JK Interview, Kigugumizi

Katoma

Senior Member
Joined
Mar 11, 2008
Posts
133
Reaction score
10
ngoja nim'kanumba mheshimiwa.


[ame]http://www.youtube.com/watch?v=hCxY2otR6w8&feature=related[/ame]
 
hivi huyu analazimishwa kuongea kiingereza si aongee kiswahili watamuwekea mkalimani.hamuoni mwenzie Hugo Chavez...hahaaaaa
 
Lugha tatizo!!! Thinking in "Swahili" and speaking in "Foreign language".

hahaha
mwalimu wangu wa kifaransa alikuwa anasema kipimo cha kujua lugha ni uwezo wa kuota katika hiyo lugha!hahahaha Sasa sijui mwenzangu anaotaga kwa kiingereza!
 
.......the dangers are real and we pray that the recession does not contue........wenzako wanweka mikakati, wewe unasali??!!
 
Mwanzo nilicheka ila nilipoona video nyingine, nimegundua kuwa ANA KIGUGUMIZI. Na huwezi kumcheka mtu kwa KILEMA. Imebidi nifute ujumbe wangu wa mwanzo. Nafikiri hata kwa Kiswahili ana kigugumizi ila huwa anaongea taratibu ili kukificha au anacheka na hamkioni.
 
Last edited:
Lugha tatizo!!! Thinking in "Swahili" and speaking in "Foreign language".
Sioni tatizo ... naona yuko better hata kuliko maprof wengi wa kitanzania niliowahi kusikia wakihojiwa (ambao by the way wanaotumia kiingereza kazini kila kukicha).
 
Jamani hapa si kigugumizi ni lugha ya ung'eng'e haipandiiii!

English is not our mother tongue,we have to agree on that. Viongozi au wanasiasa wachache sana wanaoweza kuongea english fluently bila kutafuna tafuna maneno.Ni marehemu Nyerere na Salim A. Salim waliokuwa wanakiongea Kiingereza saafi. Mkapa wanasema naye anajaribu lakini mimi nafikiri ni kile cha kuandika halafu anasoma kama kasuku.

Anachozungumza Rais Kikwete hapa ni kujaribu kuunganisha vipande vipande vya kiingereza(broken english).Ukisikiliza kwa makini hata tenses anazichanganya hapa.

Tatizo letu ni kuwa tunakionea haya Kiswahili. Yeye angetafuta Mmarekani aliyekaa Bongo miaka kadhaa akamsaidia kuongea lugha hii ya watu.

Nashauri viongozi wetu waandamizi wanapokwenda ng'ambo wawe wanatafuta wakalimani itawasaidia.

Makoye
 
Kigugumizi kinamjia anapofiki kwa kikwere halafu anazungumza kiingereza!! Asingekuwa na kigugumizi kama angezungumza kikwere halafu mtu mwingine akatafsiri, kwa mtindo huo angekuza lugha ya kwao!!.
 
chonde chonde makoye..teh tehhhhh
 
Tatizo siyo lugha tatizo ni kwenda kwenye interview mtu haujajiandaa. Inawezekana majibu aliyo toa hapo ni spontaneous na wala hakujiandaa ata jibu vp maswali.
 
Kigugumizi kinamjia anapofiki kwa kikwere halafu anazungumza kiingereza!! Asingekuwa na kigugumizi kama angezungumza kikwere halafu mtu mwingine akatafsiri, kwa mtindo huo angekuza lugha ya kwao!!.

Bulesi Mkulu akiongea Kikwere hana kigugumizi.....duuu hii kali ya wiki, sasa kikwere ataeleweka na wangapi?
 
Tatizo siyo lugha tatizo ni kwenda kwenye interview mtu haujajiandaa. Inawezekana majibu aliyo toa hapo ni spontaneous na wala hakujiandaa ata jibu vp maswali.

Hili nalo linaweza likawa lilichangia ila ukiangalia na kusikiliza kwa makini utaona kabisa hata maswali kama vile yalikuwa hayaeleweki au ndo tusema lugha ilikuwa 'more difficult'
 
mhhhhhhhh!! sijui ndio kigugumizi au ndio..................!!!!!!! Muammar al- Gaddafi alihojiwa Larry king live CNN kwa raha zake alikuwa na mkalimali.
 
mbona message inafika? what is wrong with that? mbona mizungu haijui kiswahili na wakiongea tunakubali kuwa hawajui kiswahili? iweje rais wetu ananjaribu kuongea lugha yao hata kama siyo nzuri lakini ni much better than angeongea kiswahili na atumie mkarimani.

Tatizo la watanzania ni ulimbukeni, kwani usipo ongea kiingereza ndo kwamba hujui? au huja elimika? Tuache ulimbukeni wa kujiona tu wa magharibi kumbe ni maskini wa tanzania tu!!!

Big up JK!!!!
 

Magezi wewe ndio mwenye matatizo ya kujipendekeza kwa Mkulu. Viongozi wetu akiwemo Jakaya ndio malimbukeni kwani wanadhani wakihutubia au kujibu maswali kwa lugha zao wataonenekna hawajasoma, unfortunately wakizungumza hiyo lugha ya malkia ndio wanaonyesha ukihiyo wao.Viongozi wetu tatizo lao ni lack of confidence mbona wenzao wanaume wa shoka kama Chavez na Gadaffi wanatumia lugha za kwao wanapohutubia!!
 
nimecheka sana maana sijui mkuu huwa nafanya nini wakati mwingine
anatka kuwa kama kanumaba yaani ni aaibu ana kwa mkuu wa nchi kama huku kuwa hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…