JK, Sikia Hili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK, Sikia Hili!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkereketwa_Huyu, May 8, 2012.

 1. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  JK, sikia hili. Nina wiki sasa toka nifike hapa Burundi na hizi habari za kina Ngeleja na mawaziri wengine wafujaji wa nchi mpaka huku zimeenea na watu wanatushangaa sana mpaka wanadiriki kusema kuwa sie ni watu wa huruma na tutawasamehe tu kwa wizi waliotufanyia. Kingine, mwenyeji wangu akaniuliza, hivi kwa nini Tanzania mtu akipewa ukurugenzi ama uwaziri anafanya pati ya kufa mtu wakati Burundi, Rwanda, Uganda mtu unaogopa kupata hiko cheo? Alinifungua macho na nikabaini kwamba huyo apewaye hayo madaraka anajuwa kuwa ataiba na ile kazi aliyopelekwa kuifanya hatoifanya ila atageuza na kuwa mradi wake yeye mwenyewe huku wananchi anaowatumikia wanakufa njaa. Kwa mtaji huu, kwa nini hawa watu wasitaifishwe na kunyongwa na kuwa fundisho kwa taifa? Kwa nini wenzetu waweze sie tushindwe? Kikwete tafadhali ua hawa watu, hatutaki utuchekee tena tumechoka sasa tunataka vitendo. Nakuja Bongo Alhamisi nikute taarifa ya hukumu imetolewa ili nije kuua mtu, tafadhali nialike.
   
 2. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pamoja!....Tutashinda.
  Siyo Tanzania niujuayo. Watanzania ni wanafiki. Ukipewa madaraka yatumie. Usipoyatumia hata kujiwekea kidogo siku uking'atuka halafu umechapika, mwana utalia. Kwanza watakucheka, watakudharau, watakukebehi na mwisho utakufa na presha halafu utakuwa umeharibu na maisha ya baadaye ya wanao kwani watakosa baba kwa sababu muda mwingi ulipoteza kuwatumikia watanzania wasiokuwa na adabu. Mwendo upo pale pale. Mifano midogo tu, kuna jamaa alikuwa jaji mkuu akaugua, akakosa 10mil kwenda kutibiwa, kaanza kutembeza bakuli, wapi na wapi? Rushwa kwa Tanzania bado ni suala gumu sana kwa sababu watu wake (watanzania) ni wanafiki, wavivu, wambea, waoga n.k...
   
 3. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu sidhani kama uliyemuandikia huu ujumbe atakua amekuelewa unamaanisha nini, kwa sababu yeye mwenyeni ndiye kinara wa huo uchafu wote, in short yeye ndiye jambazi mkuu...
   
Loading...