JK na CCM wamevunja KATIBA ya NCHI?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,977
20,243
Tangu ccm imalize mkutano wake wiki jana, kumeibuka staili mpya ya chama hiki katika kuendesha siasa zake!

Chama kimeamua kuchukua nafasi ya serikali, kinazindua miradi ya maendeleo ya nchi, kinatoa karipio kwa watendaji wa serikali, kinawapa maagizo mazito mawaziri,

Na zaidi kinapita nakuwapa ahadi mpya wananchi utadhani ni serikali mbadala ya Tz!

Hivi katiba ya nchi inaruhusu Kinana kutoa leseni za madini? Mbona ni kazi ya wizara husika?, katiba inamruhusu kumshurutisha Muhongo, Kagasheki, Mwakyembe, au Mwambungu?

Katiba inamruhusi Nape kumkaripia Said Mwema?

Naomba wadau tuangalie kwa pamoja katiba inasemaje hasa marekebisho yake yaliyozaa mfumo wa vyama vingi inasemaje juu ya vyama na serikali?

Leo tukiwachekea tutakuja kustuka Nape na Kinana wakipangua baraza la Mawaziri kwa maagizo ya Mwenyekiti wao!

Lazima kuwe na mstari wa kugawa kati ya majukumu ya chama na serikali.

Chama ni msimamizi wa serikali kiliyoiunda tu, kitoe ushauri huko sio kuingilia utendaji wa serikali!

Serikali ni ya WANANCHI haina chama haina itikadi kwamjibu wa katiba iliyopo na ijayo daima!
 
Leo tukiwachekea tutakuja kustuka Nape na Kinana wakipangua baraza la Mawaziri kwa maagizo ya Mwenyekiti wake!

hili nalo neno
 
we umedundua leo, hata bungeni waziri mkuu alitoka tamko rasmi kwamba wakuu wa mikoa na wilaya ni makada wa chama so ni ruksa kufanya kazi za uhamasishaji na ujenzi wa chama --- aka kuhakikisha ccm inashinda chaguzi zote ndani ya wilaya / mikoa yao
 
Wale ni watendaji wa umma, ukada wao upo kwenye chama chao tu!

Tuzingatie katiba tusiseme kama ni mazoea tu, CCM inavunja katiba ya nchi waziwazi!
 
Tangu ccm imalize mkutano wake wiki jana, kumeibuka staili mpya ya chama hiki katika kuendesha siasa zake!

Chama kimeamua kuchukua nafasi ya serikali, kinazindua miradi ya maendeleo ya nchi, kinatoa karipio kwa watendaji wa serikali, kinawapa maagizo mazito mawaziri,

Na zaidi kinapita nakuwapa ahadi mpya wananchi utadhani ni serikali mbadala ya Tz!

Hivi katiba ya nchi inaruhusu Kinana kumshurutisha Kagasheki, Mwakyembe, au Mwambungu?

Katiba inamruhusi Nape kumkaripia Said Mwema?

Naomba wadau tuangalie kwa pamoja katiba inasemaje hasa marekebisho yake yaliyozaa mfumo wa vyama vingi inasemaje juu ya vyama na serikali?

Leo tukiwachekea tutakuja kustuka Nape na Kinana wakipangua baraza la Mawaziri kwa maagizo ya Mwenyekiti wao!

Lazima kuwe na mstari wa kugawa kati ya majukumu ya chama na serikali.

Chama ni msimamizi wa serikali kiliyoiunda tu, kitoe ushauri huko sio kuingilia utendaji wa serikali!

Serikali ni ya WANANCHI haina chama haina itikadi kwamjibu wa katiba iliyopo na ijayo daima!

Utakiambia nini CHAMA cha KIMUNGU? Toka lini CHAMA sio SERIKALI wanagawa

Leseni kwa Wachimba MADINI??? HIYO NI KOSA KIKATIBA; Ni Sawasawa na RAIS KIKWETE anavyoitisha VIKAO vya CCM-NEC; CCM-CC IKULU DAR

** NI kununua WAPIGA KURA? Wamuulize Mr. ROMNEY alitumia 2 BILLION DOLLARS kununua kura na bado alishindwa na Wapiga KURA MASIKINI wanaojali HAKI zao na SIO MAPESA ya KUMWAGA au KOFIA; KHANGA; SCAFU na VINGI...

A.-Kinana-akikabidhi-leseni-kwa-wachimbaji-wadogo-machimbo-ya-MugusuGeita-leseni-21-zimetolewa-1024x687.jpg

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi leseni za wachimbaji wadogo machimbo ya Mugusu, Geita, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mkoani Geita. Jumla ya leseni 21 zilikabidhiwa kwa wachimbaji hao baada ya kutolewa na serikali ili kuwwezesha wachimbaji wadogo nao kunufaika na madini badala ya wachimbaji wakubwa tu.
 
Mwanangu Yericko Nyerere tatizo la Bongo si CCM bali kuzuka utawala wa kisultani wa Jakaya Kikwete. Kesho utamsikia mkewe hata mwanae nao wakitoa maagizo. Kulikuwa na uzi humu ukiuliza mke wa makamu wa rais anafungua miradi kama nani? Sasa tunakabiliwa na utawala balaa badala ya utawala bora. Tuna walaji tunaowaita viongozi. Kiongozi gani asiyejua mipaka ya mamalaka yake? Kiongozi gani asiyeongoza bali kujifanyia madudu bila kujali kuna kesho? Ni balaa kweli kweli.
 
Wameona kuna ombwe la kiutawala dhaifu amedhoofika mno kwa hiyo wanaturudisha enzi za chama kushika hatamu.
 
Utakiambia nini CHAMA cha KIMUNGU? Toka lini CHAMA sio SERIKALI wanagawa

Leseni kwa Wachimba MADINI??? HIYO NI KOSA KIKATIBA; Ni Sawasawa na RAIS KIKWETE anavyoitisha VIKAO vya CCM-NEC; CCM-CC IKULU DAR

** NI kununua WAPIGA KURA? Wamuulize Mr. ROMNEY alitumia 2 BILLION DOLLARS kununua kura na bado alishindwa na Wapiga KURA MASIKINI wanaojali HAKI zao na SIO MAPESA ya KUMWAGA au KOFIA; KHANGA; SCAFU na VINGI...

A.-Kinana-akikabidhi-leseni-kwa-wachimbaji-wadogo-machimbo-ya-MugusuGeita-leseni-21-zimetolewa-1024x687.jpg

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi leseni za wachimbaji wadogo machimbo ya Mugusu, Geita, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mkoani Geita. Jumla ya leseni 21 zilikabidhiwa kwa wachimbaji hao baada ya kutolewa na serikali ili kuwwezesha wachimbaji wadogo nao kunufaika na madini badala ya wachimbaji wakubwa tu.

Daaaaaaah mkuu umeongeza maumivu yangu ya moyo!

My god! Yani haya utayaona tanzania tu!
 
Mwanangu Yericko Nyerere tatizo la Bongo si CCM bali kuzuka utawala wa kisultani wa Jakaya Kikwete. Kesho utamsikia mkewe hata mwanae nao wakitoa maagizo. Kulikuwa na uzi humu ukiuliza mke wa makamu wa rais anafungua miradi kama nani? Sasa tunakabiliwa na utawala balaa badala ya utawala bora. Tuna walaji tunaowaita viongozi. Kiongozi gani asiyejua mipaka ya mamalaka yake? Kiongozi gani asiyeongoza bali kujifanyia madudu bila kujali kuna kesho? Ni balaa kweli kweli.
Mzee wangu,

Inaniuma sana kuona wanatuendesha watakavyo!
 
Leo tukiwachekea tutakuja kustuka Nape na Kinana wakipangua baraza la Mawaziri kwa maagizo ya Mwenyekiti wake!

hili nalo neno

Kama sijakosea ni kwamba chama kinachoshinda uchaguzi ndio kinaunda serikali, kwahiyo serikali iliyopo ni ya CCM
kwa maana hiyo basi CCM kuamrisha viongozi wa serikali yake ni kama baba kumuongoza kijana wake hamna shida!!

