JK ataka wanasiasa wasitumwe mijadala ya uchumi

JK ataka wanasiasa wasitumwe mijadala ya uchumi

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
2,274
Reaction score
305
JK amesema

Uwaziri ni cheo cha kisiasa na si vyema nchi kutuma mwanasiasa kufanya majadiliano ya uwekezaji wakati kuna wataalamu waliobobea katika sekta mbalimbali wenye uwezo wa kutetea maslahi ya nchi katika majadiliano na wawekezaji.

Aliyasema juzi jioni wakati akijibu swali la mmoja wa wajumbe wa mdahalo wa kwanza wa Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi (WEF)

Rais Kikwete alikiri kuwa watu kama mawaziri hawana uwezo mzuri wa kujadili na kutetea maslahi ya kibiashara katika mikutano hiyo kwa kuwa watapoteza kilichokuwa kikitarajiwa na akapendekeza kuwa, ni vyema kutumia wataalamu ambao wana uzoefu na mambo yanayojadiliwa na kushauri wapewe mazingira mazuri kutetea maslahi ya nchi.

Akasema kama linalojadiliwa linahusu siasa zaidi, hapo ndipo mahali muafaka kumtuma Waziri wa Mambo ya Nje ambaye atakuwa na uzoefu wa kisiasa kuliko mtaalamu.

My Take: Mbona haya yamekuwa yakisemwa kwa muda mrefu na watu mbali mbali bila kutiliwa maanani na serikali yake? ni mara ngapi wanasiasa hasa mawaziri wamekuwa wakikataa ushauri wa wataalamu mfano, mikataba ya Richmond(Dowans), IPTL, TRL,TICTS, ushauri wa Lipumba wasinunue Rada ya bil 40, waliambiwa wasinunue ndege ya ATC ni mbovu wakabisha nk, utakuta wengi wa wajumbe kwenye misafara ya kibiashara nje ya nchi ni wanasiasa na ndio wanaokuwa wasemaji wakuu wenyewe wanaita kuchangamkia dili, mambo haya ndiyo yanatuingiza kwenye hasara kubwa tunajikuta tunalipa fidia ya mabilioni ya shs kila siku, IPTL.

JK asiwe mnafiki asiishie kusema tu naye awe mfano aheshimu maoni ya wataalamu wake, watu wanamshauri asitie saini sheria mbovu za mikataba feki ya madini bado amepitisha halafu leo anatuambia nini, ma-dili mengi ya mawaziri wake ndiyo yanafanya wasikubali ushauri na hilo analijua wazi, mimi naona anajipendekeza kwa wageni aonekane na yeye amechangia kitu wakiondoka wala hafuati aliyosema he doesn't walk the talk, nafikiri hata hayo maoni yake ameyatoa kisiasa zaidi hayatoki moyoni.
 
Jamaa yuko out of phase always, no connection between what he says and what he does.
 
Mbona yeye ndio msafiri mkuu wa kutafuta wawekezaji nchi za nje au yeye sio mwanasiasa.
 
Hapo ndipo JK anatakiwa kufahamu kwamba wenzetu Mawaziri wao sio Wanasiasa, hivyo anapotoa majibu ya jumla nchi nyingine watamshangaa. Anachotalkiwa yeye kufanya ni kuondoa kabisa mfumo wa chama kimoja cha CCM kinacholazimisha Waziri (Mtaalam) ni lazima awe Mbunge (mwanasiasa).
 
It is high time someone told Jakaya to walk his talk; sometimes I suspect the guy is a somnambulist!! Hivi sasa waziri wake wa miundombinu anahangaika dunia nzima kutafuta wawekezaji , kwanini hamuambii kuwa shuhuri hiyo awaachie wataalam? Ubinamu kazini hauna tija ubakizeni huko msoga!!
 
Back
Top Bottom