JK; Alishazoea kuhadaa, wala simshangai

JK; Alishazoea kuhadaa, wala simshangai

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,946
Reaction score
38,663
Wadau,
Suala la uteuzi wa wajumbe ama wabunge wa Bunge la Katiba Mpya limekuwa gumzo nchini ambapo tayari benbdera mbili zimepandishwa. Bendra ya kwanza ni ya wanazi ama wahafidhina ambao kwao lolote linalofanywa na serikali kwao ni sahihi na watatetea kwa nguvu zote hata kama lina madhara huko mbeleni

Bendera ya pili ni wale ambao wanapenda kuyachambua mambo ili kupima matokeo yake kabla ya kufanyika kwa jambo hilo.

Halafu kuna wale wasio na bendera ambao kwao wanaona lolote ni majaaliwa, Hawapingi wala hawakubali yaani msimamo wa kati.

Hadaa ya JK ilianzia pale alipotangaza kwamba serikali itaanzisha mchakato wa katiba mpya huku akijua kabisa kwamba ile haikuwa agenda yake wala chama chake. Kwa ushahidi wa hilo, ni pale Waziri mwenye dhamana na katiba (Celine Kombani) alipotoa msimamo wa serikali kwamba hawana nia wala mpango wa kurekebisha katiba au kuunda katiba mpya. Na pia Katiba haibadilishwi kwa maneno ya mitaani. Pia alikuja Werema (Mwanasheria Mkuu) aliyesema kuwa hakuna suala la katiba mpya kwenye mipango ya serikali. Ndipo JK aliibuka na kuhaidi serikali itasimamia mchakato wa katiba mpya.

Wengi mlishangilia, na hamkuona ni tatizo pale watu wale wale (Kombani, Werema) kusimamia hatua za lazima za awali za mchakato wa kuandaa muswada wa sheria ya Rasimu ya Katiba Mpya. Wengi hamkuliona na hata wachache waliojitokeza kupinga namna mchakato ulivyoendeshwa kwa ujanja walionekana ni wapiga kelele tu.

Haya sasa! Sheria ikapitishwa kwa mbwembwe (kuukomoa upinzani Bungeni) ila raia wengi walipiga kelele kutohusishwa na mchakato ule lakini baada ya kupitishwa bungeni huku tishio la upinzani kuzunguka nchi nzima kuipinga sheria ile likiitikisa serikali ya JK. Hatimaye alitumia turufu ya kuwaita viongozi wa upinzani na makundi mbalimbali ikulu, ambapo siyo Ikulu hata wahusika waliowahi kusema kile walichokubaliana na JK. Hatimaye ikaundwa Tume ya Warioba ambayo pamoja na mambo mengine ilionekana wazi alijaza makada kwenye tume ile. Wengi mlikaa kimya hakuona tatizo kwa sababu ya upofu wa kutopenda kufuatilia mambo.

Rasimu ya Kwanza ilipotoka, ndipo mimi binafsi yangu nilipoona kwamba Kikwete amedhamiria kusimamia mchakato wa katiba ambapo haina utashi wa wengi (raia). kupitia rasimu ile kuliundwa mabaraza ya Kata na Wilaya ya Katiba huku kukiibuka malalamiko mengi ya kimsingi kuhusu uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza hayo. UDINI na UKADA ulihusika katika kuunda yale mabaraza lakini hakuna kilichorekebishwa zaidi ya kubeza malalamiko yale na mchakato ukaendelea.

Lilipoanza kuongelewa suala la Bunge la Katiba, watu waelewa walianza kupiga kelele kuhusu utaratibu wa kuwapata wabunge wa Bunge la Katiba. Moja ya masuala waliyopinga ni pamoja na
  1. Wabunge wa Bunge lililopo kutoshiriki kwenye Bunge la Katiba kutokana na hadidu za majukumu yao.
  2. Rais asiteue wajumbe wa Bunge hili bali wananchi wawapigie kura kwa utaratibu rasmi ili kupata wabunge wa Bunge Maalum la Katiba
  3. n.k.