Hayo ni mawazo yangu tu ya ujumla, sijaingia saana katika katiba.....
 
haya mazoea yana mipaka na kwanini uruhusu mazoea yakutawale hadi uzeeni changes begins with you nani atakukomboa kama sio mwenyewe kujifunga mkanda mkuu,
 
Ni kweli chama kinachoshinda ndicho huunda serikali, lakini pale kimalizapo tu kuunda serikali hiyo basi huwa ni serikali ya WANACHI.

Chama kinabaki kuwa msimamizi wa ndani ya chama tu, kinatolea ushauri au karipio ndani ya chama tu,

Hakitakiwi kutoka na kuingilia serikali ya wananchi, kiwasimamie mawazi wake huko ndani ya chama sio nje ya chama,

Waziri anapokuwa nche ya chama ni waziri wa wananchi wote, yani TLP, CHADEMA, CUF, nk

Ila akiwa ndani ya ccm ni mwanachama mtiifu

Majukumu ya chama yameainishwa vema kwenye katiba ya nchi, na majukumu ya serikali vivyohivyo yameainishwa!

Kuna mipaka maalumu na hawapaswi kuingiliana kwa namna yoyote ile!
 
haya mazoea yana mipaka na kwanini uruhusu mazoea yakutawale hadi uzeeni changes begins with you nani atakukomboa kama sio mwenyewe kujifunga mkanda mkuu,

Bravooo! Umenena sana mkuu, chagizo kuu la kimageuzi
 
Daaaaaaah mkuu umeongeza maumivu yangu ya moyo!

My god! Yani haya utayaona tanzania tu!

Sipati picha viongozi wa ANC wanapofanya kazi za mawaziri...Hili la CCM ni kituko aisee, yaani ndio kusema hizi leseni cha uchimbaji madini mdogo kama sio mwanaCCM huwezi kupata? Hili si ni jukumu la Watendaji wa Serikali hili, sasa hapa CCM imehusikaje? Elimu ni muhimu, lakini ELIMU YA URAIA INAHUSIKA ZAIDI HAPA, hCCM wameamua kufanya ujangili kweupe namna hii? Hatari sana hii
 
Tangu ccm imalize mkutano wake wiki jana, kumeibuka staili mpya ya chama hiki katika kuendesha siasa zake!

Chama kimeamua kuchukua nafasi ya serikali, kinazindua miradi ya maendeleo ya nchi, kinatoa karipio kwa watendaji wa serikali, kinawapa maagizo mazito mawaziri,

Na zaidi kinapita nakuwapa ahadi mpya wananchi utadhani ni serikali mbadala ya Tz!

Hivi katiba ya nchi inaruhusu Kinana kutoa leseni za madini? Mbona ni kazi ya wizara husika?, katiba inamruhusu kumshurutisha Muhongo, Kagasheki, Mwakyembe, au Mwambungu?

Katiba inamruhusi Nape kumkaripia Said Mwema?

Naomba wadau tuangalie kwa pamoja katiba inasemaje hasa marekebisho yake yaliyozaa mfumo wa vyama vingi inasemaje juu ya vyama na serikali?

Leo tukiwachekea tutakuja kustuka Nape na Kinana wakipangua baraza la Mawaziri kwa maagizo ya Mwenyekiti wao!

Lazima kuwe na mstari wa kugawa kati ya majukumu ya chama na serikali.

Chama ni msimamizi wa serikali kiliyoiunda tu, kitoe ushauri huko sio kuingilia utendaji wa serikali!

Serikali ni ya WANANCHI haina chama haina itikadi kwamjibu wa katiba iliyopo na ijayo daima!

CCM wanajisahau wanahisi wapo kwenye mfumo wa chama kimoja!
 
Kama kuna jambo lilinishitua, basi ni hili la kinana kutoa lesseni za uchimbaji madini kwa kweli hapa ndo sijaelewa kitu kabisa. Nafikiri haya ndo matokeo ya nchi kuongozwa na serikali dhaifu.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom