JK kupewa Uwaziri wa Michezo kwasababu ya kutokuwa na umakini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK kupewa Uwaziri wa Michezo kwasababu ya kutokuwa na umakini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BornTown, Sep 14, 2010.

 1. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Lipumba: Kikwete amekosa umakini Monday, 13 September 2010 20:22 0diggsdigg

  Elias Msuya, Masasi

  MGOMBEA wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba amesema kukosekana kwa umakini kwa mtetezi wa nafasi hiyo kupitia tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete, ndiko kulikomsababishia ashindwe kuwawajibisha watuhumiwa wa ufisadi wakiwemo mawaziri na watendaji wa serikali yake.

  Profesa Lipumba aliyasema hayo juzi, alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Masasi, mkoani Mtwara.

  Alisema Kikwete ni mtu wa mzaha hata katika mambo mazito na kwamba hali hiyo amekuwa nayo tangu akiwa chuoni.

  "Huyu mgombea urais wa CCM namfahamu tangu tukiwa chuoni. Nikiingia Ikulu nitamfikiria walau kumpa uwaziri wa Michezo na Utamaduni maana hawezi kufanya majukumu mengine nyeti," alisema Profesa Lipumba.

  Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba alieleza kusudio lake la kufuta mfumo wa ununuzi wa mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani, ambao amesema unamnyonya mkulima.

  Alisema zao la korosho halimnufaishi mkulima kwa kuwa linauzwa kwa mfumo huo alioeleza kuwa ni kandamizi kwa watu wa kipato cha chini.

  "Mkulima analazimishwa kuuza korosho zake kwa mfumo wa stakabadhi ghalani. Kilo moja ni Sh800 lakini, anakatwa ushuru wa gunia, unyaufu na pembejeo. Halafu mkulima hapewi fedha yote bali hupewa Sh 400 kwanza hiyo nyingine inshaalah. Mungu akipenda ndiyo analipwa," alisema.

  Alisema kama ataingia madarakani ataufuta mfumo huo na kuwaruhusu wakulima wauze korosho zao kwenye masoko yenye faida na yasiyokuwa na ukiritimba.

  Kuhusu ajira, Lipumba aliponda takwimu za serikali zinazosema kuwa CCM imetengeneza ajira zaidi ya 1.3 milioni.

  "Ajira wanazozungumzia wanaziita za sekta binafsi. Yaani vijana wanavyozunguka na kuuza bidhaa kwenye stendi za mabasi ndiyo ajira za CCM.

  Kule Dar es Salaam, kuna wanaookota chupa za maji na kuziuza. Hiyo nayo CCM imeijumlisha kwenye ajira zake milioni moja," alisema Lipumba.

  Profesa Lipumba pia aliubeza Mpango wa Maendeleo ya Shule za Sekondari za kata (MMES), akisema hauwezi kusaidia kuboresha elimu kwa kuwa hakuna walimu wa kutosha wala vifa vya kufundishia.

  "Kuna shule moja nimeikuta huko Lindi ina walimu watatu na wote wanafundisha masomo ya Kiswahili na kiingereza. Mmoja wao ametoka shule ya msingi hana uwezo wa kufundisha," alisema.

  "Shule hizi zimejengwa kwa ajili ya walalahoi lakini, vigogo wanapeleka watoto wao kwenye shule za English medium ili waje kuwatawala watoto wa maskini," aliendelea kusema profesa Lipumba.

  Awali akiingia katika mji wa Masasi, msafara wa mgombea huyo ulipokelewa kwa msafara mkubwa wa pikipiki na bajaji huku wafuasi wa chama hicho wakilisukuma gari lake.

  Katika jimbo hilo, CUF wamemsimamisha Clara Mwatuka atakayepambana na Mariam Kasembe wa CCM.
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,924
  Likes Received: 12,130
  Trophy Points: 280
  Hili nalo neno.
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kama hayupo makini mi naona angeazia kwenye Udiwani.
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  [​IMG]

  Rais Sarkozy akiwa kwenye Mazoezi

  [​IMG]

  [​IMG]

  Rais Kikwete naye akiwa kwenye Mazoezi!
   
Loading...