JK amtaabisha Nape

JK amtaabisha Nape

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,483
  • Yaliyomkuta kwa magamba yajirudia kwa mawaziri mizigo



KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amepoteza uhalali wake wa kuendelea kushika wadhifa huo, kutokana na utendaji wake kukinzana na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Hali hiyo inatokana na taswira inayozidi kujitokeza kati ya wawili hao katika kusimamia masuala mazito yaliyoasisiwa na chama hicho.

Kwa nyakati tofauti, umejitokeza msigano ambapo wakati Nape akizunguka kwa wananchi mikoani kunadi msimamo wa CCM kuhusu jambo fulani, Rais Kikwete baadaye anajitokeza na kutoa mtazamo tofauti.

Hatua hii imeibua mkanganyiko kwa wananchi, na hivyo baadhi kufikia hatua ya kushauri Nape aachie ngazi ili kuonyesha kuwa amesalitiwa badala ya kuendelea kuonekana adui kwa wale anaosimamia wang'olewe.

Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Bukoba, Dk. Azavery Lwaitama, alizungumzia hali hiyo akisema inaonyesha kuwa hakuna mawasiliano kati ya Rais Kikwete na sekretarieti yake ya chama.

Alisema kuwa kama kungekuwa na mawasiliano ya kutosha, rais asingewateua tena baadhi ya mawaziri waliodaiwa na chama chake kuwa mizigo kuendelea kushika madaraka.

Mwishoni mwa mwaka jana, wakiwa katika ziara za kuimarisha chama mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Nape mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, aliwataja baadhi ya mawaziri akiwaita mizigo kutokana na kushindwa kuwajibika ipasavyo.

Katika mikutano yao tofauti ya hadhara, Nape alikwenda mbali zaidi akisema mawaziri hao lazima waitwe mbele ya Kamati Kuu ya chama kujieleza na kuchukuliwa hatua.

Mawaziri waliotajwa ni Christopher Chiza (Kilimo na Chakula) na Naibu wake, Adam Malima, Dk. Shukuru Kawambwa (Elimu na Mafunzo ya Ufundi) na Prof. Jumanne Mghembe (Maji)
Lakini kama hiyo haitoshi, katika kikao cha wabunge wa CCM na Rais Kikwete mjini Dodoma mwaka jana, mawaziri Dk. Mathayo David (aliyekuwa wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) na Kawambwa walidaiwa kupwaya na kutakiwa kuondolewa ili kunusuru chama.

Pia vikao vilivyopita mwaka jana, Bunge likiongozwa na wabunge wa CCM walimtaja Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia pamoja na naibu wake Agrey Mwanri kama mizigo kwa kushindwa kukomesha ufisadi kwenye halmashauri.

Katika hatua ya kushangaza, Rais Kikwete katika mabadiliko ya baraza lake hivi karibuni, aliwarejesha mawaziri wote watuhumiwa isipokuwa Dk. Mathayo aliyeng'oka kwa shinikizo la Bunge.

Kurejeshwa kwa mawaziri hao kumeibua mjadala mkali kwa wananchi, huku wengi wakihoji ni kwanini rais hafanyi mawasiliano na chama chake ili kuondoa chuki zinazoweza kujitokeza.

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Kikwete kusigana na CCM, kwani hata wakati wa utekelezaji wa falsafa ya kujivua gamba iliyoasisiwa mwaka 2011 na kusimamiwa na sekretarieti, baadaye ilishindwa kutokana na msimamo wa mwenyekiti huyo.

Itakumbukwa kuwa baada ya falsafa hiyo kuasisiwa, Nape na Naibu Kaibu Mkuu wa CCM (Bara) wakati huo, John Chiligati, walizunguka mikoani wakijiapiza kuwa watuhumiwa wa ufisadi lazima wang'oke ndani ya siku 90.

Hadi muda huo unamalizika, ni mtuhumiwa mmoja pekee, Rostam Azizi, aliyekuwa mbunge wa Igunga ndiye aliyejiuzulu huku akiwatuhumu Nape na Chiligati kuwa walipotosha dhana nzima.

Nape aliwataja Rostam, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, kuwa ni miongoni mwa wanaotakiwa kujivua gamba.

Pia aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Pius Msekwa, alithibitsha baadaye kuwa alikutana na Chenge, Lowassa na Rostam na kwamba taarifa ya matokeo ya mazungumzo itawasilishwa katika vikao vikuu vya chama.

