JK aponzwa na Msimamo tete wa Tanzania kuhusu LIBYA Wiki Leaks yatumika Kumfunga Mdomo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK aponzwa na Msimamo tete wa Tanzania kuhusu LIBYA Wiki Leaks yatumika Kumfunga Mdomo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GHOST RYDER, Sep 6, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  JK aponzwa na Msimamo tete wa Tanzania kuhusu LIBYA Wiki Leaks yatumika Kumfunga Mdomo

  Tuhuma ambazo zinasambazwa kwa sasa na Mtandao wa Wiki leaks ni juhudi za wazi za idara ya ujasusi ya Marekani kuhakikisha kuwa inamfunga mdomo jumla JK ambaye katika siku za karibuni serikali yake imekuwa na msimamo usioegemea upande wowote katika kadhia ya NATO na serikali inayoondoshwa madarakani ya Muamar Gaddafi.

  Sikubaliani na Udhaifu wa Serikali ya JK katika masuala mengi ya msingi ambayo watendaji wake wanamunagusha kwa kiwango kikubwa na yeye kushindwa kuthubutu kutoa maamuzi mazito, lakini kwa hili la WIKI Leaks nashawishika kusimama upande wa pili wa mstari na kusema enough of these none sense from western world.

  Haiwezekani tuhuma hizo mmezikalia muda wote huo na leo ndo mnakuja kuzitoa kama lengo ilikuwa kuonyesha madhaifu haya, yalikuwa msaada mzuri kwa watanzania hapo Oktoba 2010 wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba tunakwenda kuchagua kiongozi ambaye si safi, na si leo huu ni unafiki na kutaka kutuchanganya watanzania.

  Binafsi huu ni upuuzi na nadhani Acheni Afrika ifanye mambo yake yenyewe na Viongozi waendeshe serikali zao kwa uhuru na Demokrasia. Mkisimamia mawazo ya kuongeza transparency, Accountability na Democracy nitawaelewa.

  Kuna UN Democracy charter ambayo ni suluhisho la siasa mbovu za Tanzania, hili ndilo ambalo lingesikika leo mkilipigia kelele tuiridhie charter hii ambayo Tanzania mpaka sasa wanajiuliza waridhie ama la maana itawapa safari ya mapema kuachia madaraka na si design ya suti na rushwa za kuibua muda huu.

  Hili linafanyika ili kuficha wizi wa mafuta unaofanywa na kampuni za BP, SHELL na miamba wengine huko LIBYA…Mwizi anampigia kelele mwizi mwenzie kwa kuwa yeye ana mbwa nayeweza kubweka kwa sauti kubwa zaidi.

  HAPANA,Sidanganyiki kwa hili.

  ADIOS
   
 2. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,074
  Likes Received: 7,564
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri to speak out your mind, as inaweza leta changamoto na kuibua mengi, pia sijapata bado muda wa kuifuatilia kiundani taarifa ya Wikiliks kuhusiana na suala hili, kwasababu sasa hivi nimejikita zaidi katika zile taarifa za mahojiano na wafungwa wa Guantanamo kuhusiana na AL-queda. Kuhusu suala hili na namna ulivyoliwasilisha labda niulize swali moja....Je walipoibua kuhusu mahojiano ya Dr. Hosea na yule ofisa wa ubalozi walikuwa wanajaribu kumfunga mdomo juu ya nini?
   
 3. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama kweli JK anaweza kupelekwa shopping na tajiri wa Kempiski tuu, Marekani ingeshindwa kumfunga mdomo kweli? Mbona hata weaklieaks ni adui wa marekani? Tukubali tuu kwamba raisi wetu is too cheap wala Marekani wasingepata shida ya kumfanya asupport operation ya Libya.
   
 4. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Mtoa mada unataka kutuaminisha hapa kuwa US inataka kuua mende kwa Roketi?
   
 5. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Nadhani kama nia yako ni kuwafikishia ujumbe Wamarekani ungewaandikia kwa Kiingereza halafu si kupitia JF sababu inawezekana wasione madai yako. La pili ni kama una ushahidi kuwa wao ndiyo waliorusha hiyo cable mtandaoni. WikiLeaks ipo mtandaoni na mtu yeyote anaweza kuitembelea akasoma, isitoshe imewakwaza sana Wamarekani baada ya siri za mawasiliano yao kuvuja, sasa iweje waitumie dhidi ya serikali ya hovyo kama ya Vasco?
  Kama wana nia ya kuifunza adabu serikali hii kuna njia nyingi na zenye madhara kwa mustakabali wa nchi lakini haiingii akilini kwamba masuala ya suti za kuhongwa ndiyo bakora wanayoitumia kuhusu msimamo wa TZ juu ya Libya.
   
 6. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,414
  Likes Received: 1,974
  Trophy Points: 280
  kuhusu watendaji kwamba ndio wanaomuangasha ulitegemea nini kwenye serikali ya uswaiba? kumbuka maneno ya lowassa hakukutana na mkuu barabarani wengi aliowaweka madarakani hakukutana barabarani kwa kifupi kajiangusha mwenyewe.
   
 7. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi katika kauli ambazo zinznitia kichefuchefu nikizisikia ni hizi, ACHENI AFRIKA IFANYE MAMBO YAKE YENYEWE.
  Vikao vya AU vikikaa ajenda yao kubwa ni hiyo tu, kuteteana na kulindana basi,

  Mambo ya msingi kama mabaa ya njaa hawayazungumzi, tumeona hapa Somalia, Taarifa zimetolewa na WFP na mashirika mengine ya EU, cha kushangaza kikao cha mwisho cha AU hakikuongelea balaa la njaa linaloikabili Somalia wala bahadhi ya nchi za Afrika, wao wakawa wanamtetea mwenzao kanali Gadhafi, na kuishutumu NATO.

  Jukumu la njaa na matatizo ya waafrika wanawaachia wazungu, haohao wanaowaambia matatizo ya waafrika waachie waafrika wenyewe.
  Gadhafi akiua raia wake kwa kisingizio cha waasi, "jumuhia ya Ulaya msiingiliwe".
  Raia wakikosa chakula wanakufa kwa njaa, "jumuhia ya Ulaya tunaomba mtusaidie"

  Hawa ndio viongozi wetu wa kiafrika.
   
 8. m

  mbasamwoga Member

  #8
  Sep 6, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Libya ni vita ya wakubwa........ Tanzania haiwezi kufukirika kaka abdul.
   
 9. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,074
  Likes Received: 7,564
  Trophy Points: 280
  Iwe kwa kiingereza au Kiswahili au lugha nyingine yoyote ile wamarekani ujumbe huupata na kuulewa, hawafanani na sisi ambao usipooongea kiingereza thamani yako hupungua na kukufanya uonekani ni mtu duni kitaaluma na kiufahamu.....
  Kuhusu angepitia wapi au media ipi kuleza malalamiko yake na kusema JF si mahala sahihi, hapo utakuwa umepotoka mkuu, nguvu ya JF ni kubwa na hufuatiliwa na watu ambao ni makini na wenye influence kubwa kuliko ile ya msitu kuvuta mvua, nimejaribu tu kukuelewesha kwakuwa naamini huifahamu JF, endelea kuwepo, soon or later you will feel the heat and come to know what JF is capable of...
   
Loading...