JK Kawageuka Museveni,Kagame?

JK Kawageuka Museveni,Kagame?

Malawi nao watatoa wanajeshi kwenda Congo.Lazima tukubali ustawi wa Congo una faida kubwa sana kwetu kiuchumi kuliko hata Kenya.
Tumejiandaaje kufaidika kiuchumi ktk Congo itayostawi.

Bila kusita namuunga mkono Rais Kikwete kwa maamuzi haya!

Mpaka lini Museveni na Kagame wataendelea kuogopwa kama ni mabwana wakubwa?
 
Tatizo la DRC na maamuzi ya SADC ni zaidi ya Rwanda na Uganda. UN wana kikosi cha kulinda usalama pale nafikiri kikubwa Africa kama sio duniani. UN wanatumia fedha nyingi kwa shughuli hii! Ajabu ni kuwa mambo haya yanatokea mbele ya kikosi hiki! Maamuzi ya SADC ni kuwaambia UN you have failed us...lakini wakati huo huo wanataka wapate support ya UN. Je hii itawezekana tuwe na vikosi viwili vyenye mandate ya UN - na sijui Kama mandate ya hivi vikosi zitatofautiana. Kuna suala la funding, bila support ya UN je SADC wataweza kumudu kwa muda mrefu? Tujue hii si kazi ya mwezi mmoja inaweza kuchukua miaka na ni aghali siyo kwa fedha tu Bali hata maisha ya vijana wetu.

Askari wetu hawaihitaji maziwa na siagi; mihogo kwa chai wao ni poa kabisa; askari wa UN ni watalii acha vijana wakalizime kidogo
 
Mkuu Ritz sisemi JK alikuwa pamoja na Museveni au Kagame.Read between the lines maelezo yangu. JK alishiriki kikao cha Kampala na kufikia maazimio kadhaa dhidi ya Kinshasa na waasi wa M23 lakini leo kayaweka pembeni maazimio hayo na kuja na azimio la kuunda Jeshi la kudhiti rebel militias Kivu chini ya SADC.

Nimeeleza kuunga mkono wazo hili lakini nikahoji sababu ya JK kuunga mkono maazimio ya Kampala wakati hakuyaafiki, je ilitokana na yeye kuzidiwa nguvu na akina Kagame na Museveni? Mbona chini ya SADC amekuja na mpango tofauti na ule wa Kampala?

WOWOWO, naomba nikukumbushe kwamba hivi ni vikao viwili tofauti na JK siyo muwakirishi wa SADC kwenye EAC na vivyo hivyo kinyume chake. Kwa hiyo JK anakwenda kama fresh member kwenye EAC na SADC. Kama EAC inahitaji muwakirishi kwenye SADC itapeleka itatuma mjumbe wake na vivyo hivyo kwa SADC kwenye EAC. Kama EAC members wake ni Museven na Kagame ambao wanakuwa karibia theluthi ya wanachama wote, huoni wanaweza kuinfluence matokeo ya mkutano wote. JK hahitaji kubishana na watu ambao anajua kabisha upande wao katika mgogoro. Alichokifanya JK ni sahihi kabisa kuonyesha kwamba anakerwa na tabia zao za udumila kuwili. Nani kigeu geu hapa, JK anayefanya maamuzi yanayooneka kwa uwazi kabisa kwa kutangazwa na vyombo vya habari au Kagame na Museveni wanaowaunga mkono waasi, M23, halafu kwenye vyombo vya habari wanakataa. Dawa ya jeuri ni kuwa jeuri zaidi yake. Big up JK. Kwanza muonyeshe Kagame kwamba anaongoza mkoa mmoja tu kwa Tanzania wakati wewe unaongoza nchi kubwa mara hamsi ya kwake kwa dharau zake alizowahi kuwa nazo. Kwa kifupi, Kagame na Museveni kwa support ya USA na Ulaya wamekuwa na kiburi sana kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati. Sasa wataona moto wake, na hao washirika wao [USA na Ulaya] kwa kuwa wanatabia ya ku-use na ku-abuse, very soon watawatupa kama kondom iliyotumika. Ndipo Rwanda itarudi tena kwenye dimbwi la ukabila tena.
 
