JK, Rais wangu unacheza mchezo wa hatari sana...

JK, Rais wangu unacheza mchezo wa hatari sana...

Chezea chama cha majanja,kitaibuka na kitu mtashangaa kimetokea wapi.Na kitapita tu mtake msitake.Sasa wako kilingeni kinawaangalia mnavyokwenda ovyo,hivi mtu kutoka Bunambiu anaelewa mabadiliko ni kitu gani?
 
Kwa historia ya nchi hii, hakuna Rais aliyefanikiwa kuwachagulia watanzania Rais wanayemtaka. Rais Marehemu ndugu Julius Kambarage Nyerere alitamani angetuchagulia Salimu Ahamad Salimu, akashindwa, wananchi wakamchagua mzee Ruksa Ali Hassan Mwinyi. Mwinyi pia alikuwa na chaguo lake, lakini naye kama mtangulizi wake Nyerere, akashindwa. Mr Clean Mzee William Benjamin Mkapa akaukwaa uraisi tena pasi na kuuhitaji. Mkapa naye akatamani mrithi wake angekuwa siyo Kikwete, lakini hali kadhalika naye akazidiwa na Wanamtandao waliokuwa wakimkampenia Kikwete akina Kingunge Ngombale Mwilu.
Nina imani kwa 100% Kikwete hajamtuma EL kwa mashekh wa Bagamoyo ila hii ni mbinu ya kimkakati ya EL mwenyewe ili kuwahadaa wananchi waamini kuwa kuna baraka za Rais wakati siyo kweli. Ikiwa ni kweli basi hii ni hofu tu ya Kikwete kuwa huenda, kwa nguvu zake EL anaweza akaupata urais na akiupata tu atatumia kiti chake pia kumkandamiza Raisi Mstaafu Kikwete. Ukizingatia kuwa Kikwete ana madudu mengi aliyoyafanya akiwa Rais na Edward Ngoyai Lowasa alivyo na visasi. Hofu inayompata Kikwete ndiyo hofu iliyompata Mkapa wakati wa kumptisha Kikwete. Sielewi ni kwa nini ubabe alioutumia kumzuia Mzee John Malechela hakuutmia pia kumzuia Kikwete.
Kama kweli Edward Ngoyayi Lowasa atapitishwa na CCM KUPEPERUSHA BENDERA YAKE YA URAIS KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2015 itakuwa kwa sababu uwoga wa viongozi wa juu wa CCM kuogopa kivuli cha Lowasa, kutaka kulindwa baada ya kustaafu na mimba ya Rushwa waliyopewa naye hivyo lazima wamzalie mtoto-URAIS. Hamna kitu kingine
Nimeyatazama haya maneno ya EL na ule ujumbe toka "msoga" kisha nimetambua kuwa JK anacheza mchezo wa hatari sana.
 
Back
Top Bottom