JK asaini sheria za Bunge bila kuzisoma!

JK asaini sheria za Bunge bila kuzisoma!

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
242
Rais Kikwete aumbuka

Na Saed Kubenea


KUMBE Rais Jakaya Kikwete hakusoma sheria aliyosaini kwa mbwembe.
Sasa baada ya kugundua kasoro zake anataka ikarabatiwe kwa njia ya
kanuni, MwanaHALISI limeelezwa.

Hilo liligundulika katika mkutano wa wajumbe wa Halmashauri Kuu
(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wenyeviti na makatibu wa wilaya
uliomalizika wiki iliyopita mjini Dar es Salaam.

Taarifa za ndani zinasema, bila aibu na hasa kwa ujasiri wa
kiongozi mkuu wa nchi, Rais Kikwete alimuuliza Philip Marmo, waziri
wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, maana ya baadhi ya vifungu katika
sheria hiyo.

Lakini katika hali ambayo haikutegemewa, Marmo alijibu kana kwamba
anamkejeli rais, jambo ambalo lilistua wajumbe wa kikao hicho cha
juu cha utekelezaji wa sera za chama.

MwanaHALISI limeelezwa kwamba Rais Kikwete alistushwa na kifungu
cha sheria kinachotaka mgombea kuwasilisha katika ofisi za msajili,
taarifa ya fedha atakazotumia.

Kifungu hicho kinatoa siku saba kabla ya siku ya mwisho ya NEC
kutangaza majina ya wagombea.

Kifungu kingine kinachodaiwa kumstua kinahusu idadi ya wajumbe wa
kampeni. Kwa CCM, yenye hata vikundi vya ngoma na nyimbo kama ToT,
kuweka timu ndogo kunaweza kupunguza shamrashamra na kuathiri
kampeni.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, ilikuwa baada ya rais kupitia maeneo
hayo, alimuuliza Waziri Marmo iwapo kile alichokuwa akifafanua
kimetokana na sheria iliyopitishwa.

Naye Marmo, akiongea kwa sauti ya unyenyekevu alijibu, “…hiki
ndicho ulichosaini.”

Kwa kauli ya Marmo, Rais Kikwete alionekana kustuka na kusema, kama
hali ni hivyo, basi sheria itakuwa imeingilia hata mchakato wa
wagombea ndani ya vyama, kimeeleza chanzo chetu.

Taarifa zinamnukuu rais akihoji kwa nini “sheria imekwenda mbali
mno” na kuagiza papohapo kuwa wahusika waangalie ambapo sheria
inaingiliana na watengeneze kanuni zitakazoleta nafuu.

Rais amenukuliwa akimwagiza Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutengeneza
“kanuni vizuri” ili kuondoa mwingiliano unaoleta ugumu wa
utekelezaji.

Hoja ya maelekezo ya sheria mpya ya gharama za uchaguzi ilikuwa
moja ya ajenda za kikao cha NEC, wenyeviti na makatibu wa CCM
wilaya kutoka kote nchini.

Tarehe 17 Machi mwaka huu, Rais Kikwete alisaini hadharani na kwa
mbwembwe Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ikulu Dar es Salaam ambapo
hafla hiyo ilihudhuriwa na majaji, wabunge, viongozi wa serikali na
vyama vya siasa, mabalozi na waandishi wa habari.

Hata hivyo, sheria hii imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya siasa na
wanaharakati, kabla na baada ya kusainiwa kuwa itakuwa ya udhibiti
kwa wenye msimamo tofauti na watawala.

Aidha, siku tatu baada ya sheria hiyo kusainiwa, mbunge wa Karatu
(CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa alitupa kombora kwa kusema sheria
aliyosaini rais ilikuwa na vipengele ambavyo havikujadiliwa bungeni
na kwamba “viliingizwa kinyemela.”

Ubishi wa Mwanasheria Mkuu wa serikali, Jaji Frederick Werema
kwamba hakukuwa na chochote kilichofanywa kinyemela ndio umekuza
hoja ya Dk. Slaa na kufanya achimbue zaidi kshfa hiyo.

Katika kufukua, Dk. Slaa amekwenda hadi kwenye kumbukumbu za bunge
(Hansard) na kuthibititisha kuwa Kifungu 7 (3) ambacho kimo katika
sheria aliyosaini rais hakikujadiliwa bungeni na hivyo
hakikurekodiwa katika hansard.