Hata hivyo, baadaye kwenye kikao cha Kamati Kuu (CC), Rais Kikwete alisema kuwa dhana hiyo ilipotoshwa na kuonekana iliwalenga baadhi ya watu, jambo alilosema halikuwa kweli.

Kwa msimamo huo, Lowassa, Chenge na watuhumiwa wengine walijiona washindi na hivyo Nape na sekretarieti yake kutafsiriwa kama viongozi waliokuwa wakiendesha siasa za chuki ndani ya chama.

Tangu wakati huo, yamejengeka makundi ndani ya chama ambayo kwa kiasi fulani yanamwona Nape na sekretarieti kama wafitini wanaojitwika jina la mwenyekiti kuwashughulikia wengine.

Kwa hivyo, hata uamuzi wa Rais Kikwete kuwarejesha baadhi ya mawaziri waliodaiwa na sekretarieti kuwa mizigo, unaelezwa kwamba huenda ukaibua chuki kati ya mawaziri na Nape.

"Hivi hata ungekuwa wewe ni Nape, unapata wapi uhalali wa kuendelea kuongoza watu ambao mwanzo uliwaona hawafai kiutendaji, lakini sasa wamerejeshwa na mkuu wakof?
"Hawa kwa vyovyote watamjengea Nape na sekretarieti yake chuki. Vile vile watamdharau kama kiongozi wao kwa sababu ni mara ya pili sasa anasigana na mwenyekiti wake," alisema mwenyekiti wa CCM wa mkoa ambaye aliomba kuhifadhiwa jina.

Hatua ya Rais Kikwete kuwateua watuhumiwa haiishii ndani ya CCM pekee bali hata baadhi ya wabunge walidai kushangazwa na uteuzi wa Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi, kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula wakati bado anatuhumiwa kuomba rushwa.

Juni 13, 2011, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila, aliwataja wabunge wawili wa CCM bungeni akidai waliomba rushwa katika halmashauri ambayo hakuitaja.

Akichangia mpango wa maendeleo wa miaka mitano, Kafulila aliwataja Zambi na Mbunge wa Bahi, Omary Badwel akidai kwamba aliwakamata wakiomba rushwa kwa viongozi wa halmashauri.

Hadi sasa tuhuma hizo zimekaliwa na ofisi ya spika, huku Kafulila akisisitiza kuwa kile alichokisema ni ukweli mtupu na kwamba ushahidi wake alishaukabidhi, lakini anashangazwa na ukimya uliopo.

Baada ya Kafulila kuibua tuhuma hizo, Badwel alikumbwa tena na kashfa nyingine baada ya kukamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), akidaiwa kuomba rushwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo.

Hivi sasa mbunge huyo anaendelea na kesi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Chanzo: Tanzania Daima
 
Kuna tetesi za kua ccm imejikata vipande kuna ile ccm ya kikwete na kundi lake na kuna ccm ya Nape Nnauye na kundi lake.

Hii ni kila mtu kujionyesha ubavu wake na kukomoana ,mgawanyo huu umekuja pale ndani ya ccm kua na mawazo tafauti kuhusu mchakato wa katiba mpya ilioletwa na kikwete, wako walimpinga kufufua mpango huu na ni wale wenye kutaka itumike katiba ile ile ya zamani.

na wako akina Jk na kundi lake kutaka mfumo wa katiba ilopo ubadilike na kua na kurudishwa kwa Tangayika.

Sasa Nape na kundi lake wanapingana na mabadiliko haya aloyaleta Jk na kusababisha mikomoano, kuto kuwaondoa Waziri mizingo Asemao Nape ni kukomoana kimadaraka na kutunishiana misuli.
tuangalie hatma ya vigogo hawa na muelekeo wa ccm 2015.
 
Hao ndio CCM orijino! Ni uongo na usanii kwa kwenda mbele.

Tanzania bila CCM inawezekana jamani.
 
Na bado hali itazidi kuwa mbaya make hata aliyekuwa wakimtegemea kuwapitisha salama mwaka 2015 kanyang'anywa vyeo vyote na kuna hatihati ya kufukuzwa uanachama.Intelijensia ya CDM iko juu sana aiseee!!!!!.
 
  • Yaliyomkuta kwa magamba yajirudia kwa mawaziri mizigo



KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amepoteza uhalali wake wa kuendelea kushika wadhifa huo, kutokana na utendaji wake kukinzana na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Hali hiyo inatokana na taswira inayozidi kujitokeza kati ya wawili hao katika kusimamia masuala mazito yaliyoasisiwa na chama hicho.

