JK Kawageuka Museveni,Kagame?

JK Kawageuka Museveni,Kagame?

Wowowo!!
JK alifanya jambo la msingi sana kutowapinga papo hapo!! hata ningekuwa mimi ningefanya vivyo hivo katika misingi ifuatayo:-
1. JK alienda kikaoni alishatoa msimamo wa Tanzania ila wao walikuwa hawajasema msimamo wao hadharani. kwa hiyo chochote kile kitachosemwa kinyume cha ule msimamo wa wazi ulotolewa na Tanzania kingekuwa hakikubaliki straight away. and thats what happened!! Na kwamba wale jamaa wangekuwa na akili wangeahirisha hicho kikao maana jamaa alishasema mambo ambayo yapo nje ya mpango wao!!
2. Haikua jambo la busara kwa Tanzania kutoa hdharani tamko lolote linalopingana na yaliyosemwa na mseveni kwa sababu yangeongeza mpasuko katika ule mgogoro kwani kila mmoja wetu anajua jinsi gani Uganda na Rwanda wanavyokwiba rasilimali za Wakongomani.
3. Aliye na nguvu siku zote hana haja ya kujibizana bali huchukua hatua. Tanzania ilichukua hatua za kiutawala dhidi ya M7 na KG kupitia SADC. Tanzania ina nguvu na uzoefu katika kusimamia amani katika nchi zenye civil wars [refer:- Lebanon; Liberia; Sudan; Zimbabwe; Namibia; e.t.c] kwa hivo wanajua intelijensia ya civil wars.

Mkuu Papa hata mimi kama umesoma bandiko langu naunga mkono azimio hili la SADC kupeleka neutral force Goma, DRC kuzima operesheni za waasi wa M23,tena naona wamechelewa sana.Hoja yangu niliyonayo na JK ni yeye kushindwa kuwaeleza ukweli akina Kagame na Museveni kwenye kikao cha awali cha Kampala na yeye kushiriki kutoa maazimio ambayo kwa kweli yalikuwa kama ya kitoto na yenye kuwabeba waasi hawa.

Nadhani JK was supposed to be firm on the matter na kuonesha kutokukubaliana na maazimio hayo.Kitendo cha yeye kushiriki kikao kile ambacho kilitoa maazimio ya Kampala bila kuonesha kuyapinga na baadaye kushiriki kikao cha SADC ambacho kimekuja na maazimio yanayokanyaga kikao cha Kampala (Hata kama ni mema na tunayaona ya busara) kinampunguzia credit na kama Rais anayeongoza moja ya majeshi imara Afrika alipaswa kuwaonesha akina Museveni kwa nini wanapaswa kuacha undumilakuwili na kusitisha miradi yao huko Goma.
 
y
You are darn rite buddy!!
we must fight for our interest! Wazaire hawana asili ya ugomvi kama tulivyo wa-TZ!! wanaovuruga mambo ni hawa Rwandan and Uganda!! ni wakti sahihi kudhibiti hii hali!!


WanaJF,
Tukumbuke, Kabila mkubwa (Baba yake na Joseph) aliingia madarakani kwa msaada wa vikosi vya Rwanda na Uganda. Rwanda na Uganda sio kuwa walikuwa wanampenda sana Mzee kabila bali walikuwa na maslahi wanayonyemelea. Masharika mwa DRC, kuna ou kabila la wanyamulenge, hawa ni watutsi wenye asili ya Rwanda. Wanyankole wa Uganda (kabila la mseven) ni watutsi bila hata kuacha shaka lolote. Pamoja na kwamba Rwanda na Uganda walikuwa wanafukuzia mali asili za DRC pia nia yao kama walivyokuwa wamekubaliana na Kabila mkubwa ni kuanzisha kile kinachoitwa 'HIMA (TUTSI) EMPIRE, ambayo itamega sehemu ya mashariki mwa DRC na kuunganishwa na nchi za Rwanda na Uganda, pia tukumbuke Kagame alikuwa Mkuu wa Intelijensia wa Mseven kabla Kagame hajapata madaraka ya urais nchini Rwanda na Kagame aliingia madarakani kwa msaada wa vikosi vya Uganda.

