Wasee,
Mie nilisha wahi kuuliza siku za nyuma, je ni nani amefanya study au poll ya kujua kwamba ni nini hasa opinions za waislam wa Tanganyika juu ya kadhi courts??........mie nasikia hasira na donge moyoni kwasababu watu wanatumia issue hii, waislam na uislam wao for cheap political gains!!! Wallah, huu ni ufisadi kushinda ufisadi...... hii issue ni ya kuiacha, yeyote atakae taka kuifufua basi mmuogope kwasababu si rafiki yenu.
Mie nimeishi Tanzania mpaka nafika 21yo, kwenye familia ya kiislam hasaaaa Dar na Tanga.....sikuwahi kusikia hata siku moja watu(ndani ya familia) wakizungumzia jinsi uislamu wao ulivyopungufu ati kwasababu hamna kadhi courts!!!........sasa leo ghafla bin vuu, haya yanatoka wapi??. Acheni kuwa na "blackboard mentality" meaning, watu wanawajaza ujinga, wanafuta, wanaweka mwingine nyie mmebung'aa tu kama jiubao kwenye ukuta darasani.
Wake up people.....hii ni "political IED," mnatumika, hawa jamaa ni opportunistics, wanataka ku-divide ili watawale/kushinda chaguzi kwa ku-avoid really issues........maisha na matatizo ya TZ ni bigger than Kadhi courts, get real pple.!!