Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Tangu ccm imalize mkutano wake wiki jana, kumeibuka staili mpya ya chama hiki katika kuendesha siasa zake!
Chama kimeamua kuchukua nafasi ya serikali, kinazindua miradi ya maendeleo ya nchi, kinatoa karipio kwa watendaji wa serikali, kinawapa maagizo mazito mawaziri,
Na zaidi kinapita nakuwapa ahadi mpya wananchi utadhani ni serikali mbadala ya Tz!
Hivi katiba ya nchi inaruhusu Kinana kutoa leseni za madini? Mbona ni kazi ya wizara husika?, katiba inamruhusu kumshurutisha Muhongo, Kagasheki, Mwakyembe, au Mwambungu?
Katiba inamruhusi Nape kumkaripia Said Mwema?
Naomba wadau tuangalie kwa pamoja katiba inasemaje hasa marekebisho yake yaliyozaa mfumo wa vyama vingi inasemaje juu ya vyama na serikali?
Leo tukiwachekea tutakuja kustuka Nape na Kinana wakipangua baraza la Mawaziri kwa maagizo ya Mwenyekiti wao!
Lazima kuwe na mstari wa kugawa kati ya majukumu ya chama na serikali.
Chama ni msimamizi wa serikali kiliyoiunda tu, kitoe ushauri huko sio kuingilia utendaji wa serikali!
Serikali ni ya WANANCHI haina chama haina itikadi kwamjibu wa katiba iliyopo na ijayo daima!