Baada ya Kabila mkubwa kuingia madarakani, wananchi wa DRC walianza kupiga kelele kuhusu uwepo wa watutsi wengi kwenye serikali na hasa Jeshi la DRC. Generali Kabarebe ambaye kwa sasa ni Waziri kama sio Mkuu wa Majeshi ya Rwanda alikuwa Mkuu wa majeshi ya DRC wakati wa kabila mkubwa. Bizima Karaha (Jina halisi ni Bizimana) alikuwa member wa cabinet kwenye serikali ya DRC naye alikuwa mnyarwanda achilia mbali nafasi nyingine nyeti ambazo hadi leo wanyarwanda wamejichomeka. Sasa Kabila mkubwa baada ya kelele nyingi za wananchi wa DRC aliamua kuvunja makubaliano na kuamuru majeshi ya Rwanda kuondoka nchini DRC, kutokana na tamko hilo wote tunajua yaliyompata Mzee kabila.

Sasa hujuma za M23 mashariki mwa DRC, ni kagame na Mseven wanaotaka kujaribu kutimiza ndoto zao za kuanzisha na kjenga HIMA EMPIRE AU TUTSI EMPIRE. Bahati mbaya jumuia ya kimataifa imeshawashtukia kuhusu kusudio lao hilo. Lakini tutazame madhara ya kukosekana utulivu mashariki mwa DRC kwa Tanzania. Asilimia kubwa ya biashara zinazoendeshwa nchini DRC zinatokea Tanzania au zinafka DRC baada ya kuingilia Tanzania, kwa maana nyingine Tanzania kiuchumi inaitegemea sana DRC. Kuiacha DRC iendelee kuandamwa na hao watutsi ni sawa na kuacha uchumi wa Tanzania uzidi kudidimia kisa kagame na mseven wanataka kuanzisha hima empire na kuiba raslimali za DRC.

My take,
Acha tupeleke majeshi DRC ili tulinde miraji yetu, tufahamu pia kwamba sio rahisi kupigana na waasi waliozoea mazingira na jiografia ya mashariki mwa DRC lakini ni bora kufanya hivyo kuliko kusubiri na kushuhudia maslahi yetu ya kiuchumi yakianguka. Mugambe aliwahi kutoa pendekezo wakati ule Rwanda inaivamia DRC, yeye alisema, wakti Rwanda inapigana mashariki mwa DRC, Tanzania kama mwananchama wa SADC itoa ardhi yake ili vikosi vya SADC vianzishe mashambulizi vikitokea Tanzania kwenda Rwanda, Hapo Mhe. Mkapa aliona noma na kukataa pendekezo sahihi la Mugambe kwani lingmfanya kagame ku-withdraw majeshi yake ili aje atetee nchi yake kwa uvamizi huo. Tumuunge mkono mhe. Rais kwa hatua ya kuungana na wananchama wa SADEC kupelekea askari mashariki mwa DRC. lAKINI MWISHO, mashariki mwa DRC kuna waswahili wengi sana wenye mafungamano na watu wa kigoma, kwa hiyo kwa interest ile ile ya akina kagame na mseven na sisi ni hivyo. Haya wenye kujua zaidi tuchangia.
 
katika SADC hakuna wa rais wa kuaminika wote wapiga deal, wameona uganda na rwanda wanafaidi nao wanataka wapige za kwao, DRC like JAY Z it is a real deal,
 
Watz tuwe waelewa..hv tunawajua kagame na mseveni..leo wako kivu..kesho utawsikia wako rusumo na misenyi...hogera JK tuanze kujenga heshima ya tz ...ni kwa kuwafuata huko walipo..kumbukeni jeshi la rwanda kwa sasa lina idadi kubwa ya askari..watawamudu vp ndani ya nchi yao...ni kwa kuwatafutia UN mission na chokochoko ndani ya nchi jirani..ili wao wabaki salama...tuamke watz ..tuko tayari kusaidia congo..ili kuleta heshima kwa tz
 
katika SADC hakuna wa rais wa kuaminika wote wapiga deal, wameona uganda na rwanda wanafaidi nao wanataka wapige za kwao, DRC like JAY Z it is a real deal,

