Ila anafanya vizuri hivi tujiulize uhuru anaotoa JK umesaidia sana kufukua mengi kwa kweli japo anachelewa kuchkua hatua.Ni kweli aliwah kusema,siku aliyopokea hzo taarifa IKULU ndo alimwambia CAG apeleke Bungeni zijadiliwe
Katika hotuba yake kwa watanzania kupitia sherehe za Mei Mosi leo, Rais Kikwete amezungumza mengi kuhusu taarifa za CAG na utekelezaji wa mapendekezo ya CAG. Mojawapo ya mambo aliyosema ni kwamba aliagiza CAG aweke taarifa za ukaguzi wazi ili wananchi wazijadili. Sijawahi kusikia hiyo kauli wala waraka unaoelekeza hivyo. Lakini hilo siyo tatizo.
Enzi za utawala wa BWM, idara na Wizara nyingi za serikali ndo ziliwezeshwa kuanzisha tovuti na kuweka taarifa muhimu za serikali. Ofisi ya CAG nayo ilianzisha tovuti yake kipindi hicho, kama ilivyokuwa nyingine, kwa ufadhili wa serikali za nje.
Wakati huo CAG alikuwa akibandika taarifa zote za ukaguzi. Yaani taarifa kuu kama zinazobandikwa sasa (serikali kuu, serikali za mitaa na Mashirika ya umma). Alifanya zaidi, akibandika taarifa za ukaguzi na hesabu za kila Wizara, shirika la umma na kila halmashauri na mkoa. Hakuishia hapo, alitoa nakala zilizosainiwa kwa mtu yeyote (mtu yeyote) aliyeomba nakala ya ukaguzi ya taasisi yoyote ya umma.
Kuanzia mwaka 2006, CAG hajabandika taarifa za ukaguzi za taasisi moja moja na alikataa kutoa nakala za taarifa hizo pale zilipoombwa. Madai yake yalikuwa "Ni maagizo kutoka juu". Pia ukifuatilia taarifa hizo kwenye taasisi husika zimezuiwa kwa maelezo hayo hayo.
Ni vema ikaeleweka kwamba aina ya taarifa anazobandika CAG tangu 2006, hazimuwezeshi mtu kupata picha nzima ya financial management ya taasisi moja moja na hivyo hutaweza kutoa maoni wala kutatua matatizo yaliyopo. Pengine ndiyo maana, kama alivyosema Rais, hati safi zimeongezeka kipindi cha utawala wake, lakini pia amekiri viwango vya ufujaji wa pesa za umma vimepindukia kila ngazi ya serikali.
Swala la pili, Rais amesema aliagiza mjadala wa wazi wa ripoti za CAG bungeni. Hilo niwaachie mpime wenyewe!
Nimeona nitoe maoni yangu tu
JK kusema kweli katoa uhuru wa kweli wa mambo kuchambuliwa sasa ni wakati wa sisi kutunga sheria mtu apelekwe mahakamani moja kwa moja baada ya hapo lakini yeye kama mkuu wa nchi hawezi kufanya hivyo maana sheria nazo zatungwa na Bunge. Na wabunge ndio wanakuwa wakali bila kujua je rais ana mamlaka ya kumfunga huyo waziri au ana uwezo wa kumtimua tu kazi? Sasa ina sadia nini kama atamtoa uwaziri bila kumwajibisha? Kuna pich napata tunakimbilia kumlaumu tu rais bila kujua mipaka ya utendaji wake.
Ila anafanya vizuri hivi tujiulize uhuru anaotoa JK umesaidia sana kufukua mengi kwa kweli japo anachelewa kuchkua hatua.
LAKINI NIMEANZA KUHISI NA KUONA KUWA TUTAMKUMBUKA SANA KWA UHURU HUU NA STYLE YAKE YA KUWAFUMBUA WATANZANIA, HILO HALITAKUWA NA MJADALA SUBIRINI BAADA YA 2015, TENA IKITOKEA MKAFANYA KOSA CCM AWE MEMBE!!!
ILA AKIWA SLAA/ZITTO/MKIRA NAO WAENDELEZE UHURU HUO.
JK kusema kweli katoa uhuru wa kweli wa mambo kuchambuliwa sasa ni wakati wa sisi kutunga sheria mtu apelekwe mahakamani moja kwa moja baada ya hapo lakini yeye kama mkuu wa nchi hawezi kufanya hivyo maana sheria nazo zatungwa na Bunge. Na wabunge ndio wanakuwa wakali bila kujua je rais ana mamlaka ya kumfunga huyo waziri au ana uwezo wa kumtimua tu kazi? Sasa ina sadia nini kama atamtoa uwaziri bila kumwajibisha? Kuna pich napata tunakimbilia kumlaumu tu rais bila kujua mipaka ya utendaji wake.
Mkuu uhuru wa kujadili ripoti za CAG bungeni umetolewa na JK? Mimi nadhani Bunge la mwaka huu halikujadili kwa upana sana ripoti za CAG kama lilivyowahi kufanya miaka ya nyuma. Utagundua kwamba kilichopelekea Sahihi 70 ni Wabunge kuchoka kujadili tu kila mwaka na hatua hazichukuliwi. Nadhani hivyo
Ni kweli aliwah kusema,siku aliyopokea hzo taarifa IKULU ndo alimwambia CAG apeleke Bungeni zijadiliwe