JK na ziara zake kwenye Wizara

taffu69

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,094
538
Kuna taarifa kuwa leo JK ameanza ziara kutembelea wizara zote. Kubwa nililoshuhudia ni msongamano wa magari kipindi cha mchana kwenye maeneo ya katikati ya jiji wakati alipokuwa anatoka Wizara ya Fedha kwenda Ofisi za Mamlaka ya Mapato na kilichotokea ni magari kushindwa kutembea kwa zaidi ya saa nzima.

Jambo la kujiuliza ni kama ziara anazofanya zinaongeza tija katika utendaji na ukuaji wa uchumi wetu ama ndiyo ile ilimradi siku imesogea.

Kama ni muhimu kukutana na watendaji wa hizo wizara, haiwezekani watendaji hao kwenda Ikulu mna kutoa taarifa husika badala ya JK kuanza kuzunguka kila kona na msururu mkubwa wa magari jambo linalosababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa jiji kwa ujumla?
 
Sio msongamano barabarani hata huko bandarini kazi zimesimama
 
Kipindi kile Makamba akiwa Mkuu mkoa DSM, basi ndo alikuw wa kufukuza arudi kijijini kwao.
Kwenda wizarani uta achieve nini, anasaini kwenye kitabu cha wageni, sijui anaulizia kazi zinaendeleaje, sjui anakagua makambrasha ya malipo ya wafanyakazi hewa, tenda hewa, kongamano na warsha hewa na .... sijui approach yake ikoje?
Na anaridhika kuwa sasa amemaliza wizara ya miundombinu, elimu, fedha sasa naenda wizara ya nishati....sijui atahoji bado hamjanunua mitambo ya dowans?
Ni kama katuni za Tom&Jerry.
 
Kuna taarifa kuwa leo JK ameanza ziara kutembelea wizara zote. Kubwa nililoshuhudia ni msongamano wa magari kipindi cha mchana kwenye maeneo ya katikati ya jiji wakati alipokuwa anatoka Wizara ya Fedha kwenda Ofisi za Mamlaka ya Mapato na kilichotokea ni magari kushindwa kutembea kwa zaidi ya saa nzima.

Jambo la kujiuliza ni kama ziara anazofanya zinaongeza tija katika utendaji na ukuaji wa uchumi wetu ama ndiyo ile ilimradi siku imesogea.

Kama ni muhimu kukutana na watendaji wa hizo wizara, haiwezekani watendaji hao kwenda Ikulu mna kutoa taarifa husika badala ya JK kuanza kuzunguka kila kona na msururu mkubwa wa magari jambo linalosababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa jiji kwa ujumla?

Hajui afanyalo. Alipoingia awamu ya kwanza aliwaita hadi wakuu wa wilaya akawapa eti semina elekezi. Matokeo yake ni nini zaidi ya kuongeza ufisadi na kutumia pesa ya serikali bure kwa semina ambazo hazina tija. Mwache azidi kututesa.
 
Jana alikuwa wizara ya fedha then akaenda TRA, alipata kusikiliza kero za wananchi wateja wa huduma za TRA bt cha ajabu hakuzitolea majibu!
 
Kufuatia JK kuanza Ziara za kutembelea Wizara na Taasisi mbalimbali za Umma kuangalia utendaji kazi na performance kwa ujumla, inahisiwa kuwa idadi ya wachangiaji kwa kipindi hiki itashuka kufuatia wale walioko katika public service kujifanya wako busy na ujengaji wa Taifa wakihofia wasije kutwa wakiwa busy na JF, twitter, fb nk.
Wacha sie tusio waajiri wa jk tuvinjari-Any time, any where we are in touch!
 
kuwa busy kutoa michango humu JF ni kazi kubwa sana na tena ya kuleta maendeleo kuliko kazi hizo za maofisi ya public service.....!
 
Huyo jk ndo anajifanya yuko busy .... hajui hata priority zake ni zipi.
Anapoteza resources nyingi sana kwa ziara zake za kipuuzi zisizo na tija. Ina maana ameshindwa kupata feedback kutoka kwa watendaji wake akiwa ofisini kwake hadi akapotezee watu muda wa kufanya shughuli zao?
Just imagine manhours lost : kufunga barabara na kusababisha watu kushindwa kuendelea na majukumu yao; pia watu wanaondamana naye ni wengi na hawafanyi chochote isipokuwa kuunga bogi.
Na maofisini hukuo aendapo ana disrupt shughuli zote ili watu wamsikilize.
Anaemzuga hasa ni nani ili aonekane ni mfuatiliaji kumbe ni mzembe tuu. Pathetic !!
 
mkuu....nashukuru kwa kuwakilisha fikra zangu pia
 
JK kutembelea ofisi za Wizara zilizoko DSM haisaidii na wala hawezi kuona ufanisi ulivyo kama anasahau Ofisi za wizara mbalimbali zilizoko mikoani na wilayani. Ni ahibu kukuta ofisi za erikali Wikani na mikoani wafanyakazi wanatumia mabenchi kama viti vya ofisini. Afike huko ajionee nchi yake anayoiendesha.
 
Kufuatia JK kuanza Ziara za kutembelea Wizara na Taasisi mbalimbali za Umma kuangalia utendaji kazi na performance kwa ujumla, inahisiwa kuwa idadi ya wachangiaji kwa kipindi hiki itashuka kufuatia wale walioko katika public service kujifanya wako busy na ujengaji wa Taifa wakihofia wasije kutwa wakiwa busy na JF, twitter, fb nk.
Wacha sie tusio waajiri wa jk tuvinjari-Any time, any where we are in touch!

Mkuu Nani kakwambia, kwani anakuja kwenye Laptop yangu? isitoshe ni siku moja kwa wizara na tupo ktk wizara mbalimbali.. Hatutishiki na hilo, usihofu kazi tunachapa na jf tunachangia!
 
My Boss ameshapiga marufuku JF ofisini kwani kampuni hii imefaidika na ufisadi wa EL
yaan ukifumwa tu lazima umtajie ID yako hapohapo na ole wako uwe umemkandia EL
 
mkuu.... sasa unafanyeje
 
Back
Top Bottom