JK atoa Pole | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK atoa Pole

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Oct 20, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  [h=1]Rais Kikwete[/h]Written by Ghalib // 20/10/2012 // Habari // 8 Comments


  Rais wa Tanzania Jakaya kikwete
  Rais Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema kuomboleza kifo cha askari polisi Said Abdulrahman aliyuawa kikatili visiwani Zanzibar.
  Abdulrahman wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), aliuawa kinyama kwa kupigwa mapanga kichwani na mikononi usiku wa Jumatano wiki hii katika eneo la Bububu wakati akirejea nyumbani baada ya kazi kazi.
  “Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na taarifa za kuuawa kikatili kwa askari wetu Said Abdulrahman wa kikosi cha Kutuliza Ghasia usiku wa tarehe 17 Oktoba wakati akirejea nyumbani kwake, baada ya kukamilisha zamu yake ya kulinda usalama wa raia na mali zao kwa siku hiyo,” alisema Rais Kikwete.
  “Kitendo hiki cha mauaji ni kitendo kiovu, ni cha kikatili na kinachostahili kulaaniwa na kufanyiwa kila aina ya uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria haraka iwezekanavyo,” alisema Rais Kikwete katika salamu hizo.
  Alisema anaungana na familia hiyo kumwomba Mwenyezi Mungu, ailaze roho yake mahala pema peponi .
  CHANZO: NIPASHE
  Zanzibar hakukaliki
  Huko Zanzibar, hali ya usalama iliendelea kutoweka kufuatia kuongezeka kwa ghasia zinazoaminika kufanywa na wafuasi wa kundi la Uamsho.
  Wafuasi wa kundi hilo juzi usiku walivamia makaburi ya Wakristo na kuyaharibu ikiwa ni pamoja na kubomoa misalaba, huku wakitishia kuchoma moto Kanisa la Anglikana.
  Watu hao pia waliharibu hosteli inayomilikiwa na Kanisa la Anglikana Mkunazini, huku wakitishia kufanya uharibifu zaidi.
  Kutokana na hali kuwa tete zaidi, baadhi ya wakazi wa Unguja ambao ni Wakristo wameanza kuukimbia mji huo, ambapo jana zaidi ya watu 60 waliwasili katika bandari ya Dar es Salaam.
  Kuchafuka kwa hali hiyo kumeiweka Serikali ya Umoja wa Kitaifa katika wakati mgumu hasa kufuatia hatua ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka CCM kususia vikao vyake juzi wakipinga ghasia hizo na kuwataka wakuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Bara na Zanzibar kujiuzulu.
  Tanzania Daima


  [h=4]Related Posts[/h][h=3]FARID ACHA UTOTO[/h]
  [h=3]Baraza la Wawakilishi[/h]
  [h=3]Vipeperushi vyasambazwa Zanzibar, vya watia khofu wakristo[/h]


  [h=3]Waandishi wako katika hatari[/h]
  [h=3]Vipindi vya Uamsho vyapigwa marufuku[/h]

  [h=3]8 Comments on "JK atoa Pole"[/h]


