JK bado hujapata sababu ya umasikini wa watanzania?

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Akiwa ziarani rais wa JMT alikiri kutojua chanzo cha umasikini,,akajibu hivi Hata mimi sijui sababu,huwa najiuliza kila siku swali hilo lakini sijapata jibu,mwisho wa kunukuu
Leo namwuliza JK ni zaidi ya mwaka tangu akiri kutojua sababu ya umasikini t Tanzania,na ni zaidi ya mwaka akijiuliza sababu,Je bado hajapata jibu?
Nawasilisha
 
JK.jpg Teh teh teh teh the. I actually don't know why my country is so pure!
 
Bwanae, acha hizo matani zako kwa Mhe Kikwete.

Akapate wapi hizo sababu wakati kwake yeye mifuko yooote imejaa utajiri; akitazama mfuko wa nyuma kushoto ni Tanzanite, na kulia ni makaa ya mawe kule Liganga. Kwingineko mfuko wa mbele kulia ni dhahabu wa msitu wa kule Bukombe, kulia ni Almasi ya mwadui Shinyanga.

Ndio, nasema Kikwete akajulie wapi umasikini wetu wakati pale Magogoni ni milo miraba minne kutwa mara tano hadi hapo ukimwambia kule Tandale bei za nafaka zimechachuka unategemea mtaelewana kitu bado????

Umasikini wetu Tanzania ni kama baridi kali sana tu kwa nyoka zisizo na magamba kule Ludewa; Watanzania tukaze buti hapa mpaka kieleweke tu!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom