JK aonja nguvu ya CHADEMA Mwanza

JK aonja nguvu ya CHADEMA Mwanza

NDEO

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2011
Posts
813
Reaction score
189
AIS Jakaya Kikwete jana alipata wakati mgumu, baada ya kukutana na nguvu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Mwanza katika ziara yake, huku Waziri wake wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, naye akijikuta akizomewa mbele yake.

Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, alivunja mwiko baada ya kujiunga katika msafara huo wa raia akiwa na gari lenye alama za Movement for Change (M4C) lililokuwa limefungwa bendera mbili za CHADEMA.
Hata hivyo maofisa usalama walipata wakati mgumu kulizuia gari hilo lisiwepo katika msafara huo, jambo lililozua tafrani kidogo katika uwanja wa Furahisha ambapo Kikwete alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara.
Awali wakati wa uzinduzi wa wodi ya wazazi iliyoko eneo la Butimba, Rais alilazimika kumpa Wenje nafasi ya kuwasalimia wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo, kutaka kufanya hila ya kumnyima haki hiyo kama mbunge wa jimbo husika.

Baada ya viongozi wote kutambulishwa bila Wenje kutajwa, wananchi walianza kupaza sauti wakitaka mbunge wao naye atambulishwe.

Wenje baada ya kusimama alimshukuru Rais Kikwete kwa kumpa nafasi hiyo lakini akamwomba amvumilie kidogo atoe salamu maalumu ya wana Mwanza.

Kama kawaida ya CHADEMA kwenye salamu yao, Wenje aliwaomba wananchi wakunje ngumi kisha akawasalimu kwa kibwagizo cha peoples… nao wakamwitikia power!

Akiwa katika viwanja vya Furahisha ambapo Rais Kikwete alichelewa kuanza mkutano wake, Wenje alifika hapo na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi huku polisi wakiwazuia bila mafanikio.

Ilipofika saa 12 jioni kabla Rais hajaingia uwanjani, wananchi hao walimtaka Wenje awahutubie huku wakidai bendera ya taifa ishushwe kwani muda wake ulikuwa umefika.

Kikwete aliingia uwanjani hapo saa 12:10 akiongozana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali lakini wananchi hawakuonyesha kumshangilia badala yake walikuwa wakimwonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA wakiimba ‘peoples…power’.

Katika hatua ya kushangaza wananchi hao walimshangilia kwa nguvu mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, aliyekuwa ameongozana na Rais huku wakiwazomea Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata, ambaye hakufika kabisa mkutanoni hapo.

Matata alionekana mapema wakati Rais Kikwete akisomewa taarifa ya maendeleo makao makuu ya wilaya hiyo lakini hakufika uwanjani kabisa katika viti vya mbele alionekana naibu wake, Swila Dede.

Baadhi ya wananchi hao walisikika wakisema chini kwa chini kuwa Matata ni mwizi hawataki kumsikia lakini shangwe na nderemo zikajiri pale walipotambulishwa Wenje na Kiwia.

Rais Kikwete akiwa wilaya ya Ilemela, wananchi wengi waliokuwa wamesimama njiani walimwonyesha vidole viwili ikiwa ni alama CHADEMA.

Hata hivyo, hali hiyo ilionekana kumkera kiongozi huyo wa nchi pamoja na maofisa wa usalama, ambapo wana usalama wakiwemo polisi walionekana wakiwatisha na kuwazuia wananchi kunyoosha vidole viwili.

Magufuli azomewa
Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli, alikumbana na jinamizi la kuzomewa mbele ya Rais baada ya kusimama jukwaani na kutaja jina la Matata, ambapo wananchi wengi walimzomea kwa miluzi huku wakimnyooshea vidole viwili.

Adha Magufuli alizomewa pia aliposema wabunge wa Ilemela na Nyamagana jijini hapa ni wana CHADEMA lakini ndani ya roho zao ni wana CCM.

Pia aliendelea kuzomewa aliposema kuwa iwapo Rais angehitaji kupokea kadi za CHADEMA zilizorudishwa angepokea nyingi.

“Mheshimiwa Rais, nampongeza Meya Matata (akazomewa), lakini pia wabunge wa Ilemela na Nyamagana wanachapa kazi vizuri, nje CHADEMA lakini ndani wao CCM (akazomewa).”

Akizungumza katika mkutano huo, Rais Kikwete alimpongeza mbunge wa Nyamagana kwa uchapakazi mzuri hasa kusimamia sekta ya elimu na kwamba wabunge wa namna hiyo wanastahili kuigwa.

Hata hivyo, alisema serikali yake imejipanga vizuri kuhakikisha usafiri wa reli, ndege, majini na barabara za lami vinaboreshwa maradufu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
“Serikali yangu imeweka nguvu kubwa katika kuboresha sekta ya uchukuzi, ujenzi na nyinginezo. Hii ni kutaka kuwaletea wananchi wetu maendeleo ya kisekta,” alisema.

