JK kumfuturisha Sheikh Sharif leo huku Bunge likijadili Mafuta!

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya leo, Jumanne, Agosti 9, 2011, amempokea mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Somalia, Mheshimiwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ambaye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais Kikwete. Baadae jioni leo, Rais Kikwete atamfuturisha mgeni wake ikiwa ni baada ya mazungumzo rasmi. Futari ya Rais Kikwete na Sheikh Sharif pamoja na mazungumzo rasmi ya kiserikali yatafanyika Ikulu jijini Dar es salaam. Rais huyo wa Somalia ataondoka kesho jumatano kurejea kwao.

My Take: Futari ya Rais JK na Sheikh Shariff inafanyika huku Taifa likiwa katika kizungumkuti cha shida ya mafuta na huku serikali ikiwa haijatoa kauli yoyote kwa wiki zima sas!!!!!

Hakika kikwete ni kilaza sana,nilimcheki jana mpaka nikaona kinyaa kwa alivyoongea

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya leo, Jumanne, Agosti 9, 2011, amempokea mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Somalia, Mheshimiwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ambaye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais Kikwete. Baadae jioni leo, Rais Kikwete atamfuturisha mgeni wake ikiwa ni baada ya mazungumzo rasmi. Futari ya Rais Kikwete na Sheikh Sharif pamoja na mazungumzo rasmi ya kiserikali yatafanyika Ikulu jijini Dar es salaam. Rais huyo wa Somalia ataondoka kesho jumatano kurejea kwao.

My Take: Futari ya Rais JK na Sheikh Shariff inafanyika huku Taifa likiwa katika kizungumkuti cha shida ya mafuta na huku serikali ikiwa haijatoa kauli yoyote kwa wiki zima sas!!!!!

ungetumia font ndogo pia ungeeleweka!

kwa kweli kama ni raisi tunaye, C ZANI KAMA ATATOKEA RAISI KAMA KIKWETE HAPA DUNIANI, KIKWETE NI WA KIPEKEE SANA.

HIZO GARAMA ZA KUFUTURISHA WATU NI KODI ZA WATANZANIA? AU NI MAPATO KUTOKA ILE HOTEL YA BILILA KULE SERENGETI?

BARA LA AFRICA LINA VIONGOZI WENGI SANA WAISILAAMU BUT C JAWAHI SIKIA WANAFUTURISHA WATU IKULU.

KAMA KUNA IKULU AMBAYO HAINA HADHI HAPA DUNIANI NI YA TANZANIA, IKULU YA TZ NI KAMA UKUMBI WA BUNGE LETU KILA SIKU WAGENI WAKWENDA KUUZA SURA

Ni kuwa hata Dodoma jioni hii limetolewa tangazo kuwa makamu wa pili wa rais wa Zanzibar atakuwa anafuturisha wabunge , sasa umeme ukikatika ingekuwa poa ili wakumbuke kuwa pamoja na masuala ya imani bado wana wajibu wa kuutekeleza kwa taifa.

Kikwete ndiyo zake, yeye mambo magumu huwa hataki kuyagusia ila tu, starehe na burudani kama hizi utamkuba .Acha tu ajiuze kwa majirani

Kuna public relations disaster inaendelea hapo Magogoni. Nahisi mtu wa mawasaliano/public relations hapo Ikulu hajaelewa nini hasa malalamiko ya watu huku mtaani. Na kwa maoni yangu tatizo sio kwamba watu wanataka wamuone rais akiwa na watu wa kawaida, viongozi wa dini au hata watoto yatima, ila wanataka AONGOZE nchi. Asimamie sheria na utendaji wa idara za serikali. Hizi picha za futari zingekuwa na maana tu kama mambo yalikuwa yanaenda sawa huku mtaani. Lakini kumuona rais anapakuwa kuku na wali na maandazi wakati umeme hakuna, mafuta/petrol hakuna, uchunguzi kuhusu michango ya Jairo haujulikani umefikia wapi na huku UDA imeuzwa, ni error of judgement.

Badala hizi endless picha za futari wangeweza hata kumshauri rais atembelee kituo kimoja cha mafuta! Siku 7 sasa raisi hajaongea kuhusu mafuta lakini kila kukicha tunaona picha mpya za futari. Nirudie kusema safu wa washauri ikulu inaonekana kutojua hali halisi na hivyo kumshauri rais visivyo. But again, nani aliwaweka hao washauri Ikulu?

Napita tu...lakini akili zetu zipo pahali pake kweli? I doubt! Labda zko kule alikosema Masaburi

Kikwete ndiyo zake, yeye mambo magumu huwa hataki kuyagusia ila tu, starehe na burudani kama hizi utamkuba .Acha tu ajiuze kwa majirani

Ukisikia kashfa dhidi ya uislamu ni kauli kama hizi. Funga ni Ibada katika uislamu na nguzo, leo ishakuwa starehe na burudani?