Mnyonge mnyongeni ila mpeni haki yake!!!!!!!1
JK hakukubaliana na hao jamaa [M7 na Kg]. Kumbukeni jambo moja kwamba kabla hajaenda uganda alishasema tanzania itasaidia kutoa walinzi wa amani. lakini baada ya kile kikao cha uganda M7 kama mwenyekiti wa kile kikao alitoa maazimio ambayo hayakuwa na kipengele hata kimoja kilichotoka Tanzania. Tafsiri yake ni rahisi sana kwamba KAgame na M7 walimgeuka JK wakijua yeye ni kilaza watampelekapeleka tu bila kujua kwamba Tanzania bado ina marafiki wengi na wanaoiheshimu. Kawasiliana na Angola, Msumbiji, Sauth Africa, Zimbabwe na Namibia wakakubaliana kuwadhibiti hawa majambazi wawili. Kilichofuatia JK katumia mlango wa nyuma kuwadhibiti M7 na Kagame [jikumbushe udharura wa hicho kikao cha SADC kilichotanguliwa na kamati ya SADC ya ulinzi na usalama]. JK played a very smart game on this! we must aknowledge and praise his move!!

Ni ajabu sana Kagame na Museven wanatuhumiwa kusaidia waasi wa M23 na haohao (watuhumiwa) ndiyo wako moto kweli kutafuta suluhu DRC.Ati wanajifanya kuratibu mazungumzo kati ya Waasi na Serikali ya Kinshasa. Kweli kuna suluhu hapo? Si kutaka kumtesa na kumbana Joseph Kabila kuishia kuruhusu nchi kukaliwa na waasi hawa?

Ninachoshindwa kuelewa ni kitendo cha JK kuafikiana na akina Museveni na leo ghafla anaingia makubaliano mengine na SADC tena yenye kutengua makubailiano ya Kampala. Je JK hakuona tatizo katika maazimio ya Kampala? Alizidiwa nguvu na akina Kagame? Maswali ni mengi hapa.

Mimi sishangai, kwani mmseashau JK ni kigeugeu. Wakati wowote yeye anaweza kukubadilikia. Mnasahau hata humu nchin huwa anawageuka mawaziri wake? Huyo ndiyo JK bwana, mwingine photocopy. By the way huu msimamo wake wa sasa nauunga mkono.
 
Mnyonge mnyongeni ila mpeni haki yake!!!!!!!1
JK hakukubaliana na hao jamaa [M7 na Kg]. Kumbukeni jambo moja kwamba kabla hajaenda uganda alishasema tanzania itasaidia kutoa walinzi wa amani. lakini baada ya kile kikao cha uganda M7 kama mwenyekiti wa kile kikao alitoa maazimio ambayo hayakuwa na kipengele hata kimoja kilichotoka Tanzania. Tafsiri yake ni rahisi sana kwamba KAgame na M7 walimgeuka JK wakijua yeye ni kilaza watampelekapeleka tu bila kujua kwamba Tanzania bado ina marafiki wengi na wanaoiheshimu. Kawasiliana na Angola, Msumbiji, Sauth Africa, Zimbabwe na Namibia wakakubaliana kuwadhibiti hawa majambazi wawili. Kilichofuatia JK katumia mlango wa nyuma kuwadhibiti M7 na Kagame [jikumbushe udharura wa hicho kikao cha SADC kilichotanguliwa na kamati ya SADC ya ulinzi na usalama]. JK played a very smart game on this! we must aknowledge and praise his move!!.....

Unajua hizi nchi zimekuwa zikitufikiria sana kuwa sisi ni bogus na siyo smart sana. Kagame na Museveni wanafikiria wanajua sana kuliko Tanzania wakati Tanzania ndo imewalea na kutoa ulinzi na usalama wa ukanda huo mzima.

