
  Wakati huohuo, jana chama hicho kimefanikiwa kuzoa wanachama 60 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) jirani na nyumbani kwa Mbunge wa Muheza, Harbert Mtangi.
  Wanachama hao walijiunga na CHADEMA muda mfupi baada ya Mbowe kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Misozwe.
  Mbowe aliwaeleza wakazi wa Misozwe kuwa hakuna haja ya kumng’ang’ania mbunge huyo kwa kipindi cha miaka 10 hadi inafika wakati anajiona kama sultani wa kijiji.
  Alisema hakuna haja ya kufunga ndoa na mbunge au chama na kama wanaona mbunge hawafanyii cha maana wana haki ya kuchagua mwingine tena wa kutoka chama makini cha CHADEMA.
  “Ninyi watu wa Tanga mmefunga ndoa na CCM au mbunge? Mnakaa naye muda wa miaka yote hii na hafanyi mambo ya maendeleo halafu mmemng’ang’ania kujiita eti CCM wakereketwa na huku mkiwa na maisha magumu. Acheni kumfanya mbunge kama sultani,” alisema Mbowe.
  Huku akishangiliwa na wananchi, Mbowe alitoa mfano kuwa kama kijiji kuna duka moja lazima muuza duka ataringa, lakini kama kuna maduka mawili mteja una uwezo wa kuchagua duka na kutoa mfano kuwa CCM ni sawa na duka moja, hivyo wanatakiwa kuongeza CHADEMA liwe duka la pili na kutoa huduma bora kwa wananchi.
  Naye Mbunge wa Viti Maalum, Grace Kiwelu, alieleza kusitikitishwa na kitendo cha Mtangi kuvuta umeme kutoka mjini na kuruka nyumba za wapiga kura wake na kuweka kwenye nyumba yake pekee. Alisema kitendo hicho kinaonyesha ni jinsi gani mbunge huyo asivyowajali wapiga kura wake.
   
 2. b

  bigilankana Senior Member

  #2
  Dec 18, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Akishavunja hilo baraza ndio CHADEMA inapata nini? Wapinzani wa Tanzania jamani wanasikitisha sana. Akivunja anapata sifa ya kuchukua hatua kisha anachaguliwa tena kwa kishindo. Elezeni sera za chama chenu. Hivi toka hawa jamaa wameenda Tanga mmesikia hoja yeyote zaidi ya kelele?
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,910
  Trophy Points: 280
  du hapa kuna utata ,,je hao wananchi wana kipato cha kuwawezesha kujiwekea umeme??
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Dec 18, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wala asilivunje baraza lake! amalize nao tu. Si hagombei mwakani..
   
 5. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Ni wajibu wa mbuge huyo kuwawezesha wapiga kura wake wawe na uwezo wa kujikimu katika maswala muhimu ya kimaisha (basic needs) kama wananchi hawana uwezo huo nani wa kuwawezesha? (bulding capacity). Kwa kuwaruka wananchi wake na kupitisha umeme kwake tu inatuonyesha nini? utawala bora? kwa nini naye asiwe sehemu ya matatizo hayo aishi bila umeme ili atafute suruhisho kwa ujumla? kujiwekea umeme kwake na mkewe ndo maisha bora kwa kila mtanzania aliyoahidi wakati anaomba kura? au kukwepa majukumu yake?

  Tumegundua tatizo moja tu la umeme, je mangapi aliyoyafanya bila kuwashirikisha wapiga kura wake (kuwaruka)? huu ndiyo uongozi bora siyo?
   
