JK amefanya kazi kubwa

JK amefanya kazi kubwa

kilombero yetu

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Posts
1,004
Reaction score
117
Sababu nyingine kubwa inayowafanya watanzania waendelee kuiamini serikali ya JK ni ukweli kwamba Tanzania ni miongoni mwa mataifa manne barani Afrika ambayo uchumi wao unakua kwa kasi,unajua hv sasa nchi iko pazuri in terms of ujenzi wa miundo mbinu kama barabara za lami,viwanja vya ndegen.k....

JK vilevile amefanya kazi kubwa kuhakikisha hospitali zote za mikoa hapa nchini zinaboreshwa na kupandishwa hadhi ..nchi imepiga hatua katika kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga, ugonjwa wa UKIMWI unaweza usiwe janga la Taifa tena kulingana na takwimu tulizonazo.

Sasa serikali ihakikishe reli ya kati inaboreshwa na reli ya Arusha-Tanga inajengwa upya...kuhusu tatizo la nishati ya umeme ni dhahiri kwamba tatizo hili nalo linaelekea kusuluhishwa baada ya ugunduzi wa gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
sababu nyingine kubwa inayowafanya watanzania waendelee kuiamini serikali ya JK ni ukweli kwamba Tanzania ni miongoni mwa mataifa manne barani Afrika ambayo uchumi wao unakua kwa kasi,unajua hv sasa nchi iko pazuri interms of ujenzi wa miundo mbinu kama barabara za lami,viwanja vya ndegen.k....JK vilevile amefanya kazi kubwa kuhakikisha hospitali zote za mikoa hapa nchini zinaboreshwa na kupandishwa hadhi ..nchi imepiga hatua katika kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga, ugonjwa wa UKIMWI unaweza usiwe janga la Taifa tena kulingana na takwimu tulizonazo.....sasa serikali ihakikishe reli ya kati inaboreshwa na reli ya arusha-Tanga inajengwa upya...kuhusu tatizo la nishati ya umeme ni dhahiri kwamba tatizo hili nalo linaelekea kusuluhishwa baada ya ugunduzi wa gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara.....MUNGU IBARIKI TANZANIA

AMEN. Na sala zeu zisikilizwe na Mwenyezi Mungu!.
 
Ndugu yangu, unaongea siasa kumsifu JK. Uchumi umekua?? Hivi unajua maisha yamekuwa magumu zaidi kuliko yalivyokuwa kabla hajaingia madarakani? Mfumuko wa bei ulishafikia 19%, sasa uchumi ukikua kwa 7% alafu mfumuko wa bei uko 19%, je kimahesabu hapo uchumi umekua? Kama uwezo wako wa kupata pesa umeongezeka kwa 7% lakini bei ya manunuzi imeongezeka kwa 19% bado unaringa kuwa uchumi umekuwa, si kujidanganya? Alafu, je mgawanyo wa huo uchumi ukoje? Ninachokiona ni kuwa, pesa zinajirundika kwa mafisadi wachache tu, na watanzania walio wengi wamekuwa fukara zaidi. In fact, hali imekuwa mbaya zaidi, vijana wengi wana hali ngumu sana. Na hili linajionyesha katika vitendo vya uhalifu. Wiki iliyopita tu wamempiga risasi mwanafunzi wa mwaka wa nne pale chuo kikuu cha dar es salaam na kuwanyanganya laptops. Lakini vitendo vya wizi, vimeongezeka sana, kwa sababu vijana hawana pesa, hawana chakula wanaona hiyo ndiyo best option waliyo nayo. Na Lowasa amelisema kuwa hili ni bomu linakokaribia kupasuka.
By the way, suala la Ukimwi na vifo vya mama waja wazito kupungua, in fact havikupungua ila kilichoimarika ni ukusanyaji wa data sahihi tu. Wengi tuliozaliwa vijijini tutakumbuka kuwa wakunga wa jadi walikuwa efficient sana. mwanamke kufa wakati akizalishwa na mkunga wa jadi ilikuwa ni kitu cha nadra sana. mimi hata sikumbuki mwanamke kijijini kwetu aliyefariki wakati anazalishwa na mkunga wa jadi huko vijijini. Lakini baada ya kuwasomesha wasichana wadogo na kuwaambia wazalishe watu, ndio vifo hapo vikaanza. Na taarifa zilikuwa zinakuwa exaggerated. Ni ka taarifa za ukimwi tu zilivyokuwa zinakuwa inflated.
Kasi ya ujenzi wa barabara imepungua sana. In fact, Mkapa aliwezesha ujenzi wa barabara mkubwa zaidi ya JK. Hata ile ya kwenda Mtwara alijenga sehemu kubwa yeye ikiwa ni pamoja na daraja la Mkapa, na baada ya kuondoka hakuna kilichoendelea cha maana. Mwaka 2010 nilipakia basi kwenda Mtwara, bado haijaisha. Ushauri wako kuhusu reli ni mzuri, lakini nakuhakikishia kuwa hautachukuliwa kwa sababu wadau wakubwa wa usafirishaji hasa wa mizigo kwa kupitia malori hapa nchini ni pamoja na huyo unayemsifu JK. Kwa hiyo akiimarisha reli atakosa biashara. Suala la uimarishaji reli lingekuwa dogo sana, hata ukikopa hela kwa ajili ya ujenzi wa reli inalipa sana kwa sababu gharama za usafiri wa reli ni 10% ya gharama za usafiri wa barabara. Lakini hilo halitafanyika hata siku moja kwa sababu utagusa ulaji wa watu wachache, na anayeendelea kuumia ni mwananchi wa kawaida.
Tatizo la nishati ya umeme linaendelea akushughulikiwa, kwa kasi ndogo. South Korea iliwekeza hela kama nne za kitanzania (3bil. Usd) kwa ajili ya umeme wa bahari na geothermo, kwa muda wa miaka mitatu mradi wa umeme ukakamilika wakapata 3000MW, sisi siasa hizi zilianza mwaka 2008. Ninapoandika huu ujumbe miaka mitano imeshapita, na katika hiyo miaka ukiangalia bajeti ya nishati na madini kwa kila mwaka imekuwa zaidi ya trilioni moja. Ina maana kuwa zaidi ya trillion 5 zimeshatumika, hatuoni umeme wa kutosha. Kwa hiyo wanashughulikia midomoni tu na kuwadanganya watu kama wewe
 