By the way Mkapa alikuwa akifuturisha Ikulu hiyo hiyo. Lakini kubwa zaidi ingekuwa mwezi wa kawaida huyo mgeni si ange kirimiwa chakula cha jioni ? sasa badala yake kuwa futari ndio ishakuwa nongwa kodi zetu zinatumiwa vibaya?

Acheni chuki wakristo

naanza kukosa imani na JF. Nadhani ipo haja ya kuwa tunataja basi umri baadala ya kuandika ID feki. Ili kusudi mtu ukiona post unaangalia na umri ndo unachangia. Watua hapa wanaandika baadae ndo wanafikiria walichokiandika. Pumba tupu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya leo, Jumanne, Agosti 9, 2011, amempokea mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Somalia, Mheshimiwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ambaye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais Kikwete. Baadae jioni leo, Rais Kikwete atamfuturisha mgeni wake ikiwa ni baada ya mazungumzo rasmi. Futari ya Rais Kikwete na Sheikh Sharif pamoja na mazungumzo rasmi ya kiserikali yatafanyika Ikulu jijini Dar es salaam. Rais huyo wa Somalia ataondoka kesho jumatano kurejea kwao.

My Take: Futari ya Rais JK na Sheikh Shariff inafanyika huku Taifa likiwa katika kizungumkuti cha shida ya mafuta na huku serikali ikiwa haijatoa kauli yoyote kwa wiki zima sas!!!!!

We kweli ni kuku!! Mawazo yako kama ya ya kuku anayefuta mdomo kabla hajamaliza kula. Pumba tu umeandika hapa.

Ni kuwa hata Dodoma jioni hii limetolewa tangazo kuwa makamu wa pili wa rais wa Zanzibar atakuwa anafuturisha wabunge , sasa umeme ukikatika ingekuwa poa ili wakumbuke kuwa pamoja na masuala ya imani bado wana wajibu wa kuutekeleza kwa taifa.

Unless sijui ila nijuavyo futari/kufuturu ni suala la kiimani zaidi kuliko kiserikali. Ni muhimu viongozi wetu, hasa wa juu kabisa kama rais, makamu, au waziri mkuu wakawa makini kutokugeuza masuala yao ya kiimani yaonekane kama ya kiserikali; well, pengine ni "ukarimu" wa kitanzania, lakini inaweza leta shida huko mbele ya safari. Tafsiri zinaweza kuwa tofauti miongoni mwa wananchi.

kwa nini Tanzania tu? Dunia nzima Tanzania ndo kuna viongozi waislamu? mbona huko kwingine hawafuturishi watu kihivyo? Alikuwa JK, keo Makamu wa Raisi, kesho kutwa utasikia Pinda naye.
na hizo tukumbuke c hela za mfukoni mwao, ni kodi za walala hoi hoi hizo

Jamanieeeeeee Raisi ofisi yake iko ikulu makzi yake pia yako ikulu sasa wageni wake awapokelee wapi ??? Na futari je afuturie wapi kama sio IKULU ????

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya leo, Jumanne, Agosti 9, 2011, amempokea mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Somalia, Mheshimiwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ambaye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais Kikwete. Baadae jioni leo, Rais Kikwete atamfuturisha mgeni wake ikiwa ni baada ya mazungumzo rasmi. Futari ya Rais Kikwete na Sheikh Sharif pamoja na mazungumzo rasmi ya kiserikali yatafanyika Ikulu jijini Dar es salaam. Rais huyo wa Somalia ataondoka kesho jumatano kurejea kwao.

My Take: Futari ya Rais JK na Sheikh Shariff inafanyika huku Taifa likiwa katika kizungumkuti cha shida ya mafuta na huku serikali ikiwa haijatoa kauli yoyote kwa wiki zima sas!!!!!

We kilaza kweli, so kwa sababu hakuna mafuta basi watu wasifuturu???

Jamanieeeeeee Raisi ofisi yake iko ikulu makzi yake pia yako ikulu sasa wageni wake awapokelee wapi ??? Na futari je afuturie wapi kama sio IKULU ????

Safi; Ikulu ni ofisini na nyumbani kwake afuturu haina shida. Lakini kuna sababu gani kutuonesha kwenye vyombo vya habari kwamba rais sasa anafuturu? Makamu rais sasa anafuturu; waziri mkuu sasa anafuru? Sidhani kama kuna umuhimu wa wananchi kujua mambo hayo.

ama kweli birds of the same feathers flock together..huyu rais wa somalia wananchi wanakufa na njaa yeye anafunga safari hana tofauti kabisa na mwenyeji wake jk.

Back
Top Bottom