Mtunga sheria huyo kutoka Karatu amesema pia kuwa chochote
kilichojadiliwa bila kuamuliwa na bunge kilikuwa kinatarajiwa tu
katika kanuni au fafanuzi za au ainisho za maneno na taratibu
lakini siyo katika vifungu vya sheria.

Katika majibu yake kwa kauli za Dk. Slaa, Jaji Werema alitetea
serikali na kuthibitisha kuwa kifungu hicho kiliwekwa na waziri
Marmo.

Dk. Slaa amesema katika andishi maalum, “Hakuna mwenye mamlaka,
hata rais hana mamlaka hayo, sembuse waziri.

“Baada ya mjadala katika Kamti ya Bunge zima, maneno yakikubaliwa
ndiyo hayo yanaingia kwenye sheria na serikali haina mamlaka ya
kwenda kuyarekebisha inavyotaka. Ndiyo maana ya kusema ‘kifungu
kimepitishwa,’ ” ameeleza Dk. Slaa.
Akiweka msisitizo, Dk. Slaa anasema, “Kitendo cha kuchomeka
kinyemela ni kitendo kibaya sana na kinapaswa kulaaniwa, kwa
sababu, kwa utaratibu huu wataalam wanaweza kuipeleka nchi pabaya
kwa kupenyeza jambo lolote wanalotaka wao hata kama halijajadiliwa
au limekataliwa na Bunge.”

Dk. Slaa anafafanua hatua ya serikali ya kuingiza mambo kinmyemela
katika sheria kuwa ni kosa la jinai na kusema hata kifingu
walichochomeka kinyemela kina madhara makubwa.

Kifungu kilichoongezwa na serikali kinataka timu ya kampeni
kukaguliwa na watendaji wa serikali ya CCM.

“Kampeni ndiyo inayobeba mikakati na siri yote ya uchaguzi.
Haiingii akilini kabisa kuwa serikali (pengine unayotaka kuiondoa
kwenye uchaguzi ambayo ndio haki ya msingi ya kila mgombea) ndiyo
inaweka mkono wake kwenye udhibiti wa mikakti hiyo,” anafafanua Dk.

Slaa.

Anasema kuweka kifungu kama hicho ni “wenda wazimu, kwa mtu yeyote
aliyefikiria jambo hilo, au anaandika tu kutoka mezani na au hajui
maana halisi na majukumu yake.”

Kutokana na kuibuka kwa kashfa hii, serikali sasa imeamua sheria
hiyo irejeshwe bungeni ili kufanyiwa marekebisho yanayostahili.
Naye Dk. Slaa tayari ametoa pendekezo: “Namna pekee ya kuepukana na
athari hiyo ni kwa serikali kukiri imefanya makosa, na ndio
ustaarabu bila kutafuta visingizio.”

Anasema serikali iwasilishe kwenye Mkutano wa 19 wa Bunge hili
ulioanza jana, kitu kinachoitwa “Miscellaneous Amendment” –
marekebisho ya sheria mbalimbali – na au ikichelewa sana katika
Bunge la Bajeti.

Wachunguzi wa mambo wanasema Rais Kikwete atakuwa amesikitishwa
sana na hatua ya wasaidizi wake ya “kumchomekea” vitu ambavyo
baadaye vinamomonyoa hadhi yake kama mkuu wa nchi.

Miongoni mwa wanaotajwa kuwa wamempotosha au wameshindwa kumsaidia
rais, ni pamoja na Jaji Werema ambaye ametetea uingizaji kinyemela
kipengele ambacho hakikujadiliwa bungeni.

Mwingine anayetajwa ni waziri Marmo ambaye ambaye nduye hasa
ametajwa kubuni na kuingiza maneno ya kifungu kinacholaaniwa.

Source: Mwamahalisi Issue No. 184
 
Kikwete amevunja sheria yake

Na Saed Kubenea

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kujihalalisha kwa fedha
badala ya sera.

Sasa kinahaha kutafuta mabilioni ya shilingi, siyo kwa ushindani,
bali kwa shabaha ya kuzamisha vyama vingine.

Ilikuwa Ijumaa wiki iliyopita, CCM ilipozindua mpango wa
kuchangisha Sh. 40 bilioni kwa ajili ya kile ilichoita “kampeni za
uchaguzi mkuu.”