sababu nyingine kubwa inayowafanya watanzania waendelee kuiamini serikali ya JK ni ukweli kwamba Tanzania ni miongoni mwa mataifa manne barani Afrika ambayo uchumi wao unakua kwa kasi,unajua hv sasa nchi iko pazuri interms of ujenzi wa miundo mbinu kama barabara za lami,viwanja vya ndegen.k....JK vilevile amefanya kazi kubwa kuhakikisha hospitali zote za mikoa hapa nchini zinaboreshwa na kupandishwa hadhi ..nchi imepiga hatua katika kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga, ugonjwa wa UKIMWI unaweza usiwe janga la Taifa tena kulingana na takwimu tulizonazo.....sasa serikali ihakikishe reli ya kati inaboreshwa na reli ya arusha-Tanga inajengwa upya...kuhusu tatizo la nishati ya umeme ni dhahiri kwamba tatizo hili nalo linaelekea kusuluhishwa baada ya ugunduzi wa gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara.....MUNGU IBARIKI TANZANIA

Mtabadili ID kila uchwao hadi mmalize majina yote ya dunia hii.

Kwa kukusaidia, angalau unge fuatilia mchango wa yule Mh. Kessy bungeni. Licha ya kutoa pumba kila siku Bungeni, elimu ya M4C imemuingia na kuweza kuipasha ukweli serikali yake ya MAGAMBA.

Hivyo viwanja vya ndege nani mwenye uwezo wa kuvitumia kama sio MAFISADI?

Au hujui kwamba wakati wa Mwl Nyerere viwanja vya ndege vilikuwepo hadi wilayani. Flying Doctors walikuwa wanarusha ndege zao hadi kwenye Air Strips za vijijini. Wewe unabaki kusifia viwanja vya ndege vya kutoroshea rasilimali zetu!

Kiongozi! Unapo leta mada JF, jaribu kushirikisha akili yako. Si lazima kila kitu upate maagizo kutoka kwa Mwigulu!!!
 
Elimu jeee?

"To know the enemy is half the victory"
 
Maendeleo yanapimwa by using two indicators
1.Qualitative indicators.
2.Quantitative indicators.
Tz mostly wanatumia quantitative indicators kam vile barabara,reli,hospitali na majengo makubwa ambayo hayana mchango wowote kwa mwananchi wa kawaida unless they have measured in terms of services they provide in right proportion.Hakuna maendeleo wala in economic development point of view.
 
Kikwete atakumbukwa kwa Katiba mpya tuu,kama hataiingiza uccm ktk jambo hilo!!!na kuwapa kina mama nafasi nyingi katika govt haswa za ubalozi!Hana jipya alilofanya labda yake binafsi kama kupenda safari etc
 
Sijui ni macho yangu au ni akili zako!!! Haya tutaendelea "kuiamini" serikali sikivu
 
Naona unataka JK afurahi kwa mara ya kwanza tangu ajiunge JForum............
 
labda kazi ya kusafiri nje kula bata kwa hela za wavuja jasho wadanganyika, zaidi ya hapo hamna kitu
 
Hongera! Umeteuliwa kua mkuu wa wilaya ya lumumba
 
ni kweli nakuunga mkono sana.....kaua,kaacha vilema,katoa ruksa kupigwa,katoa kucha,meno,pasua macho,tia ngeu watu,kutoweka hadi leo hawajulikan wakowapi...ni mengi sana haya yanatosha.
 
Back
Top Bottom