Naona heshima ya Tanzania ilianza kushuka mpaka Kagame kusema kwamba angekuwa raisi wa Tanzania angeifanya kama Ulaya. Ujumbe gani huu kwa raisi wa Tanzania.

Na yeye anafikiria watanzania tunasahau kwa haraka sana. Mimi binafisi tangia nisikie hiyo kauli amabayo naiona ni tusi kwangu, kwa raisi wangu na kwa watanzania wote, nimekuwa nikijaribu kumjua sana huyu Kagame na chanzo cha Kiburi cahake.

Nimegundua kuwa ni puppet mzuri sana wa matajiri wa Marekani na Ulaya ambao wanamtumai kuharibu utawala wa Ukanda wa Afrika, has DRC ili waendelea kuiba mali zetu.

Mtu kama huyo aliyenunuliwa always hajitambui kabisa zaidi ya kuwa Power Monger. Anaweza kufanya lolote kwa ajiri yake binafsi na ndo maana amekuwa akikandamiza wanasiasa nchi kwake.

Kwa hatua hii, hata hiyo EAC ife tena na tuizike, hakuna shida kabisa, ila SADC ibakie na idumu milele. Ideolojia za viongozi wa Afrika ya kusini, Zimbambwe, Namibia, Angola, Zambia na Musumbiji, achana na homosexual Malawians ambao nao raisi wao wa kwanza alikuwa pupet wa UK, zinafanana kabisa kwamba tunajiamini na tuna uzalendo wa nchi zetu. Ni bora tushirikiane na hawa watu kuliko hiyo EAC yenye kelele nyingi za kiwizi tu.
 
chezea JK weye, huyu Raia ni wakipekee nasema huwa agombani namtu yeye anaitikia kisha anafanya analoona yeye lina fahaa kabila lazima arudi nyumbani TZ kusema kwa baba maana ndiye wa kumsaidia ni kweli hatuwez kumtupa ndugu yetu kabila huyu ni ndugu yetu anajua wema wa Tz na hawezi kusahau
 
Mpaka lini Museveni na Kagame wataendelea kuogopwa kama ni mabwana wakubwa?

Mkuu hawa hawaogopwi,nadhani kila nchi inaangalia maslahi yake ikijiingiza kwenye huo mgogoro.Lakini huwa nahisi ipo siku hawa wataitenga Tanzania kwenye hiyo EAC maana huko tuendako tutatofautiana kwenye mengi.
 
Mkuu MTAZAMO, uhuru wa nchi za kiafrika nyingi umekuwa dhaifu kwa kufikiria kwamba baada ya kutangazwa tu, wakoloni walikoma kufikiria jinsi ya kuzinyonya nchi hizi. Hili ndo limepelekea kujikuta kwenye ukoloni mambo leo bila kijijua. Kikubwa hapa ni kuulinda uhuru daima na milele. How?
Kuwa na uchumi imara.
Kuwa na elimu bora.
Kuwa na afaya bora.
Kuwa na umoja katika nchi ili kunapotokea adui, anakuwa adui wetu wote kama nchi.
Kuwa na jeshi la kutosha.
Na mambo mengine kibao.
Kwa hiyo, lazima tujiwekeze kwenye hivyo vitu kwani huji M25 inaweza kutengezwa na hao watu ikaelekezwa Tanzania kama wanaona ndo kikwazo kwa kile wanachotaka. Lazima tuwe tayari kujilinda kwa kila kitu.
 
REPUBLIC OF KIVU
Why not?Leo kuna Sudan Kaskazini na Sudani Kusini,Binafsi naiona Congo ni kubwa mara mbili na robo ya Ethiopia kiasi kuwa Utajili mali ya asili yake auwafaidishi wakongomani kwa kuwa augawiki ipasavyo.Nimepata kusikia ujio wa NCHI INAITWA KIVU kwa mwenendo huu naona kuna haki pia ya kuhoji umma wa kama Nchi iyo iwepo au la!!!Watanzania kwenda huko ni kwenda kutuliza kwa muda kisha baada ya miaka kadha wa kadha kinanuka upya!!!

