Mimi nimezipenda sana nukuu hizi kama nilivyozisoma kwenye gazeti la mwananchi."Kama hatutabadilika katika suala la rushwa mwaka 2015 tutakuwa na wakati mgumu sana na kama mwaka huo tutafanikiwa kuishika Serikali, basi mwaka 2020 hatutarudi tena madarakani. "Najua rushwa ipo na mnaendelea kupokea shilingi laki mbili za airtime (muda wa mawasiliano), ndugu zangu hatutafika ama wengine watavuka na wengine kukwama," , "Viongozi wa chama ndio mmekuwa mawakala wa kusambaza rushwa bila hata aibu. Nawaombeni tubadilike, kama tutaendelea hivi hali yetu itakuwa ngumu sana katika chaguzi mbalimbali, nawaambieni," "Tuna vijana wengi kutoka katika vyuo mbalimbali ambao wanaweza kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu, hivyo hatuna budi kuachana na hawa wala rushwa ambao watatupotezea sifa yetu kwa wananchi"
"Tukipoteza urais ndiyo tumekwisha na chama kinaweza kufa.","Wenzenu wakiendelea kutembelea wanachama na kuitisha mikutano, nyie mnabakia kuimba wembe ni uleule ushindi, shauri yenu mtakatwa,"
"Tukipoteza urais ndiyo tumekwisha na chama kinaweza kufa.","Wenzenu wakiendelea kutembelea wanachama na kuitisha mikutano, nyie mnabakia kuimba wembe ni uleule ushindi, shauri yenu mtakatwa,"