  1. abdulmajid 20/10/2012 kwa 10:50 mu · Jibu
   fitna tupuu za mfumo kristo sasa MOHAMED ABOOD NA KAMANDA DINYO WAJIUZULUUU kwa kulitia taifa kwenye vuruguu balozi wa tanganyika nchini zanzibar imekukuta wakaru wamakara lwaa……….
  2. Abdullahu 20/10/2012 kwa 11:14 mu · Jibu
   JK Kuuliwa kwa polisi ni funzo kwa wale wote wasioitakia mema Zanzibar.
   Kuanzia viongozi, Askari wote, pamoja na wanamaskani wa CCM hasa Kisonge.
   Wajue linapotokea vurugu mtu yeyote anaweza kufa kwani kifo hakichagui mtu.
   Fitna, matusi na ubaguzi hazitosaidia katika kuijenga au kuikomboa nchi yetu.
   Kila mtu anawajibu wa kumuheshimu mwenzake.
  3. last-warning 20/10/2012 kwa 11:26 mu · Jibu
   Wewe rais wa tanganyika tunajua wazi kuwa wewe umeekwa kwa lengo la kuulinda msalaba na kuwadhalilisha waislam,tunaapa waislam wote wallah wabilah hatutokusamehe hadi siku ya kiyama,umefikia step ya kuwapa pole wale waliodhalilisha kitabu cha allah na kuwaahidi utawashulikia wote waliotetea kitabu kile,na leo unatoa pole kwa askari moja alieuliwa lakini unasahau wazanzibari wanaopigwa risasi kila siku kwa amri yako wewe,tunaapa tena huku tukiwa tumeshika kitabu cha allah hatukusamehe hata ufanye jambo lolote la kuridhisha waislam na hatuamini kama wewe ni muislam.
  4. santorini 20/10/2012 kwa 11:33 mu · Jibu
   CCM wamefanya vitimbi na sasa M/Mungu amepindua vitimbi vyao hawana pa kushika.
   Hakuna kupunguza kasi ila kuzidisha kasi ya mapambano na mamluki.
   Mdomo wa kisonge umepigwa na kiarusi,maskani imetokwa kinu.
   Mohamed aboud daiper zote hazimfai.
   Nguvu ya wananchi ndio itakayo simamisha Dola kamili ya zanzibar.
   Muaamsho muwaidh wetu na kamba ya M/Mungu ndio ahadi madhubuti tuliyoahidiwa ushindi mbele za maadui wa haki.
   JK muuaji mkubwa ,mpinzani wake bagamoyo alituma askari kumuua lakini M/Mungu alimhifadhi
   majaraha aliyoyapata yanatosha ushahidi mbele ya M/Mungu kujieleza na aliekufa katika tukio hilo ni askari wake mwenyewe ,ama kweli mchimba kisima —————————–
  5. last-warning 20/10/2012 kwa 11:54 mu · Jibu
   Huyu jk kila siku unaskia anaanguka kwenye majukwaa nini kinamsibu??hakai akafikiria kwanini yanamfika haya?nataka aweke polisi kila sehemu ila ajitahidi asisahau kueka polisi kaburini kwake waje wapambane na malaika coz yeye anajiona kwa sababu anatoa amri kwa allah wewe utakua zaidi ya mtumwa.,
  6. Habib 20/10/2012 kwa 12:00 um · Jibu
   ***UNAFIKI WA VIONGOZI WA SERIKALI***
   .Akiuliwa askari mmoja tuu basi inakua kesi kuuubwa hadi kufikia kupeana pole (za kinafiki), lakini RAIA ata wakiuliwa 100 basi inakua ni halali kabisa na wala sio kosa!!!
  7. last-warning 20/10/2012 kwa 12:01 um · Jibu
   JK TUNAMUOMBA ALLAH MUFARIKI WEWE NA MWINYI TUKUEKEENI MISALABA COZ HAMUNA TOFAUTI NA HAWA WANAOPENDA MSALABU NA MTUME WETU AMETWAMBIA KAMA TOFAUTI YETU SISI NA WAO NI SALA NA SIFA YA SALA INAAMRISHA MEMA NA KUKATAZA MABAYA ILA WEWE UNAAMRISHA MABAYA NA KUKATAZA MEMA
  8. makame silima 20/10/2012 kwa 12:16 um · Jibu
   Ama kweli ccm ni mfumo Kristor? Na ndio maana hata viongozi wetu wa Serekali wajitao waislamu wamejiegemeza huko kwa kufanya kazi na maelekezo ya maaskofu na Kanisa Katoliki.
   Hivi kweli ukandamizaji huu unaotokea Dar kukandamizwa waislamu chini ya Amiri Jeshi Mkuu Jakaya Kikwete haoni au ndio kujipendekeza na Kanisa?.
   JK kutatua matatizo hakuhitaji nguvu za kijeshi kunahitaji busara na maelewano tu, nguvu hazizai faida ispokuwa hasara kwa Taifa unaloliongoza.
   Maandamano ni haki na huhitaji kuomba kibali bali ni kuwarifu tu Jeshi la polisi ili kuweka ulinzi , sasa kuzuia na kuwabana sauti wananchi ni kuwanyima haki yao ya kimsingi kujieleza na kutowa dukuduku lao.
   Huu ni ubakuzi wa Serekali ya Jk chini ya Mwevuli wa Kanisa na Dodoma, Maara ngapi maskofu na wafuasi wao hufanya wanalolitaka bila Serekali kusema kwii.
   Maaskofu wamefunguliwa mlongo (Open doors)milango iko wazi wakati wowote Ikulu kuonana na rais bila kizuwizi chochote na maskofu wamehamia huko kuiongoza Serekali na kuipa maelekezo.
