JK kufuta tatizo la maji Simanjiro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK kufuta tatizo la maji Simanjiro

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gerad2008, Oct 25, 2010.

 1. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Naye Kikwete, akiwa Simanjiro mkoani Arusha, pamoja na mambo mengine, aliahidi kutafuta Sh30 bilioni kwa ajili ya kumaliza tatizo la maji kwenye jamii ya wafugaji.
  Akizungumza kwenye viwanja vya makao makuu ya Wilaya ya Simanjiro, Orkesumet, Kikwete alisema serikali yake ijayo pia itatoa ruzuku ya dawa ya josho za ng’ombe kwa wafugaji.“Jitihada za awali za tatizo la maji tayari zimeelezwa na mbunge wenu (Christopher Ole Sendeka), lakini serikali inajipanga kumaliza kabisa tatizo hilo," alisema Kikwete na kuongeza:
  “Tunahitaji kuwa na Sh 30 bilioni kwa ajili ya kuvuta maji kutoka mto Ruvu na huu ni mradi mkubwa ambao mipango ya awali ya kuomba fedha imeshaanza.”
  TLP kuwashughulikia matajiri
  Naye mgombea wa TLP, Muttamwega Mgaywa amehitimisha kampeni zake mkaoni Dar es Salaam kwa kutangaza kuwashughulikia mafisadi.
  Alisema iwapo atachaguliwa kuwa rais atahalikikisha kila mfanyakazi wa serikali aliyejenga nyumba yenye thamani inayofikia Sh300 milioni, atajieleza ameijengaje.
  "Nitakapoingia madarakani ukinunua gari la Sh70 milioni tutakuomba ujieleze umeinunua kwa fedha kutoka wapi, ukisomesha watoto kwa Sh3 milioni hadi 5 milioni tutakuuliza umetoa wapi," alisema Mgaywa.
  NCCR- Mageuzi 'walilia' posho za mawakala
  NCCR-Mageuzi imesema Tume ya uchaguzi (NEC) ina jukumu la kuwalipa posho mawakala wa vyama vya siasa watakaoshiriki katika zoezi la usimamizi wa kura za wagombea katika uchaguzi mkuu.
  Mkurugenzi wa kampeni na uchaguzi wa NCCR-Mageuzi, Faustin Sungura aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa chama chake kimeshtushwa na taarifa iliyosambazwa na Nec kuwa haiwajibiki kuwalipa au kuwapa posho mawakala wa vyama vya siasa.
  Alisema hatua hiyo ni kukiuka wajibu wake wa kupanga, kusimamia na kuendesha uchaguzi katika misingi inayowezesha uchaguzi kuwa huru na wa haki.


  Habari hii imeandaliwa na Salim Said,Musa Mkama,Hussein Kauli Joyce Mmasi,Gedius Rwiza, Mussa Mkama, Kizitto Noya, Simanjiro na Julieth Ngarabali, Pwani
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Kufuta tatizo la maji siyo sawa na kufuta maandishi ya penseli.

  hizo porojo za kuombea kura tu
   
Loading...