WOWOWO
JF-Expert Member
- Aug 3, 2011
- 599
- 457
SADC yatengea waasi wa M23 Sh160 bilioni
JUMUIYA ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), imepanga kutumia dola 100 milioni za Marekani kukabiliana na kundi la waasi wa M23 Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Kiwango hicho ni sawa na Sh160 bilioni (dola moja kwa Sh1,600), kinatazamiwa kutumika kugharimia operesheni za vikosi vya kulinda amani ya jumuiya hiyo, ambavyo vinakusudiwa kutumwa eneo hilo lenye uasi.
Viongozi wa SADC waliokutana Dar es Salaam kwa kikao cha dharura kujadilia hali ya amani nchini DRC, walikubaliana kugharimia kikosi hicho na wamewaonya waasi hao kuondoka maeneo wanayokalia. Kikosi hicho kisichofungamana na upande wowote kinatazamiwa kutumwa Mashariki kwa Congo wakati wowote, baada ya kukamilika kile kilichoelezwa hatua za awali za utendaji ambazo zinaratibiwa na asasi ya ulinzi na amani (troika), ambayo inasimamiwa na Tanzania, Namibia na Afrika Kusini.
Tanzania na Afrika Kusini zimeahidi kuchangia sehemu kubwa ya gharama kufanikisha operesheni za kikosi hicho, uamuzi ambao umepongezwa na nchi wanachama wa SADC. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa vikosi vya SADC kutumwa nchi wanachama kuzima uasi.
Akitangaza maazimio ya kikao hicho, Rais Jakaya Kikwete alisema nchi kumi eneo la Maziwa makuu zimekubaliana kuunda jeshi hilo, litakalokuwa na askari 4,000 kukabiliana na ghasia na vita ya mara kwa mara Mashariki mwa Congo.
"Kimsingi tumekubaliana kuunda jeshi na jukumu letu la kwanza litakuwa kwenda kusimamia hali ya amani huko Congo, pande zote zimekubaliana kuchangisha fedha kuliwezesha jeshi hilo kuendesha operesheni zake kwa ufanisi zaidi," alisema Rais Kikwete.
Alisema kikao cha viongozi wa SADC wamelaani vikali hujuma zinazoendelezwa na waasi wa M23, ambao hivi karibuni walifaulu kuteka mji wa Goma na maeneo mengine ya jirani.
Source: Sadc yatengea waasi wa M23 Sh160 bilioni - Kimataifa - mwananchi.co.tz
My Take:
Ni juzi tu JK kahudhuria kikao cha Kampala akiwa na Kagame na mwenzake Yoweri Museveni na kukubaliana Joseph Kabila kuingia kwenye mazungumzo na Waasi wa M23 na baadhi ya maazimio ambayo wadadisi wengi wa mgogoro wa Goma, DRC waliyaona ya kitoto na yaliyolenga kuwabeba waasi hao wa M23 ambao kwa mujibu wa Taarifa za kichunguzi za UN wanatajwa kusaidiwa na Rwanda pia Uganda.
Wadadisi wengi walienda hatua moja mbele na kuhoji uhalali wa Museveni na Kagame ambao kimsingi ni watuhumiwa katika mgogoro huo kuwa mstari wa mbele kusaka suluhu na hata kuratibu mazungumzo kati ya Kinshasa na waasi hao.
Swali langu ni je kwa maazimio hayo ya SADC kuunda jeshi huru kukabiliana na Waasi wa M23 kinyume na makubaliano ya Kampala, JK kawageuka Museveni na Kagame? Au katika kikao hicho alikosa ujasiri wa kuwaambia hawa jamaa HAPANA lazima operesheni za waasi zikome Goma? Na nini hatma ya mahusiano kati ya Dar es Salaam, Kampala na Kigali?
NB: Naunga mkono wazo hili la SADC ingawa limekuja kwa kuchelewa. Tazameni picha hapo juu JK anaonekanaje?