Kwa nyakati tofauti, umejitokeza msigano ambapo wakati Nape akizunguka kwa wananchi mikoani kunadi msimamo wa CCM kuhusu jambo fulani, Rais Kikwete baadaye anajitokeza na kutoa mtazamo tofauti.

Hatua hii imeibua mkanganyiko kwa wananchi, na hivyo baadhi kufikia hatua ya kushauri Nape aachie ngazi ili kuonyesha kuwa amesalitiwa badala ya kuendelea kuonekana adui kwa wale anaosimamia wang'olewe.

Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Bukoba, Dk. Azavery Lwaitama, alizungumzia hali hiyo akisema inaonyesha kuwa hakuna mawasiliano kati ya Rais Kikwete na sekretarieti yake ya chama.

Alisema kuwa kama kungekuwa na mawasiliano ya kutosha, rais asingewateua tena baadhi ya mawaziri waliodaiwa na chama chake kuwa mizigo kuendelea kushika madaraka.

Mwishoni mwa mwaka jana, wakiwa katika ziara za kuimarisha chama mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Nape mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, aliwataja baadhi ya mawaziri akiwaita mizigo kutokana na kushindwa kuwajibika ipasavyo.

Katika mikutano yao tofauti ya hadhara, Nape alikwenda mbali zaidi akisema mawaziri hao lazima waitwe mbele ya Kamati Kuu ya chama kujieleza na kuchukuliwa hatua.

Mawaziri waliotajwa ni Christopher Chiza (Kilimo na Chakula) na Naibu wake, Adam Malima, Dk. Shukuru Kawambwa (Elimu na Mafunzo ya Ufundi) na Prof. Jumanne Mghembe (Maji)
Lakini kama hiyo haitoshi, katika kikao cha wabunge wa CCM na Rais Kikwete mjini Dodoma mwaka jana, mawaziri Dk. Mathayo David (aliyekuwa wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) na Kawambwa walidaiwa kupwaya na kutakiwa kuondolewa ili kunusuru chama.

Pia vikao vilivyopita mwaka jana, Bunge likiongozwa na wabunge wa CCM walimtaja Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia pamoja na naibu wake Agrey Mwanri kama mizigo kwa kushindwa kukomesha ufisadi kwenye halmashauri.

Katika hatua ya kushangaza, Rais Kikwete katika mabadiliko ya baraza lake hivi karibuni, aliwarejesha mawaziri wote watuhumiwa isipokuwa Dk. Mathayo aliyeng'oka kwa shinikizo la Bunge.

Kurejeshwa kwa mawaziri hao kumeibua mjadala mkali kwa wananchi, huku wengi wakihoji ni kwanini rais hafanyi mawasiliano na chama chake ili kuondoa chuki zinazoweza kujitokeza.

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Kikwete kusigana na CCM, kwani hata wakati wa utekelezaji wa falsafa ya kujivua gamba iliyoasisiwa mwaka 2011 na kusimamiwa na sekretarieti, baadaye ilishindwa kutokana na msimamo wa mwenyekiti huyo.

Itakumbukwa kuwa baada ya falsafa hiyo kuasisiwa, Nape na Naibu Kaibu Mkuu wa CCM (Bara) wakati huo, John Chiligati, walizunguka mikoani wakijiapiza kuwa watuhumiwa wa ufisadi lazima wang'oke ndani ya siku 90.

Hadi muda huo unamalizika, ni mtuhumiwa mmoja pekee, Rostam Azizi, aliyekuwa mbunge wa Igunga ndiye aliyejiuzulu huku akiwatuhumu Nape na Chiligati kuwa walipotosha dhana nzima.

Nape aliwataja Rostam, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, kuwa ni miongoni mwa wanaotakiwa kujivua gamba.

Pia aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Pius Msekwa, alithibitsha baadaye kuwa alikutana na Chenge, Lowassa na Rostam na kwamba taarifa ya matokeo ya mazungumzo itawasilishwa katika vikao vikuu vya chama.

Hata hivyo, baadaye kwenye kikao cha Kamati Kuu (CC), Rais Kikwete alisema kuwa dhana hiyo ilipotoshwa na kuonekana iliwalenga baadhi ya watu, jambo alilosema halikuwa kweli.

Kwa msimamo huo, Lowassa, Chenge na watuhumiwa wengine walijiona washindi na hivyo Nape na sekretarieti yake kutafsiriwa kama viongozi waliokuwa wakiendesha siasa za chuki ndani ya chama.

Tangu wakati huo, yamejengeka makundi ndani ya chama ambayo kwa kiasi fulani yanamwona Nape na sekretarieti kama wafitini wanaojitwika jina la mwenyekiti kuwashughulikia wengine.

