JK apewa tuzo leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK apewa tuzo leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Narubongo, Jan 30, 2012.

 1. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  jk amepewa tuzo huko Addis ababa na maraisi wa afrika, ni tuzo ya kupambana na ugonjwa hatari wa malaria barani afrika, hii ni mara ya pili kwa tz kuipata award hii inayoheshimika sana duniani

  SOURCE: TBC taarifa ya habari saa 2
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kumbe mambo ya afya yako vyema! JK anapewa tuzo juu ya mambo ya afya huku madaktari wanagoma!
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  mjinga siku zote hucheka mara mbili
   
 4. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Source ni TBC
   
 5. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hiyo Tuzo inawasaidia nini wananchi waliofiwa na ndugu zao kwa mgomo wa madaktari? Au ndiyo sifa za kijinga.......Hizi tuzo na Dr. wa heshima nao unalemaza viongozi wetu
   
 6. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Tuzo ya afya?????? Mbona dhihaka! JK anathubutuje kupokea tuzo hiyo wakati watu wake wanakufa kutokana na mgomo wa madaktari? Sasa nalazimika kuamini kuwa JK hana dhamira ...
   
 7. M

  Muggssy Member

  #7
  Jan 30, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe unaemtetea Lowasa umetumwa na nanani? huwezi kumsafisha mtu kwa maji taka maana atazidi kuchafuka tuu maana kitendo chechote cha kumsafisha Lowas kinazidi kumchafua tu bora ukae kimya
   
 8. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Naona ni kwa himiza watu waweke vibandiko vya malaria haikubaliki milangoni!
   
 9. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,141
  Likes Received: 3,330
  Trophy Points: 280
  Tuzo ya kusafiri hovyo.
   
 10. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Mh!

  Hivi Malaria imetoweka TZ? Labda kama anapokea kutokana na mafanikio kule Zanzibar.

  Kama sivyo,sioni lolote kwa upande wa Tanganyika lilomfanya jamaa apewe hiyo tuzo!

  Viongozi wetu wa Afrika wako kama wenye akili sawa! Ndio AU imedorora kuliko maelezo.
   
 11. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #11
  Jan 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  basi akirudi ataitolea hotuba,kana mnakumbuka hotuba yake wakati wa sakata la sukari na uchaguzi igunga..badala ya kuzungumzia sukari na hali ya uchumi, Penguin akawa bize kuelezea uraia wa nchi mbili na zawadi alizohongwa...NILIWAHI KULA NAE LUNCH SOMEWHERE YANI HUYU BABA MAWAZO YAKE KAMA MGOMBEA UDIWANI WA TLP HUKOO NKENGE
   
 12. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kapewa tuzo kwa lile deal la SUGU na Clouds nini? Yale matangazo ya malaria haikubaliki! wanapongezana vipofu wote hawana lolote! Kila mmoja nyumbani kwake full matatizo wamekalia propaganda za media tu.

  Huenda ikawa hata hii tuzo imechongwa haraka haraka haraka na hao jamaa zake ili kujaribu kumpigia propaganda za kutupumbaza kwenye huu mgomo!

  Kwa hiyo tuamini malaria imeisha Tz' thubutu nenda mwananyamara ukashuhudia Wagonjwa wenye drip za quinin walivyojaa!
   
 13. a

  alles JF-Expert Member

  #13
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Jan 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wanampa kichwa ili azidi kuangamiza Watanyania kwa NGAO
   
 15. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #15
  Jan 30, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Napita nawahi mgonjwa hospitalini.
   
 16. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #16
  Jan 30, 2012
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Mbona unahangaika sana na madaktari. Kugoma ni haki yao ya msingi ikliwa serikali hii haijali wataalamu wa afya badala yake inajali kada zingine. Kama wanaweza kumlipa mfanyakazi wa serikali aliye na elimu wastani na bila ugumu wowote wa kazi, ofisi kiyoyozi, nyumba hekalu, gari v8, mshahara milioni 29 kwa mwezi na kisha akaibia tena serikali, akatoroka na kuudanganya umma kuwa amekufa, wewe unaona madakatari kugoma sekta ya afya iboreshwe ni nongwa e ee? Ngoja yakufike au ni kwa kuwa hawa wenye maamuzi wanakimbilia India?

  India wanaenda kwa maelfu ya dola, ili hali wangeweza kuboresha kwao na kuponesha fedha za kigeni. Matokeo yake sekta inadumaa. Ni ushenzi sana bora wagome wote hadi shangazi zao vijijini wawapeleke India. Kudadeki. Tumechoka wananchi pia.
   
 17. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #17
  Jan 30, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mwenye akili na atafakari, Huku nyumbani hali ya Huduma za afya ni tete kwa zaidi ya Wiki, ikimaanisha hali ya huduma za afya ni mbove At the mean Time, As usual Mzee wa kutabasamu anapewa tuzo bila shaka huku akikenua kama kawaida yake, hii ni dhihaka kwake kwa kuwa nina uhakika Jk kwa sasa ndio Rais kilaza na Mwenyeuwezo mdogo wa uelewa kuliko wote, acha wampe, wasisahau kumpa na udokta pia
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  Jan 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama kuna mtu anastaili hii tuzo ya Malaria basi ni George W. Bush maana ni chini ya uongozi wake mpango mzima wa kupambana na malaria ulisukwa. Pia ni kipindi hicho hicho marekani waliamua kukaza uzi wa kusaka Uranium yetu, hivyo malaria haikubaliki na zile neti za mbu ni kama umangungo fulani.

  Hiii sio tuzo ya kwanza kwa Tanzania kwenye haya mambo ya afya kipindi hiki cha awamu ya nne. Lakini ukitizama kwa makini utaona karibu kila programme ambayo tunapata tuzo kuna involvement fulani ya marekani. Hivyo ni vigumu sana kukubali kweli Tanzania imepiga hatua kuliko nchi zote barani Afrika katika kupambana na Malaria. Binafsi sijui serikalii ya awamu ya nne imefanya nini hasa cha ziada katika kupambana na malaria! wametenga fedha zaidi? wametekeza masalio ya mbu?
   
 19. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #19
  Jan 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Uozo mtupu!

  Serikali legelege na uozo wake!
   
 20. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #20
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  TBC wanamkejili JK au? Au usikute hata waliompa tuzo wanamkejeli.
   
Loading...