 6. b

  bigilankana Senior Member

  #6
  Dec 18, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sio kazi ya mbunge hiyo. huyo kiwelu aliyesema amewezesha nani kupata umeme huko kwao. Siasa za kitoto
   
 7. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbowe ni mzungumzaji mzuri na ni mwanasiasa mwenye akili. Akiendelea na kampeni hizi nchi nzima zinaweza kufanikiwa kupata wanachama na hatimaye kujenga CHADEMA imara. Hata hivyo, kampeni za aina hii zinafaa ziende sambamba na elimu ya uraia kwa wananchi ili wajue haki zao za msingi, kuijua Katiba ya nchi yao na kujua kwamba Serikali inapaswa kuwajibika kwa wananchi.
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Dec 18, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,599
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280

  Asante sana kwa kuliona hilo, ndio utagundua kuwa hivi vyama viko kwa ajili ya maslahi binafsi.

  Mbowe na chama chake ndio walilitaja jina la JK katika list of shame, kuwa naye ni fisadi

  Mbowe anajua fika JK kashindwa nchi hii na miaka hii minne hajafanya lolote juu ya mafisadi

  Mbowe anajua fika kuwa Kikwete kaingia madarakani kwa fedha za EPA na ni fisadi mzuri tu

  Mbowe leo hii anataka atuaminisje JK ni msafi, ila mawaziri wake ndio wabovu, same style with REDET,BBC na akina makamba

  Hii statement imetolewa kujikomba kwa JK, na kama ndio hivyo mjue hakuna upinzania nchi hii, these are NGOs, unless nieleweshwe kivingine

  Mbowe sorry to say this, achilia mbali matatizo ya chama chako na kubaka demokrasia, achilia mbali matatizo yako ya elimu, nashindwa kujua tukuweke wapi katika statement yako hii,this very statement!

  Nikisema mjinga nitakuonea kwani unajua unachofanya, nikisema mpumbavu si kweli maana haukosei unalolitaka

  you are opportunist!!! mjasiriamali nguli
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Akishavunja then awaingize kina nani? toka ashike power amevinja mara ngapi? Faida yake ilikuwa nini hasa?

  - Wote waondoke mara moja, tuanze upya vunja vyama vyote vya siasa, marufuku wote waliowahi kuwa viongozi kugombea tena kwa mujibu wa sheria, tunaanza upyaa!

  - Haya maviongozi hasa magoi goi ni reflection yetu wenyewe wananchi!

  Respect.


  FMEs!
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hongera Mbowe kwa kazi nzuri sana na kwa ajili ya kampeni zote Tanzania na pia yeye ni mzungumzaji mkubwa sana
   
 11. b

  bigilankana Senior Member

  #11
  Dec 19, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi ipi? tupe rekodi yake huyu kijana toka amekuwa mbunge na mpaka sasa. Alitoa hoja gani bungeni. Aliwasilisha hoja binafsi ngapi. Aliwasilisha miswada mingapi alipokuwa mbunge na kazi nzuri kafanya katika chama chake.

  Be precise.
   
 12. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Kweli kiongozi wa "Chama mbadala" amechemka.

  JK akivunja Baraza la Mawaziri watu wataanza kumsifia tena kwa sana tu, wakati siyo ishu, kwani kama kawa ataweka washkaji zake na watu wa RA na EL kwenye nafasi nyeti kama alivyofanya alivyovunja lile baada ya "kujiuzulu" kwa Lowassa.
  Je JK ana nia thabiti ya kuondoa ufisadi? Atamgusaje RA? Si mmemsikia Chikawe anavyotafuta pretext ya kutowashtaki watuhumiwa badala ya kutafuta reasons za kuwakamata?
  Dhamira ya kukomesha ufisadi haipo.

  Akina Mbowe wanapaswa kumkosoa na kuelezea sera mbadala kwa wananchi bila kuchoka na kurudia tena na tena ili wananchi waendelee kuelewa.
  Pia waelezee maamuzi mbadala ambayo wangeyatoa kama wangekuwa ndio wanaongoza Serikali.

  Utendaji usioridhisha wa JK umetoa opportunity kwa viongozi mbadala ila hawajachukua opportunity hiyo kujieleza kwa wananchi, kwa lugha na mifano ambayo wananchi wataelewa.

  Safari ya ukombozi ni ndefu, ila ni muhimu kusafiri.
   
Loading...