JK aweka wino sheria ya posta, simu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK aweka wino sheria ya posta, simu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Apr 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  BAADA ya kusita kwa muda, hatimaye Rais Jakaya Kikwete ametia saini Sheria ya Mawasiliano inayolazimisha kampuni ya posta na simu kujisajili kwenye Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE).
  Hadi mwishoni mwa juma lililopita, Rais Kikwete alikuwa amesaini sheria sita na kutobariki sheria hiyo iliyoelezwa kuwa inakiuka masharti ambayo makampuni toka nje yalipewa wakati yakiwekeza nchini kutokana na kifungu cha 26 kuyabana kujisajili DSE.
  Kumbukumbu za Bunge kutoka katika hati ya yatokanayo na kikao cha kwanza cha Bunge kilichofanyika Aprili 13 mwaka huu, zinaonyesha miswada aliyosainiwa na Rais Kikwete
  kuwa ni wa Sheria wa Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2009 na wa Baraza la Usalama wa Taifa wa mwaka 2009 (namba 8 ya mwaka 2010).
  Mingine ni Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Ukunga ya mwaka 2010, Sheria ya Usajili na Usanifu wa Majengo ya mwaka 2009 (namba 4 ya mwaka 2010), The supplementary appropriation (for the Financial year 2009/20100 begin_of_the_skype_highlighting 2009/20100 end_of_the_skype_highlighting ya mwaka 2009, marekebisho namba 3 ya ziada ya sheria kwa mwaka 2009 na namba 2 ya mwaka 2010.
  Taarifa za rais kuiruka sheria hiyo ya makampuni ya posta na simu zilivuja na gazeti hili kuripoti wiki iliyopita.
  Habari zililidokeza gazeti hili kuwa Rais Kikwete alikataa kusaini sheria hiyo akitaka muswada wake ufanyiwe marekibisho katika kifungu cha 26 ambacho pamoja na mambo mengine, kinabana makampuni ya simu kujisajili DSE kwa lazima.
  Kifungu hicho kimepingwa na kampuni za simu nchini wakati mjadala huo ukijadiliwa kwenye mkutano wa 18 wa Bunge mjini Dodoma, zikitaka kifungu hicho kilegezwe.
  Said Arfi, ambaye ni msemaji wa kambi ya upinzani katika mambo ya mawasiliano, sayansi na teknoolojia, alionyesha kupinga kifungu hicho wakati akitoa maoni ya upinzani kuhusu sheria hiyo.
  Upinzani huo wa kambi ya upinzani na kampuni za simu, unaelezwa na chanzo hicho cha habari kwamba ulikuwa na nguvu za hoja ambazo zilimshawishi Rais Kikwete kusita kutia saini za kubariki muswada huo kuwa sheria.
  Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Peter Msolla alisema: "Sijapata taarifa hizo, lakini pia rais halazimishwi kusaini au kutosaini muswada wa sheria... yeye mwenyewe ndiye anajua na ana mamlaka hayo."
  Chanzo cha habari kilifafanua kwamba rais aliona ni vema serikali ikaweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji kuwekeza hisa zao DSE na si kulazimisha kama kifungu cha muswada huo kinavyosisitiza.
  "Rais amekataa kusaini muswada na unarudishwa bungeni ili ufanyiwe marekebisho. Serikali imeleta mapendekezo ya kubadili section (sehemu ya) 26, its a blow to bunge and Msolla (ni pigo kwa Bunge na Msolla-Peter)," kiliweka bayana chanzo hicho.
  Muswada huo pamoja na mambo mengine ulikuwa ukitoa nafasi pia kwa kampuni za simu kutumia miundombinu ya pamoja katika kupitishia na kutoa huduma za mawasiliano.
  Lengo la mpango huo lilikuwa ni kupunguza athari za wingi wa minara ambao unaweza kusababisha mwingiliano wa masafa na hivyo kuwa na athari kwa binadamu.
  Kampuni kubwa za simu nchini ni Vodacom, TTCL, Zain, Tigo na Zantel huku kampuni nyingine zikichupuka kwa kasi kama Benson Informatics (BoL), Six Telecoms.
  Jana Spika Samuel Sitta alilieleza bunge kuwa Rais Kikwete amesaini miswada miwili ya sheria za gharama za uchaguzi na wa makampuni ya simu na posta.

  http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/801-jk-aweka-wino-sheria-ya-posta-simu
   
 2. d

  damn JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ameisoma?
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu asikimbilie kusaini tu je ameisoma na kuelewa?we mwache tu ....kwanza kasaini lini wakati yuko USA?na akitoka huko atapita TIMBUKTU kidogo ndo arudi
   
Loading...