We unaonekana ni walewale,subiri unaogopa nini?. Kabila kesha wakamata askari 10 wa Rwanda pale Goma jana!. Kama alivyowahi sema Nyerere wakati wa vita na Idd Amin wa Uganda wakati huo'za masika zinawanyeshea kwa sasa,subirini za vuli'!
 
Huwa sielewi hii kitu,tuna ndoto ya kuunganisha bara la Afrika huku tukiendelea kuligawa vipande! Kesho mtaigawa Kivu alafu baadae Kivu na Congo zitaomba kujiunga EAC ambayo tunaota ije kuwa nchi moja what a dream!!!

Ni tamaa za viongozi tu,Kwa mfano Tanzania ni nchi kubwa sana pia kuliko zote EA,unadhani mkuu DSN tukitofautiana solution itakuwa kuigawa pia?

Kongo ni ya Wakongo tuwaache waamue wenyewe bila kuwaingilia na cha kuwasaidia ni kuimarisha usalama na kulijenga upya jeshi lao ili lisimamie usalama bila kuingiliwa na watawala wenye uchu.

Nakuhunga mkono mkuu, mwezi mmoja na nusu hivi uliopita nilimuona jamaa mmoja kutoka Africa kusini akihojiwa na BBC (sikumbuki vizuri kama ni mwenyeji wa Africa kusini au ni mkimbizi wa Kinyarwanda anayeishi Africa Kusini) Nilimsikia akisema DRC ni nchi kubwa mno kwa nini Kivu ya kasikazini na kusini zisijitenge na ku-form an independent Nation! Eti kama Sudan imefanikisha hilo why not DRC, kauli ya jamaa huyo ilinisikitisha sana.

Lengo la Kagame, M23 na M7 ni hilo hilo - kuimega DRC, wengi wa wanajeshi wa M23 ni Wanyarwanda wanajifanya ni Wakongomani wakiwa na lengo maalumu la kutaka kuingizwa kwenye jeshi la DRC alafu baadae walalamike kwamba wanabaguliwa na Serikali ya Kabila - fujo zianze tena na wenye hidden agenda waendelee kubeba mali za DRC; kusema kweli Mh.Kagame hasipo jirudi hatakuja kutuletea mahafa makubwa ndani ya nchi za maziwa makuu, sina shaka Viongozi wa nchi za SADC hilo wamekwisha linshitukia na watalifanyia KAZI.

Wasikubali nchi ndogo inayo ongozwa na binadamu ambaye ahambiliki avuruge watu kwa visigizio vya kutunga TU, akiendelea na ubishi wake basi majeshi ya SADC yasihishe mipakani mwa Rwanda na DRC wamfuate huko huko aliko akajibu sababu zilizo ifanya DRC ipoteze raia wake zaidi ya millioni tano kwenye vita vya kipuuzi.

Cha kufanyika sasa hivi ni kuimarisha jeshi la DRC - hilo la kwanza, la pili - watawala wenye an hidden agenda kuhusu Taifa hilo waache/wakome kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo, Wakongomani wana uwezo mkubwa wa kuongoza nchi yao bila ya kuingiliwa na mtu.
 
