JK kwanini uliwadanganya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK kwanini uliwadanganya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by frozen, Nov 9, 2011.

 1. frozen

  frozen Senior Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuna maneno mengi yanayosemwa kuhusu siasa..oh siasa mchezo mchafu, oh siasa hili. Kifupi mimi nlikuwa mmoja wa watu niliye mkubali jk ktk uchaguzi wa mwaka 2005. Japokuwa sikuwa na taarifa zake nyingi katika utendaji wake kabla ya kugombea uraisi, katika kampeni zile kwa lugha yake ya upole na kwa kutotumia lugha kali na ahadi tele za kuwapa watanzania maisha bora nikamwona mtu muungwa ambaye anania ya dhati ya kuwakomboa watanzania.

  Lakini baada ya kipindi chake cha miaka mitano nikapata picha halisi ya JK kama ni mtu mnafiki na anayeweza kutumia lugha yake vema na sura yake kulaghai wananchi wake, na mtu ambaye anakiburi na jeuri ya chini chini na vijembe vilivyo jificha.

  Katika uchaguzi wa mwaka jana bwana huyu alitumia picha mbalili mbali kulaghai watu, kama utakumbuka kulikuwa na mabango lukuki ya kimuonesha akiwabeba watoto, akiwasaidia wakinamama kuwabebesha ndoo za maji, akisalimiana na walemavu..na picha nyingine nyingi zikimpambanua kama mtu anayejali, na kweli akapata kura kutoka kwa akina mama, walemavu na wadanganyika wengine.

  Ni kweli kuna mazuri mengi umefanya lakini jk, unaiua Tanzania kmya kimya, inawezekana unajua hili au haujui,mambo ya udini yanayozungumziwa leo mwanzilishi wake ni wewe, migomo ya wanafunzi,walimu, na wafanyakazi yaliyotokea na yanayokuja mwazilishi wake ni wewe, angalia kilichotokea igunga na mabo yako ya kujivua gamba, mabilioni ya pesa yakatumika katika uchaguzi ule pasipo sababu yoyote ya msingi, na unafiki uliofanywa na viongozi kuwapata wadanganyika wawachague watu wapate ulajo..

  Angalia kinachotokea arusha leo, inawezekana haujali lakini ipo siku tu hutaamini sumu hii uliyoleta itakapo kurudia. Watu wamechoka na wanahasira kwa kuwadanganya na kuwafanya kuwa watoto wadogo. Uungwana kama mambo huwezi waachie wengine, au omba msaada usaidiwe au kili kushindwa usaidiwe na sisi wananchi tutakuelewa ndugu badala ya kutupeleka kama gari bovu.

  Hakika kila chenye mwanzo huwa na mwisho,yuko wapi gadaffi,mmbaraka wa misri na viongozi wengine ambao walikuwa wanajiona wao ni Mr Right? hakika Tanzania inamatatizo mengi sana kwa sasa na nchi ipo ipo tu mpaka tunapewa masharti ya ajabu ajabu tu kupewa misaada.

  Hasira zote juu ya serikali yako, ni kwa sababu ulitudanganya, ulijifanya Masiha wakiti wewe hauna uwezo huo, kwa nini uliwadanganya JK?
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  maandamano, migomo ya wafanyakazi na wanafunzi, machafuko ya arusha mwanzilishi ni JK au CHADEMA? Mbona unaongea kinyume? Katika haya kosa la JK nini au kuwa kimya huku akiona CHADEMA wanafanya vurugu, wakivuja sheria za nchi?. Mimi labda nimalaumu Rais wetu kwa kujifanya mjinga kana kwamba hajui kinachofanywa na CHADEMA. Hakuna rais katika nchi hii atakaevumilia uchafu kama huu unaofanywa na CHADEMA. Mimi nadhani hata CHADEMA wenyewe wanaumia kuona wanamchokoza Rais ila hachukui hatua, wangefurahi kuona Rais anachukua ahatua ili wapate cha kusema kwamba wameonewa. Hivi Polisi wangemaua kuchukua hatua stahiki kwa Chadema wangepata wapi mwanya wa kuandamana, kufanya mikusanyiko isiyo ya lazima? RAIS KIKWETE wapuuze hao na sisi WANANCHI tumeshawapuuza.
   