Kwa hivyo, hata uamuzi wa Rais Kikwete kuwarejesha baadhi ya mawaziri waliodaiwa na sekretarieti kuwa mizigo, unaelezwa kwamba huenda ukaibua chuki kati ya mawaziri na Nape.

"Hivi hata ungekuwa wewe ni Nape, unapata wapi uhalali wa kuendelea kuongoza watu ambao mwanzo uliwaona hawafai kiutendaji, lakini sasa wamerejeshwa na mkuu wakof?
"Hawa kwa vyovyote watamjengea Nape na sekretarieti yake chuki. Vile vile watamdharau kama kiongozi wao kwa sababu ni mara ya pili sasa anasigana na mwenyekiti wake," alisema mwenyekiti wa CCM wa mkoa ambaye aliomba kuhifadhiwa jina.

Hatua ya Rais Kikwete kuwateua watuhumiwa haiishii ndani ya CCM pekee bali hata baadhi ya wabunge walidai kushangazwa na uteuzi wa Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi, kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula wakati bado anatuhumiwa kuomba rushwa.

Juni 13, 2011, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila, aliwataja wabunge wawili wa CCM bungeni akidai waliomba rushwa katika halmashauri ambayo hakuitaja.

Akichangia mpango wa maendeleo wa miaka mitano, Kafulila aliwataja Zambi na Mbunge wa Bahi, Omary Badwel akidai kwamba aliwakamata wakiomba rushwa kwa viongozi wa halmashauri.

Hadi sasa tuhuma hizo zimekaliwa na ofisi ya spika, huku Kafulila akisisitiza kuwa kile alichokisema ni ukweli mtupu na kwamba ushahidi wake alishaukabidhi, lakini anashangazwa na ukimya uliopo.

Baada ya Kafulila kuibua tuhuma hizo, Badwel alikumbwa tena na kashfa nyingine baada ya kukamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), akidaiwa kuomba rushwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo.

Hivi sasa mbunge huyo anaendelea na kesi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Chanzo: Tanzania Daima

Lakini mbona kulikuwa na kauli kuwa NEC ilipeleka maazimio na si azimio moja? Ingekuwa azimio ni moja tu yaani la kuwafukuza lakini kulikuwa na azimio la kupima iwapo hiyo mizigo inaweza kusahihishwa. AU habari lazima iwe kufukuza?
 
Nape ni mchumia tumbo No.1 kuwahi kushuhudiwa ktk historia ya CCM.
 
Thubutu siasa za ccm ndizo zinazomfanya nape aishi mjini,hana ujuzi wowote unategemea ataachia ngazi?
 
Magamba ni kama wale wajenzi wa mnara wa Babeli,huyu akiomba mchanga analetewa maji,huyu akiomba spade analetewa msumari,..yaan ni lugha gongana,..

Yawezekana ni LAANA za wamama wa Tanzania wanaopata shida ya kusaka maji usiku kucha na kula wanne wanne kwenye vitanda waendapo hospitalini kujifungua!
 
06.JPG
 
Masikini nape amepigwa🔒
La mdomo
Magamba yalimshinda
Mafisadi yalimshinda
Na mizigo nayo imemshinda
Sasa tunasubiri ngonjera zake
 
Na bado, kama Lowasa watakuwa mwenyekiti huyu jamaa atatengenezewa kesi ya uhaini
 
ukiwa na akili harafu ukawa mjinga, lazima akili yako ndo ujinga wenyewe. sasa hapo Nape na Kinana bado wanafanya nini CCM??
 
Huyu kijana asivyo na haya atakuja na utetezi dhaifu humu mpk mtashangaa...........kuendekeza tumbo kubaya sana.
 
Mmesahau Nape alifikaje hapo!Kama mnakumbuka alikorofishana na aliyekuwa katibu mkuu wakati huo Mh.Makamba.Aliwatuhumu wadhamini wa UVCCM juu ya Mkataba mbovu wa ujenzi wa jengo lao (uvccm) hadharani!!.Katibu Mkuu wakati huo Makamba akamsimamisha uanachama,mpaka Mwenyekiti alipomtetea na kumbeba mpaka hapo alipofika!Kwa hiyo yanayomfika ndiyo yaliyo wafika Makamba na wenzake.Sasa leo mnashangaa SAMAKI kuishi majini!?Alipaswa kuwa na maono toka wakati huo.Yeye alijiona superstar mbele ya Mh.Makamba,mkuki kwa GURUWE ........!
 
Back
Top Bottom