Baadhi ya mawaziri walioongozana na Rais mbali na Magufuli ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, Naibu Waziri wa Ujenzi na Dk. Charles Tizeba.
 
AIS Jakaya Kikwete jana alipata wakati mgumu, baada ya kukutana na nguvu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Mwanza katika ziara yake, huku Waziri wake wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, naye akijikuta akizomewa mbele yake.

Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, alivunja mwiko baada ya kujiunga katika msafara huo wa raia akiwa na gari lenye alama za Movement for Change (M4C) lililokuwa limefungwa bendera mbili za CHADEMA.
Hata hivyo maofisa usalama walipata wakati mgumu kulizuia gari hilo lisiwepo katika msafara huo, jambo lililozua tafrani kidogo katika uwanja wa Furahisha ambapo Kikwete alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara.
Awali wakati wa uzinduzi wa wodi ya wazazi iliyoko eneo la Butimba, Rais alilazimika kumpa Wenje nafasi ya kuwasalimia wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo, kutaka kufanya hila ya kumnyima haki hiyo kama mbunge wa jimbo husika.

Baada ya viongozi wote kutambulishwa bila Wenje kutajwa, wananchi walianza kupaza sauti wakitaka mbunge wao naye atambulishwe.

Wenje baada ya kusimama alimshukuru Rais Kikwete kwa kumpa nafasi hiyo lakini akamwomba amvumilie kidogo atoe salamu maalumu ya wana Mwanza.

Kama kawaida ya CHADEMA kwenye salamu yao, Wenje aliwaomba wananchi wakunje ngumi kisha akawasalimu kwa kibwagizo cha peoples… nao wakamwitikia power!

Akiwa katika viwanja vya Furahisha ambapo Rais Kikwete alichelewa kuanza mkutano wake, Wenje alifika hapo na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi huku polisi wakiwazuia bila mafanikio.

Ilipofika saa 12 jioni kabla Rais hajaingia uwanjani, wananchi hao walimtaka Wenje awahutubie huku wakidai bendera ya taifa ishushwe kwani muda wake ulikuwa umefika.

Kikwete aliingia uwanjani hapo saa 12:10 akiongozana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali lakini wananchi hawakuonyesha kumshangilia badala yake walikuwa wakimwonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA wakiimba ‘peoples…power'.

Katika hatua ya kushangaza wananchi hao walimshangilia kwa nguvu mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, aliyekuwa ameongozana na Rais huku wakiwazomea Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata, ambaye hakufika kabisa mkutanoni hapo.

Matata alionekana mapema wakati Rais Kikwete akisomewa taarifa ya maendeleo makao makuu ya wilaya hiyo lakini hakufika uwanjani kabisa katika viti vya mbele alionekana naibu wake, Swila Dede.

Baadhi ya wananchi hao walisikika wakisema chini kwa chini kuwa Matata ni mwizi hawataki kumsikia lakini shangwe na nderemo zikajiri pale walipotambulishwa Wenje na Kiwia.

Rais Kikwete akiwa wilaya ya Ilemela, wananchi wengi waliokuwa wamesimama njiani walimwonyesha vidole viwili ikiwa ni alama CHADEMA.

Hata hivyo, hali hiyo ilionekana kumkera kiongozi huyo wa nchi pamoja na maofisa wa usalama, ambapo wana usalama wakiwemo polisi walionekana wakiwatisha na kuwazuia wananchi kunyoosha vidole viwili.

Magufuli azomewa
Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli, alikumbana na jinamizi la kuzomewa mbele ya Rais baada ya kusimama jukwaani na kutaja jina la Matata, ambapo wananchi wengi walimzomea kwa miluzi huku wakimnyooshea vidole viwili.

Adha Magufuli alizomewa pia aliposema wabunge wa Ilemela na Nyamagana jijini hapa ni wana CHADEMA lakini ndani ya roho zao ni wana CCM.

Pia aliendelea kuzomewa aliposema kuwa iwapo Rais angehitaji kupokea kadi za CHADEMA zilizorudishwa angepokea nyingi.

"Mheshimiwa Rais, nampongeza Meya Matata (akazomewa), lakini pia wabunge wa Ilemela na Nyamagana wanachapa kazi vizuri, nje CHADEMA lakini ndani wao CCM (akazomewa)."

Akizungumza katika mkutano huo, Rais Kikwete alimpongeza mbunge wa Nyamagana kwa uchapakazi mzuri hasa kusimamia sekta ya elimu na kwamba wabunge wa namna hiyo wanastahili kuigwa.

Hata hivyo, alisema serikali yake imejipanga vizuri kuhakikisha usafiri wa reli, ndege, majini na barabara za lami vinaboreshwa maradufu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
"Serikali yangu imeweka nguvu kubwa katika kuboresha sekta ya uchukuzi, ujenzi na nyinginezo. Hii ni kutaka kuwaletea wananchi wetu maendeleo ya kisekta," alisema.