 3. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Umeongea vizuri saana Mkuu,kwa kweli WATANZANIA tunaumia saana ktk mambo mengi mno,lakini nasisitiza IPO SIKU JK NA WENZIO mtabeba maumivu yetu.
   
 4. frozen

  frozen Senior Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  jk alichaguliwa kuja kuongoza watanzania na sio kukaa kimya. chadema sidhani kama wanachofanya ni fujo ila ni kudai haki au kutokubali kufanywa wajinga. mambo mangapi yanatokea katika nchi hii na ya msingi ambayo raisi kama kiongozi wa nchi anatakiwa ayatolee maelezo au kutoa final say yeye anakaa kimya,au anashangaa tu au hajui, hichi kama si kiburi au dharau ni nini? yanayotokea nchini hasa arusha ni dalili kama watu wamechoka na stahili hii ya uongozi wake na wanaona kuna kila dalili kwamba mambo yamemshinda lakina anaghumia chini chini na kukataa kukili kwamba mambo yame mzidi ndo mana nchi inaenda enda tu. nchi ni ya watanzania wote nayeye alipewa dhamana tu ya kuongoza na anatakiwa kutupa majibu nini hakipo sawa katika nchi yetu tujuwe.
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Jk kaza butu wewe ndiye Rais wa wote waliokuchagua na ambao hawakukuchagua wale ambao hawakukuchagua wasubiri kuchagua Rais wao 2015. hakuna Rais hapa Tanzania ambaye aliondoka bila kundi moja kulalamika hata mwalimu tunayeamini ndiye rais msafi hadi sasa wapo ambao hawakuridhishwa na uongozi wake, vivyo hivyo Mwinyi na Mkapa ambaye alikalibia kufungwa kwa maneno maneno
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee kikwete hoyeeeeeeeeeeeee
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280


  labda nikukumbushe tu.
  Chadema ni mfumo kamili unaomilikiwa na Watanzania wazawa kwa mamilioni. mmoja wapo ni mimi ambaye nilishajiapiza sitaiunga mkono system ya ccm mpaka naingia kaburini.
   
 8. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  "Hakuna jambo baya kama kujutia kura yako uliyopiga kwa mtu asiye sahihi,nafsi itakusuta tu"
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wewe ni Kihiyo plus masaburi na elimu ya kata na njaa uliyo nayo .Sheria zipi zinavunjwa ? wanacho fanya Chadema si juzi juzi Kigangala naye kasema hakubali ?Au wewe unakurupuka tu ?
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  sio bure umetumwa
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  kama ningesema chadema hoyeeeeeeeeeeeeeeee mbowe hoyeeeeeeeeeeee hapo sikutumwa
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wewe mwenyewe umetumwa kuniambia mimi nimetumwa kumbe wote tumetumwa
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  utakuwa ni mpuuuzi namba moja tanzania kama unadhani kikwete hana shabiki hata mmoja sio lazima nitumwe kama ninavyoamini hujatumwa na mbowe
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  tatizo lako unadhani ni makosa kuwa mfuasi wa kikwete basi hujui maana ya siasa za vyama vingi kama ni hivyo tufute vyama kibaki CCM peke yake kama zamani
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kama chadema hawakuvunja sheria na polisi hawakuvunja sheria ngoma bila bila
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  kama ulipiga kura kwa mtu asie sahihi usijute subiri uchaguzi mkuu ujao utapata aliye sahihi akujengee na nyumba
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nani kasema kikwete anahitaji kuwa Rais wako? kama hukumpa kura yako una haki ya kutubu ulukosea sana
   
Loading...