JK: Serikali haina uwezo wa kutoa huduma za jamii bure | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Serikali haina uwezo wa kutoa huduma za jamii bure

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by sijui nini, Oct 12, 2010.

 1. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete, amesema serikali haina uwezo wa kutoa huduma za jamii bure na amewashangaa wanasiasa wanaopita wakiwadanganya wananchi kuwa iwapo wakichaguliwa watatoa huduma hizo bure.
  Aliyasema hayo jana katika kata ya Mchanngimbore jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma katika siku yake ya pili ya kampeni katika mkoa huo.
  Kikwete alisema serikali ilishajaribu sera hiyo ya huduma bure lakini ilishindwa kwani bidhaa ziliadimika na huduma nyingi zilishindwa kutolewa.
  Alisema licha ya maendeleo yaliyofikiwa tangu Uhuru, Tanzania bado ni nchi maskini na haiwezi kutoa huduma bure kama baadhi ya watu wanavyowaahidi wananchi katika kampeni zao.
  Alisema CCM inaahidi mambo yanayotekelezeka na kwamba imejitahidi kuhakikisha yale yote yaliyoahidiwa mwaka 2005 katika Ilani yake yametimizwa.
  Alisema serikali iliahidi kujenga shule za sekondari kila kata na imefanikiwa kufanya hivyo na sasa kila kata ina shule mbili za sekondari, jambo ambalo awali lilionekana kama haliwezekani.
  Alisema serikali imejitahidi kwa kiwango kikubwa kuboresha elimu ya msingi na sekondari na hivi sasa wanafunzi wengi wanapata nafasi ya kwenda shule tofauti na ilivyokuwa mwaka 2005.

  CHANZO.

  Haya sasa...
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hizi shule za kata anazosema anazifahamu! kweli kwa miaka mitano aliyokaa ndo uwezo wake woote wa kodi zetu umefikia hapo?? jamani PAYEE inauma mpaka namchukia huyu jamaa anaposema haiwezekani, umeshindwa achia wenzio! na hizo VAT zinakwenda wapi sasa!! madini je, wake up!
   
 3. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  sasa si awaachie wanaoona zinawezekana ili na wao wakishindwa ndo tukue kweli haiwezekani...!!
   
 4. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kila kata mbili zina shule ya sekondari.Hilo si dogo.Ni hatua ya kupongezwa.Sasa kilichobaki ni kulinda hizi shule na kuzipatia vifaa na walimu.Hiyo ni hatua inayofuata.Haihitaji Phd kufahamu kuwa ni ahadi iliyotekelezeka.
   
 5. A

  Awo JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Awapishe wanaume wanaoweza kufanya hivyo. Yeye aendelee kusambaza mabango ya biashara!!!! Alaaaaaaaa!!!!
   
 6. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  MILIONI 100 INATOSHA KUJENGA SHULE YA SEKONDARI ILIYOKAMILIKA NA MABWENI, NYUMBA ZA WAALIMU, MAABARA, VYOO N.K. hIVYO BILIONI 133 ZA EPA ZINGEWEZA KUJENGA SHULE 1330 BADO ZA MEREMETA, TANGOLD NA WIZI MWINGINE.

  HAPO UTAGUNDUA KILICHOFANYIKA NI KIDOGO SANA KISICHOSTAHILI KUJADILIWA MAJIUKWAANI NA WATU WENYE AKILI TIMAMU. HATA HICHO KIDOGO KIMEFANIKIWA KUTOKANA NA NGUVU ZA WANANCHI NA SERIKALI KUSHINDWA KUZIPATIA SHULE HIZO VIFAA VYA KUFUNDISHIA, WAALIMU WA KUTOSHA NA VITABU. HII NI KUTOKANA NA UBINAFSI, UCHOYO NA ULAFI WA VIONGOZI WA CCM KUMLIPA MBUNGE MSHAHARA WA KUWATOSHA WAALIMU 30. ) KWA MUJIBU WA SPIKA SITTA MBUNGE MMOJA AALIPWA MILIONI 7.5, ILIHALI MWALIMU WA SEKONDARI ANALIPWA SHILINGI LAKI 2.5 TU.

  NDIO MAANA WATANZANIA WANATAKA MFUMO MPYA WA UONGOZI UTAKAOWEZA KUSIMAMIA MGAWANYO WA HAKI WA RASLIMALI ZA TAIFA TOFAUTI NA ILIVYO SASA.
   
 7. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Tatizo JK hana mikakati ya kitaalam ya kuifanya nchi iwe na uchumi imara, bahati mbaya anachokijua kusimamia kama rais ni kukusanya kodi na kutumia alichokusanya anatengeza vicious cycle.Hana uwezo wa kuibua vyanzo vipya vya mapato ila ana uwezo wa kuibua matumizi mapya kama semina elekezi nguludoto na ku-organize international eco.forum kwa the same kipato.Vyanzo alivyooacha mkapa anaendelea navyo pasi kuibua mpya.Mvivu wa kufikiria anayetegemea washauri kwa 100% HAFAI
   
 8. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hiyo point! Lazima tukubali kuwa inafika wakati wazazi nao wachangie elimu za watoto wao> Hii biashara ya bure bure hii ni tamu sana masikioni lakini utekelezaji wake sio mchezo!

  Fees za aina yote zimefutwa elimu ya msingi, na kila mtoto aliyefika umri wa kuingia shule darasa la kwanza aingie, tena bila ya kulipa chochote, na asirudishwe nyumbani eti kwa kukosa mchango wa madawati, au majengo au whatever - michango yote iwe ni ya kijiji kwa ujumla na sio kwa mzazi/mlezi aliye na mtoto/watoto shuleni. Matokeo yake Tanzania imepata tuzo ya kuwaandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule kwa 95%.

  Kwa sekondari, serikali ya JK imepunguza ada za shule za sekondari za serikali hadi kufikia shilingi 20,000! Vilevile, serikali ilizichukua shule nyingi sana zilizokuwa za private na za kata etc na kuzifanya ziwe za serikali. Changamoto sasa ni kuboresha hizo shule na elimu itokanayo - kweli walivurunda kidogo pale shule za kata zinafunguliwa kumbe walimu wake ndio kwanza wapo chuoni! MUCE na DUCE zikaungana na Mlimani kutoa walimu wenye degreee - DUCE na MUCE ni matunda ya serikali ya Mkapa lakini si ndio hao hao CCM?
   
 9. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  :hand::hand:
   
 10. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  hapo hujaongelea mabilioni ya fedha yaliopotea ambayo yangeweza kutumika kuajiri mamia ya walimu waliochoka na taaluma hii na kuamua kukaa mtaani tu...mpaka ilifika hatua mtu anaona kwenda kusomea ualimu ni kupotea!! HAPANA..BADO CIJAONA!!
   
 11. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ingawa sio utamaduni wangu kukubaliani na Kikwete kwenye kila jambo analolisema/tamka, ila kwenye hili suala la serikali kutoa huduma za jamii bure kwa wananchi, nakubaliana naye 100%. Hakuna kitu inaitwa "free lunch" hapa duniani. Ukiwapatia watanzania huduma za bure, wataendelea kuwa wavivu na wajinga. Achilia mbali kuwa nchi yetu haina uwezo huu.  So true. Nchi yetu bado ni masikini mno. Dr. Slaa anajua hilo, na Lipumba naye anafahamu hilo. And, as much as navyompenda Slaa/Lipumba kwa kile walichokileta kwenye kampeni za mwaka huu, vitendo vya wao kuwaahidi wananchi ahadi zisizotekelezeka, ni vitendo vibaya sana. Kwasababu [basically] wanachokifaya ni kuwajengea wananchi false hopes ambazo zitakuja wawinda kama wakifanikiwa kwenda ikulu
  .
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Sasa kwanini tuendelee kuwachagua hao CCM amba hawana majibu ya umasikini wetu?