Huwa sielewi hii kitu,tuna ndoto ya kuunganisha bara la Afrika huku tukiendelea kuligawa vipande! Kesho mtaigawa Kivu alafu baadae Kivu na Congo zitaomba kujiunga EAC ambayo tunaota ije kuwa nchi moja what a dream!!!

Ni tamaa za viongozi tu,Kwa mfano Tanzania ni nchi kubwa sana pia kuliko zote EA,unadhani mkuu DSN tukitofautiana solution itakuwa kuigawa pia?

Kongo ni ya Wakongo tuwaache waamue wenyewe bila kuwaingilia na cha kuwasaidia ni kuimarisha usalama na kulijenga upya jeshi lao ili lisimamie usalama bila kuingiliwa na watawala wenye uchu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu MTAZAMO, uhuru wa nchi za kiafrika nyingi umekuwa dhaifu kwa kufikiria kwamba baada ya kutangazwa tu, wakoloni walikoma kufikiria jinsi ya kuzinyonya nchi hizi. Hili ndo limepelekea kujikuta kwenye ukoloni mambo leo bila kijijua. Kikubwa hapa ni kuulinda uhuru daima na milele. How?
Kuwa na uchumi imara.
Kuwa na elimu bora.
Kuwa na afaya bora.
Kuwa na umoja katika nchi ili kunapotokea adui, anakuwa adui wetu wote kama nchi.
Kuwa na jeshi la kutosha.
Na mambo mengine kibao.
Kwa hiyo, lazima tujiwekeze kwenye hivyo vitu kwani huji M25 inaweza kutengezwa na hao watu ikaelekezwa Tanzania kama wanaona ndo kikwazo kwa kile wanachotaka. Lazima tuwe tayari kujilinda kwa kila kitu.

Tungekuwa na AU imara Afrika ingetulia.Utulivu ndio msingi wa maendeleo na kama mnao utulivu na hamjaendelea ni debate nyingine!

Tuna AU dhaifu kuliko hata OAU ilivyokuwa pamoja na mapungufu yake.
 
Tungekuwa na AU imara Afrika ingetulia.Utulivu ndio msingi wa maendeleo na kama mnao utulivu na hamjaendelea ni debate nyingine!

Tuna AU dhaifu kuliko hata OAU ilivyokuwa pamoja na mapungufu yake.

Udhaifu wa AU ni kutokana na kuwa na viongozi wasiokuwa wazalendo kwa Afrika, puppets. Mpaka pale tutakapoweza kuelimishana sisi kwa sisi kwanza, ndio tunaweza kuondoa huu udhaifu. Nchi tajiri dunia zinatumia umasikini wa baadhi ya waafrika kuwanyonya waafrika wengine. Hilo ndo tatizo. Binafsi naamini kwamba, pale kila muafrika ataelewa umuhimu wake kwa Afrika na waafrika wenzake, ataweza kulinda amani ya Afriaka, atazuia uibwaji wa rasimali za Afrika na mambo mengine mengi kibao. Afrika ni tajiri mkubwa. Jiulize haya madini yanayotengeza denge, komputa, magari na vitu vingi vya thamani yanatoka Afrika. Tukiweza kufanya biashara ya haki kama Libya walivyokuwa wanafanya kwenye mafuta, hatuwezi kuendelea kuwa masikini. Tulinde uhuru wetu, Tulinde maliasili zetu.
 
Mnyonge mnyongeni ila mpeni haki yake!!!!!!!1
JK hakukubaliana na hao jamaa [M7 na Kg]. Kumbukeni jambo moja kwamba kabla hajaenda uganda alishasema tanzania itasaidia kutoa walinzi wa amani. lakini baada ya kile kikao cha uganda M7 kama mwenyekiti wa kile kikao alitoa maazimio ambayo hayakuwa na kipengele hata kimoja kilichotoka Tanzania. Tafsiri yake ni rahisi sana kwamba KAgame na M7 walimgeuka JK wakijua yeye ni kilaza watampelekapeleka tu bila kujua kwamba Tanzania bado ina marafiki wengi na wanaoiheshimu. Kawasiliana na Angola, Msumbiji, Sauth Africa, Zimbabwe na Namibia wakakubaliana kuwadhibiti hawa majambazi wawili. Kilichofuatia JK katumia mlango wa nyuma kuwadhibiti M7 na Kagame [jikumbushe udharura wa hicho kikao cha SADC kilichotanguliwa na kamati ya SADC ya ulinzi na usalama]. JK played a very smart game on this! we must aknowledge and praise his move!!

