Dr Matola PhD
Platinum Member
- Oct 18, 2010
- 61,558
- 109,091
hayo maandamano yamepunguza makali ya maisha? Wahimize wananchi kufanya kazi. Mbona hawaelezi serikali nini cha kufanya maisha yawe bora.Baada ya maandamano na mikutano huko mwz,bukoba,mara,shy, je maisha yamebadilika? Huu si muda wa kampeni,waacheni wananchi wafanye shughuli zao.Slaa anakipeleka vibaya chama watu washamchoka kila siku kasema hili mara lile,utekelezaji zero.
Dos Santos! usilete propaganda katika ishu serious kama hii waache CDM waandamane ni haki yao kikatiba na unavyofikiria wewe kuhusu uchu wa madaraka uko wrong, na elewa kwamba JK sasa yuko katika hali tete alifikiri kuongoza inchi ni mchezo sasa ameona ikulu sio sehemu ya masikhara na hii yote ni kutokana na presha anayoipata kutoka CDM, na elewa kwamba kazi kuu ya upinzani ni kuikosoa serikali sio kujipendekeza pendekeza kama wale wenzetu wa vyama vingine.
nakukumbusha: siku ya hotuba ya JK mwisho wa mwezi Februari. alisema haya kuhusu tatizo la umeme nchini, Tarehe 15 Februari, 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa TANESCO wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme. Baraza limeitaka Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha kuwa mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi. Aidha, imesisitizwa kuwa pamoja na udharura uliokuwepo sheria na taratibu za manunuzi ya umma vizingatiwe. Pia, wahakikishe kuwa mkataba wataoingia uwe ni wenye maslahi kwa taifa. Vile vile, watoa huduma wawe ni makampuni yanayofahamika na yenye sifa stahiki na kuaminika.
Hapo kwenye red, ina maana siku zote JK alikuwa anaelewa kuwa mikataba ya IPTL,RICHMOND,SONGAS,NET GROUP haikuwa na maslahi kwa wananchi, na hili amelisema baadae ya maandamano ya CHADEMA kanda ya ziwa, sassa mimi nakushangaa sana unaposema CDM wanapoaandamana wanaleta uasi na kuonekana wana uchu wa madaraka. Tumia akili yako vizuri sio kuleta upupu usio na maana yoyote na kwa taarifa yako ujinga unaoongea humu JF huwezi kuongea mtaaani nadhani utachomwa moto aua utapokea matusi na kipigo juu.
maisha magumu mpaka watu waambiwe ni magumu? Kwani watu hawayaoni? Mbona Rais JK ktk hotuba yake amekiri kwamba maisha ni magumu.CDM wakiwahutubia watu maisha ni magumu ndo yanabadilika au kuwapotezea watu muda wa kuhangaikia maisha yao yawe mepesi. Maandamano hayana tija kwa mtz,ila ipo ajenda ambayo wewe huijui unafuata mkumbo. Kama hamkueleweka ktk kampeni ndo mtaeleweka sasa
SONGAS,IPTL,NETGROUP,kawaulize wenzio rais alikuwa nani? Tatizo mkumbo. Inaonekana hukusiliza hotuba,umehadithiwa au umeamua kupotosha kama ilivyo kawaida yenu
maisha magumu mpaka watu waambiwe ni magumu? Kwani watu hawayaoni? Mbona Rais JK ktk hotuba yake amekiri kwamba maisha ni magumu.CDM wakiwahutubia watu maisha ni magumu ndo yanabadilika au kuwapotezea watu muda wa kuhangaikia maisha yao yawe mepesi. Maandamano hayana tija kwa mtz,ila ipo ajenda ambayo wewe huijui unafuata mkumbo. Kama hamkueleweka ktk kampeni ndo mtaeleweka sasa
Hakuna sababu ya CDM kuomba serikali ya Mseto kama CUF kwani mbona ushindi upo nje nje tu bila hata ya kuwa kibaraka kama Seif! ushidi ambao utakuwa wa K.O...CCM mnalo hilo mkijaribu kuchomoa mmekwisha
Ndoto ya madaraka. JK hana sababu ya kukutana na cdm. Kwa kipi hasa,wachochee watu kufanya uasi halafu watake mazungumzo na Rais.Hawana jipya waendelee na maandamano mazungumzo ya nini. Na wao wanataka kuingia serikalini kama cuf.Waendelee kupost thread humu JF
Yani inaonyesha JF kuna watu wanaanzisha topic za kuwapa wana JF wenzao hasira,halafu hao wenzao wanaonyesha wanavyokerwa na jambo hilo,then wanakuwa wamepunguza hasira........Bahati mbaya hakuna wa kujibu(ambaye ni CCM)........SIo mbaya......JF ni sehemu nzuri ya kupooza hasira dhidi ya CCM,kama ilivyo kwa wananchi wa Tokyo na siasa za Kijapan wanavyoshauriwa kuwa na picha za viongozi wao majumbani mwao,na wakishikwa na hasira wazifanyie chochote kuondoa hizo hasira eg kuzitemea mate,kuzipiga mateke,kuzitukana nk,hahahahahahaaaMkuu hata hiyo serikari ya mseto hatuitaki,nini No Preconditions!!
hakuna mjadala wala suluhu hapa.