Baadhi ya mawaziri walioongozana na Rais mbali na Magufuli ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, Naibu Waziri wa Ujenzi na Dk. Charles Tizeba.
Taifa linawatu wajinga sana kwani kupanga kufanya vurugu kwenye mikutano ya rais inawapa faida gani huu uongo na vurugu mnazofanya zinawasaidia nini?

jaribuni kufanya siasa za hoja siasa za hoja zimepitwa na wakati ni ushamba watu wazima mnapanga kufanya vurugu halafu bila aibu mnajisifia kweli ujinga hauna majani wewe ungekuwa umeshaota majani.
 
Kwa vile nyie mipango yenu ni kutafuta sifa rais akija tena jitahidini mkojoe jukwaani labda mtapa sifa make haya matendo mengine mnafanya baada ya kupata sifa mnapata aibu tu,

Bungeni wabunge wenu wamepigana hamjapata sifa mmepata aibu,mmefanya fujo kwenye mkutano wa jk napo hamjapata sifa kwa hiyo kikubwa sasa jk akija kojoeni jukwaa kuu labda mtapata sifa.
 
hahaha uncle deo cyo kutafta sifa ila ni kumpatia ujumbe kijeba wako kuwa wana mwanza hawataki upuuzi wa kikwekwe wako huyo
 
mkuu hata mie naamini magufuli ni jembe ila nikukanushe kuhusu urais coz haiba ya magufuli ni ya kiutendaji na cyo urais pia hata wana mwanza wanampenda ila kilichofanya azomewe ni vile alivojikanyaga kwa kuwataja matata na kauli ya kuwa wenje ana uccm moyon.
 
Taifa linawatu wajinga sana kwani kupanga kufanya vurugu kwenye mikutano ya rais inawapa faida gani huu uongo na vurugu mnazofanya zinawasaidia nini?

jaribuni kufanya siasa za hoja siasa za hoja zimepitwa na wakati ni ushamba watu wazima mnapanga kufanya vurugu halafu bila aibu mnajisifia kweli ujinga hauna majani wewe ungekuwa umeshaota majani.

utakufa kwa kuhoro kutetea mavi(ccm) inahitaji roho kama ya paka..
 
Kwa vile nyie mipango yenu ni kutafuta sifa rais akija tena jitahidini mkojoe jukwaani labda mtapa sifa make haya matendo mengine mnafanya baada ya kupata sifa mnapata aibu tu,

Bungeni wabunge wenu wamepigana hamjapata sifa mmepata aibu,mmefanya fujo kwenye mkutano wa jk napo hamjapata sifa kwa hiyo kikubwa sasa jk akija kojoeni jukwaa kuu labda mtapata sifa.

inaelekea wewe nu mtoto wa juzi hujui hata kilicho mtokea dr mganga akipokuwa kwenye kampeni za urais 2005..
 
Taifa linawatu wajinga sana kwani kupanga kufanya vurugu kwenye mikutano ya rais inawapa faida gani huu uongo na vurugu mnazofanya zinawasaidia nini?

jaribuni kufanya siasa za hoja siasa za hoja zimepitwa na wakati ni ushamba watu wazima mnapanga kufanya vurugu halafu bila aibu mnajisifia kweli ujinga hauna majani wewe ungekuwa umeshaota majani.
Hiv Wananchi kumshangilia Mbunge wao ni vurugu.....Naona umeghafilika mkuu....Kama inakuuma kunywa sumu ufilie mbali hukoooo......
 
Angalizo kwa Wasomaji wa Uzi huu:

Mleta Uzi ni Mwandishi Mwandamizi wa "Kishiri Times" lenye Ofisi yake katika Kitongoji cha Mashigambiti, Kijiji cha Kishiri, Kata ya Igoma, Wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza.

Hivyo, hata uzi ameuleta kwenu kwa staili ya kishiri-kishiri na ndio maana ameanza heading ya Uzi na neno "Tetesi" na kujaza ----- kwenye uzi wenyewe!

Kwa wale ambao hawafahamu namna ya kufika Kishiri, ziliko ofisi za Kishiri Times, gazeti ambalo Mleta Uzi uliojaa ----- ni Mwandishi Mwandamizi, baadaye kidogo mtapata maelekezo. Poleni!
 
ukishiri wa mleta uzi hautuhusu, wewe kanusha kama habari alizoleta ni za uongo!!!!!
kinyume chake wewe ndio unataka kuleta porojo.

dhis taimu neki ya magamba ikikutana wataanza kuagana, manake mwenyekiti hatadanganywa tena, kajionea mwenyewe dhoruba ya nugwi, kupona ni majaaliwa!!!!!
 
Deo wewe gamba,hizo ndio changes za politics mambo taratibu but mageuzi yako karibu.maana wananchi wamechoka na propaganda zenu magamba.
 
Back
Top Bottom