Mkuu Papa hata mimi kama umesoma bandiko langu naunga mkono azimio hili la SADC kupeleka neutral force Goma, DRC kuzima operesheni za waasi wa M23,tena naona wamechelewa sana.Hoja yangu niliyonayo na JK ni yeye kushindwa kuwaeleza ukweli akina Kagame na Museveni kwenye kikao cha awali cha Kampala na yeye kushiriki kutoa maazimio ambayo kwa kweli yalikuwa kama ya kitoto na yenye kuwabeba waasi hawa.

Nadhani JK was supposed to be firm on the matter na kuonesha kutokukubaliana na maazimio hayo.Kitendo cha yeye kushiriki kikao kile ambacho kilitoa maazimio ya Kampala bila kuonesha kuyapinga na baadaye kushiriki kikao cha SADC ambacho kimekuja na maazimio yanayokanyaga kikao cha Kampala (Hata kama ni mema na tunayaona ya busara) kinampunguzia credit na kama Rais anayeongoza moja ya majeshi imara Afrika alipaswa kuwaonesha akina Museveni kwa nini wanapaswa kuacha undumilakuwili na kusitisha miradi yao huko Goma.
 
Last edited by a moderator:
Sikubaliani na Kagame/Museveni kumshurutisha Kabila awe na power sharing na M23. Wanaongoza through fear mongering na ukabila ... wananchi wa Congo wapewe elimu ya political process kama njia ya kupata serikali wanayoitaka.
Vita inawaathiri wanawake na watoto .... soi it's a noble thing to go and protect our neighbors and let these people know that enough is enough!

Pamoja na hayo yote naomba mnijuze: Inakuwaje nchi kubwa na yenye maliasili nyingi kama DRC inatishiwa na "KANCHI" kama Rwanda?
 
Huwa sielewi hii kitu,tuna ndoto ya kuunganisha bara la Afrika huku tukiendelea kuligawa vipande! Kesho mtaigawa Kivu alafu baadae Kivu na Congo zitaomba kujiunga EAC ambayo tunaota ije kuwa nchi moja what a dream!!!

Ni tamaa za viongozi tu,Kwa mfano Tanzania ni nchi kubwa sana pia kuliko zote EA,unadhani mkuu DSN tukitofautiana solution itakuwa kuigawa pia?

Kongo ni ya Wakongo tuwaache waamue wenyewe bila kuwaingilia na cha kuwasaidia ni kuimarisha usalama na kulijenga upya jeshi lao ili lisimamie usalama bila kuingiliwa na watawala wenye uchu.
Mkuu wanaoifaidi Congo ni wageni, je itakuwa hivyo mpaka lini?
 
Pamoja na hayo yote naomba mnijuze: Inakuwaje nchi kubwa na yenye maliasili nyingi kama DRC inatishiwa na "KANCHI" kama Rwanda?

Kuna hoja kwamba DRC ni kubwa hivyo Jeshi la Kinshasa linashindwa kutoa ulinzi thabiti wa mipaka yake. By the way hoja hii ya ukubwa wa DRC imekuwa iko kwenye midomo ya Wahima wengi wakitaka nchi hiyo imegwe ili kuandaa nchi mpya ya Wahima. Hizi harakati za FDRL na sasa M23 ni sehemu ya mikakati ya akina Museveni na Kagame kujenga himaya hiyo mpya.
 
