JK Era; Miaka 10 mifupi ya bunge Imara na "vibrant democracy"

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,597
46,215
Wakati wa utawala wa Jakaya Kikwete ndipo tuliposhuhudia bunge lilichongamka, likiwa na mijadala ya nguvu na mikali sana. Ni wakati ambapo kazi ya bunge ilikuwa zaidi ya kuishauri serikali, bunge lilikwenda mbali zaidi kujaribu kuisimamia serikali.

Mambo 7 yanaacha alama kubwa ya kipindi hicho cha mwaka 2005-2015

1.Huo ndio wakati ambao Waziri mkuu, Mizengo Pinda alilia hadharani ndani ya bunge kwa hoja za wabunge,

2.Huo ndio wakati tuliposhuhudia Waziri mkuu akistaafu kutokana na presha ya bunge na mawaziri kadhaa pia. Jambo ambalo ni nadra sana kwenye siasa za Africa.

3.Tulishuhudia Mwanasheria mkuu wa serikali akijiuzulu katika kipindi hiko kwa presha kubwa ya bunge pia.

4.Ni wakati ambapo majadiliano ya bunge yalionyeshwa live

5.Ni wakati ambapo kiongozi mkuu wa upinzani alipewa nafasi na hadhi yake anayostahili bungeni.

6.Tulishuhudia wanasiasa wa vyama tofauti wakipingana bungeni halafu wakikutana kucheza dansi baadaye. Tulishuhudia pia kumuona Rais na viongozi wa upinzani halisi.

7. Tulishuhudia maspika wa bunge wawili walioacha alama angalau kidogo za uhuru wa kiti cha spika

Hayo ni mambo nadra sana kuyaona kwenye nchi za demokrasia dhaifu.Huenda zilikuwa ni "busara tu" zilizotumika.
 
Huyu huyu JK ambaye baadaye tulimuita "dhaifu".... na yeye akagundua kumbe tunataka "mkali", na kutusaidia kufanya mipango aje mkali..

Huyu "Mkali" tukamuita Dikteta...
 
Kuna tofauti ya mtu mkali na katili. Inahitaji akili za kawaida kuelewa hii tofauti ila bahati mbaya sana kuna wabongo wengi ambao akili zao ziko chini ya kiwango cha kawaida.
Huyu huyu JK ambaye baadaye tulimuita "dhaifu".... na yeye akagundua kumbe tunataka "mkali", na kutusaidia kufanya mipango aje mkali..

Huyu "Mkali" tukamuita Dikteta...
 
Back
Top Bottom