   Vipi leo viongozi wengine wazuiliwe jambo hilo na kuwekewa pingamiizi na vishingizio vya kila aina?.
   Jee Watanzania chakujiuliza hii ikuli ni kwa ajili ya Kanisa Katoliki tu?, au waimbe wao Maskofu lakini Akilia Bundi huambiwa Uchuro?.
   Huu ni ubakuzi Jk wa kutenga matabaka, wewe ulitakikana usikilize Pande zote za Shilingi sio uegemee upande moja tu wa shilingi.
   Jengine ni kusikitishwa na kifo cha Koplo Saidi Abrahama kuliwa kinyama Zanzibar?
   a). Jee hukusikitishwa na kuuliwa kwa mtoto wa miaka 14 Bububu kupigwa risasi ya moto na Jeshi la Polisi? Au Koplo Saidi ndio wenu lakini huyu mtoto wa Ki-Zanzibar sio wenu ni Damu ya Utomvu Nyeupe Koplo Saidi yeye ana damu nyekundu JK?.
   b). Jee Mh Rais wa watanzania JK hukusikitishwa kupotea kwa mazingira ya Utatanishi raia wako Sheikh Faridi Hadi ndani ya nchi yako?. Na vipi baada ya kuonekana Sheikh Faridi ulimpa pole gani kutokana na usumbufu alioupata na TORTURE alizofanyiwa na majasusi walio m- KIDNAPPED raia wako?.
   Wewe ni mnafiki na mbaguzi na ndio ukaona Wazanzibar hatutaki Muungano kutokana na ubaguzi wenu wa kuyagawa matabaka ya Zanzibar na kupenyeza Sumu za ubakuzi zidi ya Wazanzibar .
   Watanganyika Fujo za Tanganyika zinahusiana vipi na Wananchi wa zanzibar kubuguziwa haliyakuwa walikuwa kimywa? Kwa kipindi hishi wananchi wa Zanzibar walio amua kutulia na kusahau yalio pita bada ya kipindi kirefu cha kupandikiziwa sumu za DIVIDE AND RULE.
   Fujo za Zanzibar wakubeba jukumu ni Serekali ya Tanzania katika kitengo cha Usalama wa Taifa, wao ndio walokuwa chachu na sosi ya yaliotokea Zanzibar.
   Watanganyika wakishirikiana na genge la Seif iddi ndio wanaohatarisha amani iliopo Zanzibar, vipi mtu katulia hajafanya Fujo Mumteke na Kum –TORTURE?, halafu museme wafuasi wake wamefanya fujo?.
   Huu ndio ubaguzi Ccm na nchi ikiendelea katika misingi hii basi haitotawalika, kwa vile kila raia ana haki sawa na mwenzake.
   FUJO LA TANGANYIKA NIMAMBUKIZI YA KULETEWA, CCM ZANZIBAR WANAINGIZWA KATIKA MDUNDIKO ULOKUWA SI WAO.
   Baada ya kipindi kirefu Wazanzibar kuishi katika maisha ya sokuwa matulivu na kuamuwa hivi sasa kusahau tafauti zao za kisiasa na kijamii.
   Watanganyika wakishirikiana na wale ccm watu wa nyumba ya motoni Seif Idd na genge lake , wanafanya kila iwezekanovyo kuturudisha kule tulikotoka.
   Hii kukamatwa kwa Sheikh Faridi walijuwa tosha kuwa Wazanzibar hawatokubali katu hata kuku ukimchukulia mtoto wake basi hakubali atakuparura vipi leo watu wawe kimya tu, huku kiongozi wao ka – disappeared?.
   Hizi zilikuwa ni isabu za kutuletea Watanganyika ili tushafua Amani ilokuweko Zanzibar na kuturudisha kule tulikotoka hawa tunao waita ndugu zetu wa damu Watanganyika.
   Utulivu wa zanzibar wenzetu unawaumiza na wanajaribu kufanya jitihada ili ubomoke na baadae wakae pembeni watusheke kwa vile hawana dada wala kaka huku, kila tukikamatana machati wao hufurahia ugomvi wa ndugu .
   Jee hawa kweli wanatutakia mema?,
   Angalia sumu za media ya Tanzania Daima newspepa wanavyojaribu kutumia kila kutokeapo kuto kufahamiana wazanzibar hupenyeza sumu kwa style ya ukungu wa kiza .
   Nikinukuu kipande hichi cha Tanzania daima.
   Kutokana na hali kuwa tete zaidi, baadhi ya wakazi wa Unguja ambao ni Wakristo wameanza kuukimbia mji huo, ambapo jana zaidi ya watu 60 waliwasili katika bandari ya Dar es Salaam.
   Jeshi, FFU wazima maandamano Dar
   Jee hawa ni ndugu zetu kweli wa Damu au ni wapandikizaji sumu na ubaguzi wa kidini kwa jamii ya watu wa Zanzibar ambao %99 ni waislamu?.
   Lakini maneno ya Allah hayendi kinyume na asemavyo M/mungu kuwa hatomficha mnafiki yoyote na kwa wale wazulumiwa basi duwa yao wakiomba M/mungu ataishuhulikia tu, na kwa mwenye kuzulumu hatofaidika chochote ispokuwa hasara.
   Mungu ibariki Zanzibar na watu wake na uzidi kuwafishuwa wanafiki na kuwapiga chapa ya unafiki, kwa hapa Zanzibar tayari tunalo kundi la watu hao wenye shapa tayari.

   
 2. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hii thread inatakiwa iwe hivi: Raisi JK atoa Pole. Kwani haya ni mamlaka makubwa kabisa katika nchi. Nanyi munaotoa maoni ya kukashi kwa kuuwa askari wa nchi, subiri sasa muone kwamba serikali ina mkono mrefu.
   
 3. Jangakuu

  Jangakuu JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  [h=2]SMZ yapiga marufuku urushwaji wa matangazo ya "Uamsho"[/h]20/10/2012
  0 Comments


  [​IMG]


  Add Comment


  [h=2]Vipeperushi vya vitisho kwa Wakristo, Viongozi vyasambazwa Zanzibar[/h]20/10/2012
  0 Comments


  Habari hii imenukuliwa kutoka ZanziNews blog
  ---

  Vipeperushi vinavyotishia uhai wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar vimepeperushwa mjini hapa kufuatia ghasia zinazoendelea kwa siku ya tatu mfululizo.

  Kipeperushi kimojawapo kinasema: "CCM kosa letu kuwatia mbwa msikitini. Sasa tunasema kuwa basi tena litakalokuwa na liwe kwa sisi CCM basi tena umoja na CUF. Nyie CUF/Muamsho Abubakari Khamis Bakar (Waziri wa Katiba), Mussa (Kamishna wa Polisi) na Azizi (Kamanda wa Polisi Mkoa) mmeshazoea fujo na sisi sera yetu CCM sera yetu amani sasa mujiuzulu mumpishe Rais afanye kazi zake, Tumechoka na nyinyi juu ya mauaji ya askari wetu. Ondokeni murudi kwenu. Wewe Abubakar hukuanza leo na jana ufisadi kazi ya ufisadi umeizoweya hadi ulifungwa jela na mafisadi wenzako, mwishowe huku SMZ kumekuokoa."

  Wakati huo huo kuna waraka umesambazwa ambao umewatisha hofu waumini wa dini ya Kikristo nchini ukisema wote watakatwa vichwa. Waraka huo ambao unasemekana umetolewa na watu wenye kujiita jumuiya ya Uamsho umeandikwa na kusambazwa katika maeneo mbalimbali huku wenyewe wakristo wakipelekewa maofisini kwao.

  Akizungumza na masikitiko, Askofu wa Kanisa la Anglikan Mkunazini, Emmanuel Masoud amesema ni wakara ambao umewastusha Wakristo kutokana na maneno mazito yalioandikwa humo ambapo ndani ya wakara huo, "Maneno yaliandikwa humu yametushitua sana sisi waumini wa dini ya Kikristo hapa Zanzibar. Kwa kwa kweli sio jambo la kupuuzia ikiwa wanasema watatukata vichwa ni jambo la hatari kabisa" alisema Masoud.

  Wakizungumzia ukweli juu ya suala hilo, Sheikh Azzan amesema Jumuiya yake haihusiki na waraka wa aina hiyo na wao kamaWwaislamu hawana sababu ya kuwatisha watu kwa kuwa wanaamini Uislamu sio dini ya kuwabagua watu wala kuwatisha watu.

  Azzan alisema wapo baadhi ya watu ambao wanatumia propaganda mbaya za kutaka kuwagawa Wazanzibari katika kipindi hiki na ndiyo wanatumia kila sababu za kuwagawanya. Aliwatahadharisha wananchi kuepukana na propaganda kama hizo kwani zinaweza kuitia nchi katika pahala pabaya na kutoweka kwa amani.

  "Sisi hatuhusiki na waraka huo aliyetoa waraka huo ni watu ambao wanapingana na amani iliyopo lakini pia ni watu wenye kueneza propaganda mbaya za kutaka kuwagawa Wazanzibari, jambo ambalo sisi tunaamini hatuna ugomvi, na Wazanzibari wote sisi ni ndugu, hatubagui awe ni Mkristo au Muislam, awe mweupe au mweusi, hatuwezi kubaguana kwa kuwa misingi ya dini yetu imekataza kubaguana" alisema Azzan.
  Source: wavuti.com - wavuti
   
Loading...