SONGAS,IPTL,NETGROUP,kawaulize wenzio rais alikuwa nani? Tatizo mkumbo. Inaonekana hukusiliza hotuba,umehadithiwa au umeamua kupotosha kama ilivyo kawaida yenu
Watakuwa wanajidanganya sana kama watakutana na Chadema kwa kudhani hili ni tatizo la Chadema, mimi nawashauri waanze na kina Mgaya wa TUCTA kwanza waelewane na waongeze mshahara stahiki ( sababu nina ushahidi wa kutosha kwamba pesa hizo zipo na nchi yetu ni tajiri ).
2. wakutane na vyama vya wamachinga wajue matatizo yao halisi na sio kuwajengea machinga complex
3. wahakikishe wote wanaowasababishia maisha magumu Watanzania wanashughulikiwa mara moja bila kuacha chembe ya shaka.
4. Lianzishwe jukwaa huru la vijana wasio na hajira ( na sio vijana watoto wa vigogo) hapo pawe ni chumbiko la mijadala ya kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana.
Zipo sababu nyingi nimetoa mawazo yangu tu kwa uchache, lakini kama kuna mpuuzi ambaye anadhani tatizo ni CHADEMA anajidanganya, kwangu mimi Chadema naona ni kama starter tu ya kuamsha hasira za watu waliokata tamaa ya maisha na hambao hawana cha kupoteza, maana duniani hawapo na peponi hawapo, je watu hawa wako wapi? mtu anaota ndoto amekufa kwa wiki mara tatu unadhani mtu mwenye maisha bora huwa anaota ndoto za kufakufa?
Ndg yangu Slaa hana mamlaka yoyote yeye sio Raisi wa nchi, kama unataka afanye mwambie JK aachie ngazi ili CDM iingie kazini uone mafisadi kama watabaki!!!! Lakini anao uhuru wa kuwaelimisha watu waishinikize serikali itimize wajibu, hasa kuwakamata wezi wa fedha lukuki za umma. Mbona hapo hugusi tukisema wezi????????? Wewe ni nani, kwa mtu mwenye uelewa kama wewe naona kuna kitu unaficha au ni mwajiliwa wa wezi hao!!!!!!!!Wewe huna kabisa uchungu wa nchi kufilisiwa na kuachwa utupu?????????Eti CDM ikae tu ikiangalia, lazima waseme hata ingalau wezi washituke wajue tunawaona kasoro wanalindwana watawala!!!!!!!!hayo maandamano yamepunguza makali ya maisha? Wahimize wananchi kufanya kazi. Mbona hawaelezi serikali nini cha kufanya maisha yawe bora.Baada ya maandamano na mikutano huko mwz,bukoba,mara,shy, je maisha yamebadilika? Huu si muda wa kampeni,waacheni wananchi wafanye shughuli zao.Slaa anakipeleka vibaya chama watu washamchoka kila siku kasema hili mara lile,utekelezaji zero.
No preconditions.
JK Kama Rais, nina hakika anayajua matatizo yote haya. Hivyo basi kwa usalama wa nchi yake na Chama chake sidhani kama amekaa tu ametulia. No! He is doing something, let us give him time after the elections and see what will happen. We learn through misktakes. Give him a second chance. Mpaka amefika hapo alipo (Rais) sidhani kama anaweza kukaa bila kutafuta suluhu ya kero zilizopo. Hiyo Ari ZAIDI, nguvu ZAIDI na kasi ZAIDI ni tofauti na Ari MPYA ....... ipeni muda kidogo hiyo ZAIDI, inaweza ikaleta matunda. Yeyote afanyaye kosa, akishaligundua hulirekebisha. Ukimsakama wakati yuko katika process ya kulirekebisha, unamvunja nguvu na ku-disturb process zake. Mnapowapump wananchi na maneno ya kuichukia Serikali, Je hao watendaji wanapowatembelea kwa ajili ya kufuatilia maendeleo si mnataka wazomewe? Hiyo itawapa nguvu kweli? Mi kwa upande wangu namsupport sana Rais wetu, namwombea afya njema na mafanikio katika jitihada zake. Namhurumia anavyosakamwa. kuongoza nchi sio mchezo jamani.