JK kipenzi cha Watanzania aliyegeuka Chukizo mbele yao

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
16,817
Reaction score
62,027
Nchi hii imewahi kuwa na makundi makuu mawili ya watu waliopendwa sana na Watanzania, Nyerere, JK na Magufuli. kundi la pili ni la Mrema na Lowasa.

Nyerere alipendwa sana sababu ya kupigania uhuru, kutumia vipawa vyake vya akili na uongozi kwa ajili yao. Huyu alifanya makosa kadhaa ya kiuongozi, na hata mwishoni mwa utawala wake wake hali ya maisha ilikuwa ni ngumu sana, lakini wananchi walimfeel kuwa huyu anapambana kwa ajili yao, walimpenda hivyohivyo na kumheshimu sana.

JK yeye ana sifa nyingi sana za ubinadamu,ni mcheshi, siyo arrogant, anajua urafiki kama wewe ni rafiki yake, siyo katili. Hizi sifa ziliwafanya Watanzania wampende. Tatizo lake kuu ni kuwa amekuwa highly irresponsible kwenye mambo makuu ya msingi ya Taifa. Kwa mfano, kwa nini baada ya kutumia mabilioni ya kodi ya wananchi kwa ajili ya katiba mpya aliuacha huo mchakato hewani unaelea?. Kwa nini anashiriki kubaka taratibu za chama cha mapinduzi katika kupata uongozi wa nchi?, Kwa nini anaiacha familia yake ionekane ya kilafi?, mke mbunge, mtoto waziri, na mke anapeleka bungeni hoja za wake wa viongozi walipwe mshahara, what a disgrace!.

Sasa katika vitu vilivyowafanya wananchi wawe na hasira kali ni mambo kama haya, mtu badala atambue kuwa yeye amewahikuwa rais wa nchi hii, na anaangaliwa na Taifa kama statesman yeye anaonelea awe "Kingmaker" ndani ya CCM, aendelee kuwa relevant kwa walioko madarakani yaani kiufupi anajihisi comfortable kuwa CHAWA PRO MAX wa mtu aliyekalia kiti badala ya kuangalia future ya Taifa. Hili limekuwa chukizo kubwa kwa wananchi.

Mtu aliyeko karibu na JK amwambie tu, kuwa yeye kimaumbile is a good guy. Aaachane na hizi cheap endeavors za kutaka upendeza mbele za mtu aliyeko kwenye kiti, au kujaribu kutafuta influence ya hapa na pale za kuwa actor behind the scene. Asimame kama statesman, awe moral pillar wa nchi hii kama akina Jaji Warioba.

Mtu una mihela mingi uliyochuma tangu ukiwa kijana na marupurupu kibao ya pensheni, una mijumba kedekede, sasa unataka nini tena?.
 
Mcheza ngoma mahiri ni yule anayejua ni wakati gani wa kuondoka stejini
 
Wa Tz ni wanafiki enzi za utawala wa Magufuli walikua wanamchukia Magu na wanampenda kikwete, Magu kadanja sahivi wanajidai wamemmiss na kumchukia kikwete ngoja na huyu maza aondoke ushuhudie unafiki wao.

Wa Tz ni wanafiki wakubwa siyo watu wa kuwawekea dhamana watakusaliti kama walivyomsaliti ,Mbowe, Mdude, Soka, Polepole na hata Lissu
 
Ukiwa haumjui Adui yako wa kweli utakuwa unamshambulia kila unayemuona anakukosoa au kukupa changamoto .

Kikwete amekuwa rais 2005-2015 nafikiri hakuna kipindi amabacho upinzani umekua na Kama kipindi chake.

Na alikuwa na uwezo mkubwa wa kuua huo upinzani usikue wala kufika popote Kama alivyofanya JPM .

Adui wa watanzania ni UJINGA wao wenyewe .

Nina uhakika 100% hata SSH akitoka madarakani akaja TAL bado kuna watu watalalamika kuwa bora SSH.

Hawa watanzania hawajui nini wanahitaji kwahiyo ni mtu mjinga pekee atakubali Ku-risk maisha yake kuwapambania .

Namuonea Sana huruma TAL .

Leo tumebaki kusikiliza tabiri za manabii na key body worries .
 
Watanzania wapi hao?
 
Ni kweli kwenye ishu ya demokrasia alijitahidi lakini mwishoni mwa utawala wake alianza kuchukua hatua mbaya sana za kuiminya demokrasia kupitia ile sheria mbovu ya maudhui mitandaoni.
 
Masuala ya nchi sio demokrasia tu, ni pamoja na maendeleo, huduma Bora, kutokuwepo kwa ufisadi, rushwa n.k

Wakati JK rushwa na ufisadi vilitamalaki sana, umeme ulikuwa shida sana, ujenzi wa miundombinu ulikuwa hafifu, ajira nzuri zilikuwa kwa kujuana na vimemo.

Msiwafanye watu hawajui wanachokitaka(gaslighting)
 
Ni kweli kwenye ishu ya demokrasia alijitahidi lakini mwishoni mwa utawala wake alianza kuchukua hatua mbaya sana za kuiminya demokrasia kupitia ile sheria mbovu ya maudhui mitandaoni.
Angle nyingine ya kuangalia hilo ni kwamba enzi sake JK upinzani haukuwa na nguvu sana kiasi cha kutishia kuchukua madaraka kwa hiyo mtawala hakuwa na hofu sana ya kiti chake na chama chake kama ilivyokuwa kuanzia 2015.

Angle nyingine ni kwa sababu nguvu ya social media ilikuwa kidogo 2010 kurudi nyuma kwa hiyo ilikuwa rahisi kuwadanganya watu wengi kwa wakati mmoja au habari kuchelewa kuwafika watu.
 
Back
Top Bottom