  Mbona wageni wanapewa misamaha ya kodi badala ya kuchangia kufuta umasikini?

  Jk grow up you or we will grow you out in October
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Shule tumejenga wenyewe tena kwa kuchanga kwa nguvu. Nakumbuka nimetoa sh 60,000 mtaani na kama 100,000 kwenye biashara yangu. Hana aibu?
   
 14. M

  Masauni JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  So true. Nchi yetu bado ni masikini mno. Dr. Slaa anajua hilo, na Lipumba naye anafahamu hilo. And, as much as navyompenda Slaa/Lipumba kwa kile walichokileta kwenye kampeni za mwaka huu, vitendo vya wao kuwaahidi wananchi ahadi zisizotekelezeka, ni vitendo vibaya sana. Kwasababu [basically] wanachokifaya ni kuwajengea wananchi false hopes ambazo zitakuja wawinda kama wakifanikiwa kwenda ikulu[/COLOR][/SIZE].[/QUOTE]
  Ngoja nikufahamishe tu ndugu yangu, whatever you believe whether negative or positive will come to pass. Ukiamini wewe ni maskini ndivyo itakavyokuja kuwa. kwa maana hutaweza kusjishughulisha, hutaweza kubuni mambo mbalimbali kwa hiyo akili yako itawaza kimaskini(itakuwa domant) kamwe hutaweza kuwa na maono makubwa. Raisi wa nchi akiamini kuwa nchi yake ni maskini ndivyo nchi itakavyokuwa, Raisi huyo hatakuwa mbunifu, hawezi kuona utajili uliopo, matokeo yake raisi atakuwa anawaza kimaskini maskini tu. Wananchi hawawezi kuwa na maono makubwa ya kuondokana na umaskini kwa sababu Kiongozi wao kashawaaminisha kuwa wewe mtanzania ni maskini tu. Watanzania ebu tuondokane na hiyo dhana mbaya.
   
 15. M

  Masauni JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK ni mjinga kabisa Kuiba mabilioni inawezekana lakini Elimu ya bure ya mamilioni haiwezekani!!!! Kweli watanzania tu wajinga na wavivu wa kufikiri . Thanks God Mungu amenipa hekima sidanganywi na mwizi wa pesa ya UMMA.
   
 16. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni vizuri kuwa wamesema haiwezekani, so wapumzike waone jinsi chadema watakavyoweza. Maana wao wameshindwa. Ahsante
   
 17. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Jakaya ni yeye binafsi kusomeshwa bure na fweza za walipa kodi sasa hataki wenzake wasomeshwe bure kama yeye AIBU!
   
 18. M

  Masauni JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Harafu kinachoniudhi ni CCM kudhani watanzania wote ni mabwege. Naomba niulize nchi hizo zinazotoa elimu ya bure ziliwezaje? Zamani hao wakina kikwete walisoma bure je, nchi ilikuwa tajiri au maskini?
   
 19. K

  King kingo JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haina maana kama CCM wameshindwa kutoa elimu bure na afya bora kwa watanzania basi wengine wanaweza kushindwa, akili za CCM sio za chadema, kinachohitajika ni utashi wa kisiasa tu. CCM wawaachie wengine waongoze ili wawaonyeshe ni jinsi gani haya mambo yanawezekana kwanini wanang'ang'ania????
   
 20. A

  August JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hivi ccm au serekali nani mwenye kipato kikubwa zaidi? mbona ccm wameweza kuwavisha watanzania t-shirt na kofia bure? itakuwa serikali kulipia mtoto shule ambaye atakuja kuongeza tija? au ni bora kuilisha familia za viongozi vizuri ili wasile rushwa lakini mwisho wa siku wana kula hiyo rushwa?
   
Loading...