Wowowo!!
JK alifanya jambo la msingi sana kutowapinga papo hapo!! hata ningekuwa mimi ningefanya vivyo hivo katika misingi ifuatayo:-
1. JK alienda kikaoni alishatoa msimamo wa Tanzania ila wao walikuwa hawajasema msimamo wao hadharani. kwa hiyo chochote kile kitachosemwa kinyume cha ule msimamo wa wazi ulotolewa na Tanzania kingekuwa hakikubaliki straight away. and thats what happened!! Na kwamba wale jamaa wangekuwa na akili wangeahirisha hicho kikao maana jamaa alishasema mambo ambayo yapo nje ya mpango wao!!
2. Haikua jambo la busara kwa Tanzania kutoa hdharani tamko lolote linalopingana na yaliyosemwa na mseveni kwa sababu yangeongeza mpasuko katika ule mgogoro kwani kila mmoja wetu anajua jinsi gani Uganda na Rwanda wanavyokwiba rasilimali za Wakongomani.
3. Aliye na nguvu siku zote hana haja ya kujibizana bali huchukua hatua. Tanzania ilichukua hatua za kiutawala dhidi ya M7 na KG kupitia SADC. Tanzania ina nguvu na uzoefu katika kusimamia amani katika nchi zenye civil wars [refer:- Lebanon; Liberia; Sudan; Zimbabwe; Namibia; e.t.c] kwa hivo wanajua intelijensia ya civil wars.

Mkuu Papa D again naomba nikuulize swali dogo tu.Kulikuwa na tatizo gani JK kuurudia msimamo wake kwenye kikao hicho cha Kampala? Njia nzuri ni yeye kukubali kushiriki na kuwa sehemu ya maazimio yake au alipaswa kutokukubaliana mapema? Huoni kwa sasa Kampala na Kigali wanaendelea na utekelezaji wa maazimio hayo (ambayo JK alikuwa sehemu yake)? Sasa huu mkanganyiko wa maazimio ya SADC na Kampala si ndiyo mpasuko zaidi?
 
Mkuu Wowowo!!
Binafsi sikuwa ndani ya hicho kikao kwa hiyo sijui kama alisisitiza msimamo wa Tanzania au aliubadili Isipokuwa kwa kuwa alishasema msimamo wake kabla ya kikao husika na kwamba hajaukanusha huo msimamo hadi sasa! then ninachukulia kuwa hakubaliani na hoja za Kagame na Mseveni katika taarifa kwa waandishi wa habari. nikupe mfano rahisi tunaouona kila siku kwamba:- Wabunge wa CHADEMA waliikataa budget ya Wizara ya Fedha lakini Bunge liliipitisha. Unafikiri kelele za wabunge wa chadema nje ya bunge baada ya kupitishwa hiyo budget ziliibatilisha? mfano mwingine ni sheria ya mabadiliko ya katiba ambayo ilipitishwa na bunge lakini CHADEMA wakaongea na rais aliyekuwa tayari kaisaini within few days before. matokeo yake ikarudi bungeni kurekebishwa unalinganishaje kelele za wabunge wa chadema baada ya budget ya wizara ya fedha na ile mbinu ya kuonana na rais baada ya sheria ya katiba?. Mfano wa pili ndiyo approach alotumia JK kuzima hujuma za Kagame na Mseveni. Ulle mfano wa Kwanza [Wizara ya Fedha] ndo unachopendekeza wewe kwamba kingefanywa na JK na hapo ndipo tunapotofautiana!!
Si kila jambo lazima ulitatue kwa kupigishana kelele na mtofauti wako!

Mkuu Papa D again naomba nikuulize swali dogo tu.Kulikuwa na tatizo gani JK kuurudia msimamo wake kwenye kikao hicho cha Kampala? Njia nzuri ni yeye kukubali kushiriki na kuwa sehemu ya maazimio yake au alipaswa kutokukubaliana mapema? Huoni kwa sasa Kampala na Kigali wanaendelea na utekelezaji wa maazimio hayo (ambayo JK alikuwa sehemu yake)? Sasa huu mkanganyiko wa maazimio ya SADC na Kampala si ndiyo mpasuko zaidi?
 
Museveni meets Russian President Vladimir Putin

By In2EastAfrica Reporter


President Yoweri Museveni has held talks with the Russian president Vladimir Putin at the Novo-Ogaryovo state residence outside Moscow.

