JK Timiza ahadi zako za Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Misenyi na Meli Mkoani Kagera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK Timiza ahadi zako za Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Misenyi na Meli Mkoani Kagera

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanga, Jun 11, 2012.

 1. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ndg wana jf ni wajibu wetu kuendelea kudai na kukumbushia ahadi muhimu kwa uchumi na maendeleo yetu ambazo Rais Kiwete aliahadi wakati anagombea urais kwa awamu ya Kwanza na ya pili lakini mpaka sasa ahadi hizo hazijatelezeka zaidi ya miaka 7 au 2 iliyopita baada ya kuchaguliwa kuwa Raisi 2005/2010
  Katika mkoa wa Kagera JK aliahadi miradi mingi mikubwa na midogo lakini utekelezaji wake ahaupo kama ifuatavyo.
  1.Kujenga uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa katika wilaya ya misenyi 2010 ili kuweza kutumika kwa ajili yawasafiri wa DRC ,Rwanda na Uganda
  2.Kununua na kuleta Meli kubwa kwa ajili ya wananchi kufidia meli ya Butiama iliyozama kwenye ziwa Vicktoria mwaka 1996.
  3.Kujenga barabara ya lami kutoka Bugene-Karagwe kwenda Ngara.
  4.Kujenga barabara ya lami kutoka Karagwe kwenda Murongo mpakani mwa Uganda.
  5.Kujenga barabara ya lami kutoka Kyaka kwenda Kayanga mwaka 2005 ,lakini barabara ujenzi umeanza mwaka jana na umesimama kutokana na kuosefu wa fedha ,wakandarsi wachina wamegoma kuendelea na ujenzi.
  Tuendelee kubainisha ahadi kubwa na muhimu katika maeneo yetu kubaini ufanisi au ujanja ujanja wa JK na chama chake ili wakati wa uchaguzi mwingin giliba na ufisadi wa maneno yadhibitiwe.
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkuu, Mbona jamaa alishakiri kwamba ahadi zake huwa hazitekelezeki!
   
 3. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,882
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  na zile alizoahidi kipindi cha kwanza utawala wake pia tusubiri miaka hii miwili?
   
 4. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,079
  Trophy Points: 280
  Duh! hapo misenyi ndo kwetu, ndo nilikuwa nategemea ajira lakin mpaka sasa naona matokeo yanakuwa sifuri! jk ebu kuwa serious na ahadi zako, tutamtolea mbavuni atakayekuja kuomba urais kupitia chama chako. muda c mrefu mtaumbuka
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,847
  Trophy Points: 280
  imemshinda kujenga bandari ya kimataifa pale wilayani kwake bagamoyo huko ndo ataweza??
  chezea mswahili na porojo wewe.......
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,600
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  zipi? za 2005 au 2010 ?
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Bajeti ya serikali ni trilioni 15 kwa mwaka wa fedha, na ahadi za jamaa thamani yake ni trilioni 96, sasa unadhani zawezaje kutekelezwa? Kwanza alishasahau ahadi alizoziweka!!!
   
 8. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  endeleeni kusubiri tu.
   
 9. n

  naivasha Member

  #9
  Jun 11, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Meli ya MV Bukoba ilizama ziwa Victoria tarehe 21 Mei 1996. MV Butihama haijazama ipo. Rekebisha hapo kwani hata mahakamani wewe waweza shindwa kiurahisi kwa kukosea hoja kizembe. Mhe JK akisema hajaahidi kuwaletea meli badala ya MV Butihama utasemaje?
   
 10. n

  naivasha Member

  #10
  Jun 11, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Meli ya MV Bukoba ilizama ziwani Victoria tarehe 21 Mei 1996. MV Butihama haijazama ipo. Rekebisha hapo kwani hata mahakamani wewe waweza shindwa kiurahisi kwa kukosea hoja kizembe. Mhe JK akisema hajaahidi kuwaletea meli badala ya MV Butihama utasemaje?
   
 11. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,322
  Likes Received: 2,687
  Trophy Points: 280
  Jk hawezi kutekeleza ahadi zote hizo kumbuka hiyo ili kuwa ni aina ya rushwa kwa wapiga kura sasa mngeweza kumpa kura hivihivi.mkono mtupu haulambwi.subirini mpaka mwaka 2015 mtakapo kujakuambiwa kuwa tumeanza kutekereza ahadi zetu hivyo tupeni kura tena ili tumalizie pale tulipoishia. kumbe wajinga ndio waliwao.
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,832
  Likes Received: 10,143
  Trophy Points: 280
  Anajiandaaa kwenda msibani akapumzike pia maana akitoka kwa Saitoti anakwenda kwa Makamu wa Saitoti then labda hadi kipindi hicho Mzee Mubarak atakua naye tayari (maana washaanza kumzushia) kwa hio ataunganisha trip, atakwepa moto wa bunge kidogo
   
 13. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aliwaingiza chaka kwa kuwapa ahadi hewa. Poleni sana watu wa misenye, endeleeni tu kusubiri huo uwanja wa ndege. Imekula kwenu.
   
 14. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Mkuu ni MV Bukoba siyo MV Butiama.
  2. Aliahidi kujenga lami kutoka Kayanga karagwe hadi Benaco Ngara
  3. Aliahidi lami kutoka Ngara hadi Rulenge.
  4. Kuhusu Uwanja wa Missenyi unanichekesha, nilinunua hadi kiwanja kuwekeza pale lakini imebakia historia. Najishangaa mwenyewe. Ha ha ha ha ha ha haaa

  Lakini tumsamehe, hawezi tena kazi hii, atuuzie nchi tu CDM watajenga kwa miaka 3 tu.
   
Loading...