WanaJF,
Tukumbuke, Kabila mkubwa (Baba yake na Joseph) aliingia madarakani kwa msaada wa vikosi vya Rwanda na Uganda. Rwanda na Uganda sio kuwa walikuwa wanampenda sana Mzee kabila bali walikuwa na maslahi wanayonyemelea. Masharika mwa DRC, kuna kabila la wanyamulenge, hawa ni watutsi wenye asili ya Rwanda. Wanyankole wa Uganda (kabila la mseven) ni watutsi bila hata kuacha shaka lolote. Pamoja na kwamba Rwanda na Uganda walikuwa wanafukuzia mali asili za DRC pia nia yao kama walivyokuwa wamekubaliana na Kabila mkubwa ni kuanzisha kile kinachoitwa 'HIMA (TUTSI) EMPIRE, ambayo itamega sehemu ya mashariki mwa DRC na kuunganishwa na nchi za Rwanda na Uganda, pia tukumbuke Kagame alikuwa Mkuu wa Intelijensia wa Mseven kabla Kagame hajapata madaraka ya urais nchini Rwanda na Kagame aliingia madarakani kwa msaada wa vikosi vya Uganda.

Baada ya Kabila mkubwa kuingia madarakani, wananchi wa DRC walianza kupiga kelele kuhusu uwepo wa watutsi wengi kwenye serikali na hasa Jeshi la DRC. Generali Kabarebe ambaye kwa sasa ni Waziri kama sio Mkuu wa Majeshi ya Rwanda alikuwa Mkuu wa majeshi ya DRC wakati wa kabila mkubwa. Bizima Karaha (Jina halisi ni Bizimana) alikuwa member wa cabinet kwenye serikali ya DRC naye alikuwa mnyarwanda achilia mbali nafasi nyingine nyeti ambazo hadi leo wanyarwanda wamejichomeka. Sasa Kabila mkubwa baada ya kelele nyingi za wananchi wa DRC aliamua kuvunja makubaliano na kuamuru majeshi ya Rwanda kuondoka nchini DRC, kutokana na tamko hilo wote tunajua yaliyompata Mzee kabila.

Sasa hujuma za M23 mashariki mwa DRC, ni kagame na Mseven wanaotaka kujaribu kutimiza ndoto zao za kuanzisha na kjenga HIMA EMPIRE AU TUTSI EMPIRE. Bahati mbaya jumuia ya kimataifa imeshawashtukia kuhusu kusudio lao hilo. Lakini tutazame madhara ya kukosekana utulivu mashariki mwa DRC kwa Tanzania. Asilimia kubwa ya biashara zinazoendeshwa nchini DRC zinatokea Tanzania au zinafka DRC baada ya kuingilia Tanzania, kwa maana nyingine Tanzania kiuchumi inaitegemea sana DRC. Kuiacha DRC iendelee kuandamwa na hao watutsi ni sawa na kuacha uchumi wa Tanzania uzidi kudidimia kisa kagame na mseven wanataka kuanzisha hima empire na kuiba raslimali za DRC.

My take,
Acha tupeleke majeshi DRC ili tulinde miraji yetu, tufahamu pia kwamba sio rahisi kupigana na waasi waliozoea mazingira na jiografia ya mashariki mwa DRC lakini ni bora kufanya hivyo kuliko kusubiri na kushuhudia maslahi yetu ya kiuchumi yakianguka. Mugambe aliwahi kutoa pendekezo wakati ule Rwanda inaivamia DRC, yeye alisema, wakti Rwanda inapigana mashariki mwa DRC, Tanzania kama mwananchama wa SADC itoa ardhi yake ili vikosi vya SADC vianzishe mashambulizi vikitokea Tanzania kwenda Rwanda, Hapo Mhe. Mkapa aliona noma na kukataa pendekezo sahihi la Mugambe kwani lingmfanya kagame ku-withdraw majeshi yake ili aje atetee nchi yake kwa uvamizi huo. Tumuunge mkono mhe. Rais kwa hatua ya kuungana na wananchama wa SADEC kupelekea askari mashariki mwa DRC. lAKINI MWISHO, mashariki mwa DRC kuna waswahili wengi sana wenye mafungamano na watu wa kigoma, kwa hiyo kwa interest ile ile ya akina kagame na mseven na sisi ni hivyo. Haya wenye kujua zaidi tuchangia.
 