Putin-R-meets-with-his-counterpart-Museveni.jpg

Russias President Vladimir Putin (R) meets with his counterpart Yoweri Museveni at the Novo-Ogaryovo state residence outside Moscow December 11



The two leaders discussed the prospects of strengthening bilateral cooperation in oil and gas and electric power
Russia has several interests with Uganda which range from supplying combat aircraft to oil and gas projects.
Uganda signed its first contract to buy six Sukhoi Su-30MK2 fighters from Russia early this year for an undisclosed sum.
On the other hand, Russia's largest independent crude producer LUK oil has expressed interest in oil and gas exploration, production and refining in Uganda.
Foreign interest in Uganda's oil sector continues to grow ever since crude oil deposits were discovered in 2006 in the Albertine Graben area along the country's western border with the Democratic Republic of Congo. Current reserves are estimated at about 3.5b barrels.
 
waswahili wanasema mchawi mpe mwana amlelee .suala la kongo na museveni na kagame na mikataba ya msituni vinajulikana ,kuwapa hii kazi ya kuleta amani congo ni kuona hawa jamaa wana muelekeo gani na congo naona ni mapema kusema zaidi kwa kuwa hapa tunaona wamekuja kukutana tena kwenye jumuia ya sadc na kuunda jeshi moja ,kuilinda congo itakuwa ni miujiza viongozi hawa kukiuka makubaliano hayo. kimsingi congo inatakiwa iwe ni tulivu uchumi ukue .
 
waswahili wanasema mchawi mpe mwana amlelee .suala la kongo na museveni na kagame na mikataba ya msituni vinajulikana ,kuwapa hii kazi ya kuleta amani congo ni kuona hawa jamaa wana muelekeo gani na congo naona ni mapema kusema zaidi kwa kuwa hapa tunaona wamekuja kukutana tena kwenye jumuia ya sadc na kuunda jeshi moja ,kuilinda congo itakuwa ni miujiza viongozi hawa kukiuka makubaliano hayo. kimsingi congo inatakiwa iwe ni tulivu uchumi ukue .

if you cannot fight them join them.

Sijui Tanzania kwanini tunalaza damu wakati wenzetu Uganda, Rwanda na Kenya wanafaidi kutoka DRC. Sijui sisi wabongo kwanini tunakua bongolala namna hiyo. Hayo madini na resources za Kongo hayana Mwenyewe, kwanini serikali yetu isiwe na mikakati ya makusudi ya kufyonza hizo Resources na kunufaika kama wafanyavyo wengine?. Kama tungekua na mikakati bora Jeshi letu lingeweza kutumwa kwenda Kongo 'kulinda amani' au 'Kuleta Mshikamano' au 'Kudumisha Udugu' au kwa kutumia kisingizio kingie chochote kwa lengo moja tu la kuchukua chetu mapema kwa manufaa ya Taifa la Tanzania kwa ujumla.

Tukijifanya waungwana eti hatuendi wengine wataenda na hakuna tutakachoambulia zaidi ya kulundikiwa wakimbizi tutunze.

181881_474270055949229_1108364857_n.jpg

I like this picture. i wonder why Tanzania is not in this meeting to discuss about its turn in this game.
 
We unaonekana ni walewale,subiri unaogopa nini?. Kabila kesha wakamata askari 10 wa Rwanda pale Goma jana!. Kama alivyowahi sema Nyerere wakati wa vita na Idd Amin wa Uganda wakati huo'za masika zinawanyeshea kwa sasa,subirini za vuli'!