Lakini ni majuzi tu Rais Kikwete alisaini sheria ya matumizi ya
fedha katika uchaguzi. Pamoja na kudhibiti matumizi ya fedha
haramu, sheria hiyo ilikuwa na saaha nyingine kubwa.

Roho ya sheria ambayo Kikwete alisaini kwa mbwembwe, ingawa tayari
imebainika kuwa itarejeshwa bungeni, ni hii hapa:

Sheria inalenga kupata “viongozi bila hila na jeuri ya fedha…”
Maneno mengine katika sheria hii ni muhimu lakini haya tunayonukuu
hapa ndiyo muhimu zaidi.

Sasa CCM imeamua kuchangisha fedha; kwa njia ya simu na kwa
kukusanya kutoka kwa walionazo. Ukumbwa wa kiwango cha fedha
kinachochangishwa, hakika ni wa kutatanisha.

Shilingi 40 bilioni (na zaidi) ni kiwango cha hila katika mazingira
ya Tanzania, pale kinapotumika tu kwa kampeni za uchaguzi wa chama
kimoja.

Kiasi hicho cha fedha ni cha jeuri ya aina yake katika jamii ambamo
umasikini ni sehemu ya maisha.

Ni wazi basi kwamba viongozi watakaopatikana kwa hila na jeuri ya
fedha, wataishi kwa hila na jeuri ya fedha juu ya vichwa vya
masikini ambao watazuiwa kukohoa.

Kwa CCM kuamua kuchangisha mabilioni hayo ya shilingi kwa matumizi
katika uchaguzi, chama hiki kimebwaga moyo wa sheria inayokataza
hila na jeuri ya fedha.

Kimefanya hivyo makusudi. Kwanza kinataka kutishia vyama vingine
kuwa “kiko juu” na hakina mshindani katika kuwa na fedha nyingi.
Pili, kinatoa ishara kwa wafanyabiashara wakubwa nchini kwamba
wakati wa kukichangia ndio huu na mchango sharti uwe mkubwa kuliko
siku zote.

Wafanyabiashara hawa wanajua vema kwa nini huwa wanachangishwa na
wao kukubali kuchangia, kama hawana manufaa na “kelele za siasa.”
Tatu, CCM ina mtaji mkubwa wa michango. Ni mwenyekiti wake
aliyesamehe watuhumiwa wa ufisadi waliodaiwa kuchota mabilioni ya
shilingi kutoka benki Kuu (BoT).

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete
hakutaja majina na watuhumiwa, kiasi walichodaiwa kuiba, kiasi
walichorejesha na kiasi hicho kiko wapi.

Ahadi yake ya kutowashitaki iwapo watarejesha fedha, ni mtaji
mkubwa. Watuhumiwa hao ambao tayari wamethibitika kuwa mafisadi kwa
kuwa wamekiri, wanatarajia kuchanga kiasi gani kwa njia ya
shukrani?

Nne, kuna wananchi mitaani ambao, katika vibanda vyao vya matembe,
ajira zao zisizosalama, uchuuzi wao unaopigwa vita kila siku na
matarajio ya kuvaa kijani kila uchaguzi, watachanga Sh. 300 au 500.
Huwezi kubishana na hawa. Ndio waendelezaji wa kauli za kuwa “damu
-damu” na CCM. Wakati mwingine husema wana damu ya kijani. Nao
watachanga.

Chama Cha Mapinduzi kinataka kitu kutoka kwa kila mtu; ili kipate
fedha na hivyo kupata viongozi kwa hila na jeuri ya fedha.
Na siyo kweli kwamba CCM itapata Sh. 40 bilioni tu. Kwa mkakati
wake huu, itapata mabilioni mengi zaidi; labda mara mbili au mara
tatu ya kiwango kinachotajwa hadharani.

Tutasikia kelele kwamba kitu muhimu ni kuripoti umepata kiasi gani
cha fedha na umezitumiaje katika uchaguzi. Hizi ni kauli za
“danganya toto.”

Kwa ubabe wa CCM na serikali yake; ule wa kukataa kutaja mafisadi
waliothibitika; kukataa kusema waliiba kiasi gani na wamerudisha
kiasi gani; na hatimaye kukaidi kuwapeleka mahakamani; nani
atawalazimisha kutamka wamekusanya kiasi gani kwa mfumo wao
wenyewe?

Kwa ukaidi na ubabe wa CCM na serikali yake; ule wa kuweka viongozi
wa siasa katika sheria ya matumizi ya fedha wakilenga kudhibiti
upinzani ndani na nje ya chama chao; nani atalazimisha chama na
serikali yake kuwa waadilifu?

Katikati ya ahadi na mbinu za kukusanya mabilioni ya shilingi, ziko
wapi mbwembwe za rais wakati wa kutia saini sheria ya kuzuia
matumizi mabaya ya fedha katika uchaguzi?

Uko wapi utukufu wa waliomsindikiza rais kusaini sheria ya kuzuia
matumizi ya fedha haramu katika uchaguzi? Kwa maandalizi haya, CCM
na serikali yake “hawajafuta” sheria aliyosaini rais?

Sheria yenyewe ina matundu. Hakuna kipengele chochote katika sheria
hii ambacho kinazuia mafisadi kuchangia chama.

Hatujaona, katika kanuni zinazojadiliwa, kipengele chochote
kinachowazuia mafisadi kuingiza fedha katika kampeni za vyama vya
siasa.

Kama vifungu hivi havimo na kama ukusanyaji fedha uko chini ya
chama chenyewe ambako uwazi ni hadhithi za alinacha, basi mafisadi
waliosetiriwa na kunusurishwa mahakama, wamepata fursa ya kutoa
asante.

Tayari ubabe wa CCM na serikali yake umeanza kudhihirika. Kwa
mfano, wadau walipendekeza na kukubaliana kuwa kiwango cha juu cha
fedha kwa mgombea ubunge kwa upande wa Zanzibar, kiwe Sh. 10
milioni.

Lakini CCM imepenyeza pendekezo ambalo tayari linaonekana
kukubaliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kwamba
mgombea ubunge Zanzibar atumie Sh. 40 milioni.

Uamuzi wa Tendwa na CCM yake, haukujali ukubwa wa majimbo ya
Zanzibar kama sheria inavyoagiza; wala idadi ya wapiga kura.
Majimbo mengi ya Zanzibar ni madogo; yenye wapigakura wachache;
pengine chini ya 10,000 na kijiografia ni madogo.

Mahali pengine, viwango vilivyopenyezwa na CCM na kukubaliwa na
Tendwa kwa majimbo ya Zanzibar, ni vikubwa kuliko vile vya Bara.
Kwa staili hii, hata Tendwa mwenyewe amepoteza sifa ya uadilifu na
ile ya kuwa msajili wa vyama vya siasa kwa sababu ya kukumbatia
matakwa ya chama kimoja dhidi ya vingine.

Na hii, inaufanya mchakato mzima wa kutunga sheria hadi kuisaini
kuonekana hauna maana na hauzingatii maslahi ya taifa.

Watanzania wengi wataendelea kujiuliza, kama Kikwete ana uwezo wa
kuchangisha mabilioni yote hayo kwa uchaguzi wa kumwongezea miaka
mitano ikulu, anashindwa nini kuchangisha mabilioni ya kuleta
maisha bora aliyoahidi.

Itakuwa vigumu kutetea Kikwete kwamba fedha anazokusanya
hazitatumika kununua kura.

Hii ni makala ya maoni binafsi katika Mwanahalisi toleo la sasa.
 
Cha kutisha ni kwamba tunaye tena for the next 5 yrs!!!!! I need to vomit!
 
Ndo maana mafisadi wanafanikiwa kumchomekea mavitu yao na kukupua mabilioni ya WaTz. Dump the man! This year!
 
Hii ndio asili ya viongozi tulio nao! Hubuni mbinu na mikakati ya kubaki madarakani na sio kumtumikia mtanzania aliyewachagua! Huwezi amini nchi hii bado kuna shule za msingi na secondary ambapo wanafunzi hukaa chini na kuandikia kwenye miguu yao! Wakuu hawa hawaju kwamba mishahara wanayomplipa mfanyakazi ni aibu na ni fedheha kubwa. Kwa miaka mitano hakuna anayewajali wala kufikiri ni nini nanma ya kuwasaidia

Lakini linapokuja suala la kubaki madarakani, hujifanya kuwageukia hao hao wananchi waliochoka na kuendelea kuwakamua just for their own gratification sake.Je Ubunifu kama huu usingeonekana wa manufaaa zaidi kama wananchi tungechangishwa kwa hiari zetu mathalani kwa ajili ya ujenzi wa hospital teule kwa ajili ya magongwa ya akina mama, magojwa ya moyo na kadhalika? Bil 40 yaweza kununua madawati mangapi na kulifanya suala la watoto wetu kukaa chini kuwa historia?
Five yrs for Christ's sake leo ndio unakumbuka unahitaji kufanya marekebisho ya sheria ya madini! This is hypocrisy of an immesuarable scale!
 
Are you really surprised?

This guy has no vision for the country. Our leaders has no vision for this country, (except 1 or 2). Few days after the law was signed he went back to initiate 40-50 billions fund raising. To me, that does not add up at all.

I am sure he can read but not comprehend.
 
Yaani Tanzani wakati mwingine inafanana na ngalawa baharini isiyo na mpiga makasia. Yaani inajiendea tu na Mungu anailinda.
 
well,its not like im trying to be funny,lakini atasoma saa ngapi na muda wote yuko safarini?
 
Yaani Tanzani wakati mwingine inafanana na ngalawa baharini isiyo na mpiga makasia. Yaani inajiendea tu na Mungu anailinda.
Tanzania ina watu wa vichwa sana kama akina Dr Slaa. Lakini nadhani katiba yetu ina shida saaaaaaaana kiasi kwamba hata kiongozi mzuri anaweza kuwa kama Kikwete alivyo.
Ni ajabu kwamba Marmo pamoja na kuchezea sheria zetu hatachukuliwa hatua si na bunge tu, bali hata boss wake na wananchi wa kwao huko Manyara sijui hawatajali kumuadhibu. Shame upon Marmo.
Tunahitaji katiba mpya Tanzania iliyotungwa si kwa haraka, wala kwa maslahi ya mtu au chama chake, bali kwa taratibu na ikishirikisha watanzania wote. Hatutaki wanasiasa kuchezea nchi yetu. Nina hakika hawataishi miaka mingi kuanzia sasa lakini the country will be there for ever. Kwa nini tuachie wana wetu na wana wao matatizo ya kuja kukatana mapanga bila sababu ya msingi? Wasidhani wa kwao watapona!
 
jk ni kipimo kizuri kwa watanzania kama je, ni timamu?

kurudi kwake ikulu kunategemea idadi ya wapumbavu

nchini, samahani situkani!!!!
 
Imagine the possibilty of tanzania without a president!
IF the kind of leaders we choose are of this kind, then
lets try a life without one? is it possible?

One can not compare Dr SLaa and Kikwete they are two
different people with different background, this is not to say
slaa does not have his own faults? Politics of complaining
if he is given power what will he complain about?

Am serious questioning the possibility of TZ without president,
IF Costa Ricca can survive without an army- as they have proved to
so far- then Tanzania can survive with no president.
 
yaani unategeme JK akae na kusoma vitu hivi atapata muda saa ngapi...maana kutwa yuko bize anajibu message kwenye simu yake ya mkononi sasa hapo kuna rais au matapishi
 
Muungwana hana muda wa kusoma ishu nyeti, yeye ni sms na mengineyo ya hovyohovyo...
 
GOD forbid ..aliyewaambia jk anasomaga chochote zaidi ya sms,.....nani??? hata magazeti anaangalia vichwa vya habari tu..muda wa kusoma miswada yenye lugha za kisheria zisizovutia ataupata wapi...sembuse hata kusoma summary za mswada husika anazoandaliwa na washauri wake wa kisekta ikulu?...au hata kupata muda wa kuwasikiiliza washauri kwa makini na kuwapa maswali ya kiuchunguzi kabla ya kusaini chochote??

Mungu bariki tu huko nje anakoenda anaweza akachomekewa kipengele cha kutuuza utumwani ndani ya nchi yetu na asikione!!!

mtu asiyependa kujisomea hafai kabisa...atabaki kutuongoza kwa ramli siku zote....just imagine na zile mbwembwe zote za kusaini ile sheria .,kumbe alikuwa hajaisoma..haijapata kutokea Tanzania..

NAPENDEKEZA PANEL YA MAJAJI IPITIE UPYA SHERIA ZOTE NA MIKATABA ALIYOSAINI KIKWETE ILI IRIDHIWE UPYA ...HILI NI MUHIMU HATA KWA WANASHERIA HUMU JITOLEENI KULIFANYA!!
 
Back
Top Bottom