Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,180
- 664
wakuu mbali ya kupiga kelele sanahapajamvini tujitahidi kujituma ili tuweze kuwasaidia ndugu zetu wanyumbani.
na kujiletea maendeleo yetu na jamii zetu. mengi muuungwana katukumbusha hapo chini
Muishio ughaibuni msisahau Tanzania - JK
2007-10-25 10:05:52
Na Maura Mwingira, Paris
Rais Jakaya Kikwete amewakumbusha watanzania wote wanaoishi nje kutosahau kuendeleza walikozaliwa na kuwaendeleza ndugu zao ambao wamewaacha nyumbani.
Rais alitoa wito huo wakati akiongea na watanzania wanaoishi nchini Ufaransa.
Alisema tofauti ya wao kuishi ?majuu? itajidhihirisha kwa kuboresha maisha ya jamii yao, ikiwa ni pamoja na kujenga makazi bora.
Aliwataka pia kukumbuka kuwekeza nyumbani na kuwavutia wawekezaji na watalii kuja Tanzania, lakini pia aliwataka wasiogope kurudi ?Bongo? pale watakapoona maisha ya ughaibuni yamewashinda.
Akifafanua kuhusu uboreshaji wa miundombinu, Rais aliwaeleza watanzania hao hatua ambazo zinachukuliwa na serikali za kulifufua shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania).
Hata hivyo, amewakumbusha kuwa Tanzania bado ni nchi maskini sana ambayo wastani wa Pato la mtu kwa mwaka ni Dola za Marekani 370 kwa mwaka, hivyo wasitarajie miujiza itakayoibadili nchi hiyo haraka haraka na kuwa nchi yenye pepo kama zilivyo nchi zilizoendelea.
Alisisitiza kuwa hata Roma au miji mingine maarufu duniani haikujengwa mara moja, lakini pamoja na changamoto mbalimbali serikali imejipanga vema kuwaletea hali bora ya maisha nafuu wananchi wake.
Kuhusu hali ya kisiasa, demokraria, utawala bora na vita dhidi ya rushwa, Rais alisema kuwa kwa ujumla hali ya kisiasa ni shwari sana, na kwamba hali ya siasa imekuwa hai (active) na kwamba uhuru wa kidemokrasia umeshamiri sana, jambo alilosema ni zuri.
Rais pia aliwaambia Watanzania hao kuwa serikali haitakuwa tayari kuwasaidia watanzania wanaoishi nje ya nchi ambao watajiingiza katika vitendo vya uvunjaji wa sheria za nchi wanazoishi.
Aliwataka kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za wenyeji wao na hasa kwa vile hakuna aliyewalazimisha kwenda huko, bali walikwenda kwa hiari yao wenyewe.
?Lakini wakikusingizia umeiba ili hali wewe hukuiba na ikathibitishwa hukuiba basi hapo serikali itakutetea kwa hali na mali,? alisema.
SOURCE: Nipashe