illusion
 
Mikakati ya M7 na Kagame inatofautiana kidogo. M7 anataka kuwa mtawala mkuu wa kanda ya ziwa. Simply he is a power hungry politician. Kagame alipojaribu kuhoji jambo hili ndipo majeshi yake yakaanzisha vita vya Kisangani dhidi ya Rwanda ndani ya Kongo. Lakini Kagame ana Mkakati wa masafa marefu wa kutengeneza utawala pandikizi katika Kongo mashariki. Angependa utawala huo uipatie Rwanda eneo salama kwa ajili ya ulinzi na pia unyonyaji wa maliasili za Kongo. Utawala huo pandikizi wenye jeshi la Wanyarwanda na Wanyamlenge hatimaye ungeshurutisha serikali ya Kongo kuitisha kura ya maoni juu ya utawala wa majimbo na hata eneo hilo kujitenga kabisa kama ilivyofanya Sudan Kusini. Mbinu hatari ya Kagame ni kuiga mbinu za Israel za kujihami na kueneza utawala wa kitusti kupitia mamlaka na watu pandikizi. Tayari ana vipandikizi vingi ndani ya jeshi na mamlaka mbalimbali za serikali ya Kongo. Yawezekana ana Vipandikizi ndani ya serikali na mamlaka yetu-Tanzania. Tunapashwa kuwa waangalifu sana. Hivyo,msimamo wa serikali yetu ni sahihi kabisa. Tanzania haiwezi kufanikisha lolote kwa kupeleka majeshi Kongo chini ya framework ya nchi za maziwa makuu ambapo vinara wakuu ni M7 na KGM, ambao ingawa ni fisi hupenda kuvaa ngozi ya kondoo. Njia sahihi ni nchi za SADCC kupeleka majeshi chini ya mfumo huru wa Jumuiya hiyo. Lakini SADCC imbane Kabila kulipia robo au nusu ya gharama zote. Ameonekana kuwa dhaifu sana kisiasa, kiutawala na kijeshi. Ameshindwa kuimarisha jeshi lake na kuanzisha juhudi za kisiasa za kuamsha moyo wa uzalendo miongoni mwa Wakongo. Wakati Goma ilikuwa imekaliwa Mpiana alikuwa akitumbuiza DAR na baadaye Mwanza. Wakongo wawe serious na kuanza kufikiria nchi yao. Kuna taarifa kwamba wafanyakazi wa serikali Kongo wakiwemo wanajeshi hulipwa mshahara wa mwezi mmoja baada ya miezi 4 au 5 ! Hivyo sehemu kubwa ya jeshi la Kabila halina nidhamu na hujilipa kwa kuwapora wananchi wa kawaida, kutoza ushuru au kuchimba madini!. Nikijaaliwa tena nitazungumzia jinsi Tanzania inavyoweza kujipanga kimkakati kulinda na kumarisha maslahi yake nchini Kongo.
 
Wapeni Congo nafasi waje waletee vijana Wao waje kufundishwa kuwa wanajeshi thabiti mbona wakati wa nyerere swapo na ANC walileta Askari hapa . Let us consolidate our position, we can make a difference
 
Kesho mazungumzo yanaendelea mjini Kampala. Tusubiri tuone.
 
Ni ajabu sana Kagame na Museven wanatuhumiwa kusaidia waasi wa M23 na haohao (watuhumiwa) ndiyo wako moto kweli kutafuta suluhu DRC.Ati wanajifanya kuratibu mazungumzo kati ya Waasi na Serikali ya Kinshasa. Kweli kuna suluhu hapo? Si kutaka kumtesa na kumbana Joseph Kabila kuishia kuruhusu nchi kukaliwa na waasi hawa?

Ninachoshindwa kuelewa ni kitendo cha JK kuafikiana na akina Museveni na leo ghafla anaingia makubaliano mengine na SADC tena yenye kutengua makubailiano ya Kampala. Je JK hakuona tatizo katika maazimio ya Kampala? Alizidiwa nguvu na akina Kagame? Maswali ni mengi hapa.

Mkuu tatizo ninalo liona nchini mwetu ni kutothamini uwezo wa JK katika masuala ya upatanishi nk. Jamaa huyu ana akili sana! Atumii mabavu au majigambo katika strategies zake za ku-resolve conflicts za within na without, what he does ni kuwapa fools enough rope alafu wajimalize wenyewe! Mbinu hii imemsaidia sana - at the end of the day mtu anajikuta amekuwa exposed ujinga wake mpaka anakosa nguvu za kumkimbilia tena JK amuokoe/kuomba msaada. JK yuko smart sana UPSTAIRS watu hawajuhi tu.