WOWOWO, naomba nikukumbushe kwamba hivi ni vikao viwili tofauti na JK siyo muwakirishi wa SADC kwenye EAC na vivyo hivyo kinyume chake. Kwa hiyo JK anakwenda kama fresh member kwenye EAC na SADC. Kama EAC inahitaji muwakirishi kwenye SADC itapeleka itatuma mjumbe wake na vivyo hivyo kwa SADC kwenye EAC. Kama EAC members wake ni Museven na Kagame ambao wanakuwa karibia theluthi ya wanachama wote, huoni wanaweza kuinfluence matokeo ya mkutano wote. JK hahitaji kubishana na watu ambao anajua kabisha upande wao katika mgogoro. Alichokifanya JK ni sahihi kabisa kuonyesha kwamba anakerwa na tabia zao za udumila kuwili. Nani kigeu geu hapa, JK anayefanya maamuzi yanayooneka kwa uwazi kabisa kwa kutangazwa na vyombo vya habari au Kagame na Museveni wanaowaunga mkono waasi, M23, halafu kwenye vyombo vya habari wanakataa. Dawa ya jeuri ni kuwa jeuri zaidi yake. Big up JK. Kwanza muonyeshe Kagame kwamba anaongoza mkoa mmoja tu kwa Tanzania wakati wewe unaongoza nchi kubwa mara hamsi ya kwake kwa dharau zake alizowahi kuwa nazo. Kwa kifupi, Kagame na Museveni kwa support ya USA na Ulaya wamekuwa na kiburi sana kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati. Sasa wataona moto wake, na hao washirika wao [USA na Ulaya] kwa kuwa wanatabia ya ku-use na ku-abuse, very soon watawatupa kama kondom iliyotumika. Ndipo Rwanda itarudi tena kwenye dimbwi la ukabila tena.

Nimefurahishwa sana na uamuzi wa nchi za SADC. Mara kadhaa nimekuwa siuamini huu muunganao wa EAC kwani kuna baadhi ya marais who can talk good with you but if you turn around they stub you on your back!. Nilishangaa kuona wanaottuhumiwa kuwasaidia M23 ndio hao hao wapo mbele kuuchukua mjadala wa kusuruhisha na ku dictate terms kwa rais Kabila. Keep it up nchi za SADC,kama alivyo n'golewa mreno kule Msumbiji,mkaburu kule South Africa,Namibia,Angola,Zimbabwe na Zambia,ndivyo wan,golewe wote wasiopenda amani waroho wa rasilimali na wanaoleta machafuko. Viva Tanzania,Viva nchi za SADC!
 
Tanzania ina nafasi kubwa juu ya mustakabali wa Congo na tutafaidika zaidi kuliko kuwa na Kenya na Uganda EAC. Kikwete amefanya maamuzi sahihi. Jeshi la Congo kwa sasa halina moral na inaonekana linadhoofishwa na Rwanda na Uganda kwa maslahi ya nchi hizi mbili. Kila mara wanasaidia waasi na mara waasi wanapopata ushindi, wanalazimisha lazima jeshi la waasi liwe integrated kwenye jeshi la Congo DRC. wengi wa hawa waasi ni Watusi na lengo la muda mrefu ni kujenga Hima empire. Mwisho wa siku Jeshi la Congo litakuwa na 50 -70% Watusi. Ukishakuwa na jeshi, kinachofuata ni nini! Kihoro alichonacho Kagame ni Jeshi la Tanzania pamoja na SADC kwenda Congo! For him, hii ni blow. Lile la UN ni useless. UN ingeweza kusaidia jeshi la SADC kwa kuliondoa lile la UN na majukumu yake yakachukuliwa na SADC ili gharama za UN zipelekwe SADC. Hii iwe ni hatua ya pili baada ya mahitaji ya nchi za SADC kule UN. Kuwa na stable DRC, tutakuwa na faida pia kiusalama!
 
Back
Top Bottom