JK ni kiboko! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ni kiboko!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng`wanakidiku, May 5, 2012.

 1. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi Dr Haji Mponda na Dr Nkya walikuwa na kiburi toka wapi wakashindwa kuwasikiliza madakitari? Hivi walikuwa hawafahamu kuwa Dr JK alikuwa anapata information toka ndani kabisa ya jopo la madakitari kupitia mwanae Salama ambaye ni dakitari? Nadhani walipaswa waache kumdanganya Rais, watekeleze matakwa ya madakitari ili kuepuka hii aibu iliyowakumba. Nampenda JK kwa hili maana kama ni kisasi wala huwezi ukajua yeye ndiye aliyeamua "Ni kamati kuu" ya CCM, eti!!?
  [​IMG]
  Madaktari wafurahia Dk Mponda, Nkya kuondolewa
   
 2. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,906
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  Nimeikubali staili ya JK, ukivurunda usisubiri kuambiwa.
  Pima upepo wa kisiasa, na changanya za zako mwenyewe!!!
   
 3. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  JK ni mzee wa kukwepa lawana. Pale tunapoonaga kwamba anachelewa kufanya maamuzi, ni kwamba anakuwa anatafuta mtu wa kutupiwa lawama kwa maamuzi atakayoyafanya.
   
 4. C

  Claxane Senior Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapa kama yuko kwenye taarabu vidole juu akalime mpunga na bado mahakamani atatinga
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu jizuie kuchambua mambo kishabiki.
  Matatizo ya Dk Mponda ni ya kisiasa na kiutawala na si criminal, unless una habari kachota mahali, weka ukweli hadharani.
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  kweli ndo aina ya raisi tuliye nae sasa!
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Serikali ipi ya kumpeleka mahakamani? Labda baada ya hii ya kukwepa lawama na bora liende!!
   
 8. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  waishukuru CC ya gambaz
   
 9. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni mawazo mgando kufikiri matatizo ya sekta ya afya yataisha kwa kuteua viongozi wapya wa wizara. Kama una akili timamu utatambua kuwa matatizo mengi ya nchi hii ni zao la mfumo mbovu wa usimamizi wa rasilimali, rushwa, ubadhirifu, uchama, taifa kukosa mwelekeo kimaendeleo, ubinafsi namaadili mabovu
   
 10. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Shine, kwa nyeti nyepesi nyepesi watendaji wote watachukuliwa hatua, kwa mfano sasa hivi kwenye halmashauri moto unawaka kinoma. Na kule nadhani ndiyo kunawezi sana na ndiyo hao unaowaona wanasomesha watoto wao academy na kuendesha magari ya kifahari huku wanapita barabara za vumbi. Nadhani ktk hili Rais tumuunge mkono hata kama wewe ulifaidika au unafaidika, tutafute njia mbadala ya kujiwezesha kiuchumi na siyo kuwa wezi kwani hii inaharibu hata ukuaji wa uchumi.
   
 11. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukiwa baba au mama nyumbani kwako "hakuna demokrasia" haswa africa. Maana hakuna atakayekuwajibisha (Haswa africa). Ila kwenye serikali ukikosea unawajibishwa na sauti ya uma kupitia hao waliokupatia dhamana. Mabadiliko yaliyofanywa yanaweza angalau kutoa matumaini ya nini kifanyike kwani Dr Mponda aliwahi kusema " Hawajibiki kwa Ma Dr, bali kwa wapiga kura wake" Na Dr Nkya aliwashawaambia ma Dr hawezi kukutana nao kisa kajichagulia ukumbi. Sasa kwa akili yako unadhani hawa ambao hawakuwa baba wala mama wa ma Dr wangeachwa hivi hivi? Unaweza kuwambia wanao hualipii karo na wakakushitaki na ukawalipia sembuse kiongozi? mfumo uliopo ni mbaya ila wa kuurekebisha ni mimi na wewe kupitia kura.
   
 12. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka hii ni mara ya 2 katika awamu hii baraza linafanyiwa mabadiliko makubwa kutokana na kashfa za ubadhirifu na ufisadi, tulitarajia baada ya Richmond mawaziri wangekua waadilifu lakini hii ni awamu nyingine ya kureshufle ulaji bata...hakuna jipya
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  May 5, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Yaani kuondolewa kwa mawaziri 6 na manaibu 2 imechukua siasa nzima ya uwajibikaji kwa kupindisha ukweli kwamba mawaziri hao walitakiwa kujiuzuru ama kuachishwa mapema. JK kweli amekomaa kisiasa kuchezea vichwa vyenu, sasa namkubali kwamba ni Politician. Na ndio maana alisema haya ni mambo ya upepo tu yatapita, leo nawaona Wabongo wote wamekenua meno kurafurahia baraza jipya la mawaziri ambalo kati ya mawaziri na manaibu wake sijui 60, asilimia 90 wamerudi kazini kama kawa. JK kawapiga bao la kisigino - JK kiboko kweli.
   
 14. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni tatizo sugu. Kibaya kwa Tanzania yetu kila kiongozi ni mwizi! Nadiriki kusema hivyo kwa sababu nilishashuhudia. Ukijifanya huibi wenzako wanakuchokngea live au wanakufanyia fitina unakufa. Hili la rushwa ni gonjwa la taifa, we tizama halmashauri zinavyotafunwa. Mfano kuna mzee mmoja alikuwa afisa mipango pale morogoro basi akaondoka kwenda shule, akamuachia kijana ashike nafasi yake, mzee wa watu karudi ili akabidhiwe kijana akakataa kabisa kumkabizi kisa alikuwa amefanya ufisadi wa hali ya juu, ikabidi mzee amuache kijana kwani ilionekana anasapoti ya watu wa juu. Na bahati mbaya muda wa kustaafu mzee ulikuwa umefika. Na mpaka sasa huyo kijana mwizi (nadhani anaitwa John) yupo anaendelea kukaimu. Sasa kama wizi upo kwenye grass root tufanyeje???? Nadhani watanzania tunapaswa kuelewa tatizo na kushauri, na kwa hatua iliyopo kwa sasa ya kuwachukulia hatua watendaji labda itazaa matunda, otherwise tunahitaji CDM waingie mtamboni watuendeshe. Ni kama Phillipine, yule mama alikuwa kama CCM, mwizi wa mali na kura, sasa jamaa wamechkua nchi na mambo yao yameanza kunyooka, na huyo mama alipata kibano (kama ambavyo Mkapa na JK watakavyokuja kupata hapo baadaye) mpaka sasa yupo hoi mara eti naumwa! Jamaa wanamuambi pumbavu ulifilisi nchi...?? unataka kwenda wapi? Suluhisho ni Kura!
   
 15. richard.nzemya

  richard.nzemya Member

  #15
  May 5, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tehetehe,napita tu
   
 16. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kiongozi asiyependa kunyooshewa mkono
   
 17. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wasalimie
   
Loading...