Kwa namna ambavyo uteuzi uliofanywa na rais akishirikiana na rais wa Zanzibar umeonesha wazi mwelekeo wa mchakato wa Katiba Mpya ulivyopangwa na kupangika. Tunaenda kuletewa katiba yenye utashi wa CCM na si vinginevyo, ushahidi ni vile ambavyo makada wa chama tawala walivyojazwa kwenye nafasi za wajumbe wa kuteuliwa. Hii inaonyesha wazi kabisa kwamba kuna makundi kwenye jamii yamebaguliwa na hayatakuwa na nafasi kwenye mchakato huu wa Katiba. Kuna watetezi (wahafidhina) wanasema kwamba majina aliyoleta rais yametokana na mapendekezo aliyopelekewa, lakini hawathibitishi kama hao wateuliwa ni miongoni mwa majina yaliyopendekezwa.... Mfano mmoja mdogo tu. Katika nafasi ya ASASI ZA KIRAIA kuna jina la Mzee Kingunge Ngombare Mwiru, mtu unakosa majibu hapo kuwa ni asasi gani ya kijamii ambayo Kingunge ni mtendaji wake na amependekezwa.... Majina ni mengi na yanadhihirisha utashi wa rais na chama chake kutuletea Katiba wanayoitaka wao.

KURA YA MAONI.

Hili ni suala jepesi mno kwa serikali hii, kwa sababu;
Kwanza sidhani kama Daftari la wapiga kura litaboreshwa kwa wakati ili kuwaingiza Watanzania waliofikia umri wa kupiga Kura.
Pili ni kwamba mchakato wa upigaji kura utasimamiwa na TUME isiyo huru wala haki kutokana na historia yake inayokipendelea Chama tawala kwenye kila uchaguzi.
Tatu, ni kwamba tambo na nasaha za viongozi wa umma majukwaani kuwaasa wabunge wa Bunge hili kutoweka maslahi yao mbele hayana mashiko kwa sababu inafahamika wazi kwamba Wanachokihubiri ni tofauti na wanachokitenda gizani.
Nne, mjadala wa muundo wa Muungano umekuzwa mno na vyombo vya propaganda ili kuiondoa jamii kwenye kujadili ama kutazama mambo ya msingi kwenye rasimu na watu kujikita kwenye ushindani wa muundo wa muungano.

Hivyo tutapata katiba mpya ndiyo, lakini ieleweke kwamba Mchakato mzima umetekwa na wanasiasa chini ya ukinara wa JK na Chama chake, Na ieleweke kwamba Katiba Mpya haikuwa kwenye ilani ya uchaguzi ama katika ahadi ya mgombea yeyote wa CCM wakati wa kampeni 2010.

Nahitimisha kwa kusema kwamba Katiba iliyopo imechezewa sana, na hiyo Katiba Mpya ijayo imeshaanza kuchezewa hata kabla haijachapwa. Na ieleweke kwamba ndani ya mioyo ya wakuu wa nchi hii HAKUNA mwenye nia ya dhati ya kuwaletea Watanzania Katiba Mpya kwa manufaa na matakwa ya raia.

Hadaa ya wanasiasa ni anguko la nchi!
 
Hakuna lililo jema litakalo toka kwenye serikali hi ya Kikwete.
 
Hakuna mtu makini kama kikwete, hata mbowe na slaa wanajua
 
Siku zote ukiona katika nchi watu hawataki mabadiliko ujue asilimia kubwa ni wajinga, tena mambumbumbu, huu ni ujinga, kama wananchi hatujajifunza kitu katka hii miaka 50 ya uhuru basi tujiandae siku moja rais wa nchi kuchaguliwa kwa kura elfu moja, ujinga mtupu
 
Siku zote ukiona katika nchi watu hawataki mabadiliko ujue asilimia kubwa ni wajinga, tena mambumbumbu, huu ni ujinga, kama wananchi hatujajifunza kitu katka hii miaka 50 ya uhuru basi tujiandae siku moja rais wa nchi kuchaguliwa kwa kura elfu moja, ujinga mtupu

kwa hiyo na wewe ni mjinga?
 
Kuna waliokuwa wanampelekea vimemo na ujumbe Rais vya kugomba kuteuliwa - kwa mujibu wa Rais JMK.
 
Utakufa na husuda na chuki ulizofundishwa ufipa

Kwanza hakuna chema alilolifanyia taifa hili wala watuwake. Ukinipa mmoja mimi nitakupa maovu 10 kwa kila mmoja. labda kuwakirimu watu wake, kwa kodi za walala hoi
 
Kuna Watanzania wenzetu ambao kwao hawaoni na wameziba njia zote za kujielimisha.

Watu wanashindwa hata kusoma hoja na kujibu items zilizoibuliwa hapo halafu wanakuja na sentensi mbili tu kujaribu kubeza kitu asichokielewa.

Nasisitiza kwamba Hadaa ya wanasiasa ndiyo anguko letu. JK ni mwanasiasa
 
Back
Top Bottom