Hata hili la Kampala usifikili alikuwa hajuhi kinacho endelea behind the scene na alikuwa anajuwa culprit wa janga lote la DRC ni akina nani - alicho fanya pale ni kuwasikiliza kwa umakini waki-shade crocodiletears na ku-blame vivuli vyao - kawasikiliza weee!!! Mwishowe alijuwa jinsi ya ku-contain tatizo hilo sugu kwa ku-spring up a surprise of a centuary kwa kikundi cha utawala wa Uganda na Rwanda, kumbuka JK ni Mwana jeshi.

Sikumbuki ilichukua muda gani tangu atoke Kampala kabla ajahitisha kikao cha dhalula cha nchi za SADC - na wote walihitikia mwaliko wake - kwa nini? Bila shaka aliwambia in advance kwamba hali ya DRC ni tete sana wanapaswa kutafuta ufumbuzi wa kudumu haraka sana, M7 na Kagame walijua fika hawawezi kuhudhulia kikao hicho moto - wakahamua ku sepa, kwa katoa visingizio vya kutohudhulia mwaliko.

Taarifa zinasema Africa Kusini itatoa logistic support, wakina Kagame na M7 wanajuwa fika kwamba hiyo haina maana ya kutoa magari/malori ya kusafirisha wanajeshi tu, Angola hatujuhi itatoa nini, Zimbabwe nayo je? Kwa kifupi utawala wa Rwanda na Uganda Unajuwa ukiendeleza vurugu zao ndani ya DRC na kushindwa kujirekebisha nyenendo zao basi hilo litawa cost dearly pamoja na utawala WAO, wasifikili dunia itavumulia milele au wanajeshi wa SADC na silaha zao watakuwa passive kama majeshi ya UN.

Labda nimalizie kwa kusema nabii hathaminiwi nchini mwake na hilo ndilo tatizo letu kuu hapa, sisemi yeye ni malahika au nini lakini ni mtu makini sana, kuchaguliwa kwake kuwa kiongozi tangu shule ya msingi mpaka chuo kikuu si bure, kuna kitu pale si bure, wakina M7 na Kagame kama walikuwa wanafikili JK ni legelege naona wameonja shubiri YAKE, kawageuzia kibao kidiplomasia mpaka wamejikuta wamebanwa between the rock and hardplace, majivuno yao ya pale kampala yame-sublime into a thin AIR.
 
Museveni meets Russian President Vladimir Putin

By In2EastAfrica Reporter


President Yoweri Museveni has held talks with the Russian president Vladimir Putin at the Novo-Ogaryovo state residence outside Moscow.

Russias President Vladimir Putin (R) meets with his counterpart Yoweri Museveni at the Novo-Ogaryovo state residence outside Moscow December 11


Heshima yako mkuu GEZA naona umerudi jamvini, karibu sana.
 
Wapeni Congo nafasi waje waletee vijana Wao waje kufundishwa kuwa wanajeshi thabiti mbona wakati wa nyerere swapo na ANC walileta Askari hapa . Let us consolidate our position, we can make a difference

Huko sahii mkuu, lakini na wenzetu hawa wamezidisha mambo ya kupenda starehe - wapo wengi hapa nchini sijawahi kuwasikia wana hadamana wakipinga uvamizi nchini mwao zaidi ya kuwasikia ma presidaa wa mabendi na mambo ya ndomboro ya solo hawatoi hata mchango wa kuwasaidia ndugu zao wakimbizi, wanasubiri nchi nyingine ziwafanyia kazi ya ulinzi nchini mwao - yakija masuala ya ukombozi wa nchi yao wako kimya kabisa.

Wame sambaa dunia nzima especially Ufaransa na Ubelgigi hawachangii chochote katika ustawi wa nchi YAO. Juzi juzi ndio nilisikia walifanya mahandamano mjini London walikwenda Ubarozi wa Rwanda kupinga nchi hiyo kuvamia nchi yao.
 
Back
Top Bottom