JK alikusudia Kutudanganya, au alidanganywa ili atudanganye? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK alikusudia Kutudanganya, au alidanganywa ili atudanganye?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, May 1, 2012.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Katika hotuba yake kwa watanzania kupitia sherehe za Mei Mosi leo, Rais Kikwete amezungumza mengi kuhusu taarifa za CAG na utekelezaji wa mapendekezo ya CAG. Mojawapo ya mambo aliyosema ni kwamba aliagiza CAG aweke taarifa za ukaguzi wazi ili wananchi wazijadili. Sijawahi kusikia hiyo kauli wala waraka unaoelekeza hivyo. Lakini hilo siyo tatizo.

  Enzi za utawala wa BWM, idara na Wizara nyingi za serikali ndo ziliwezeshwa kuanzisha tovuti na kuweka taarifa muhimu za serikali. Ofisi ya CAG nayo ilianzisha tovuti yake kipindi hicho, kama ilivyokuwa nyingine, kwa ufadhili wa serikali za nje.

  Wakati huo CAG alikuwa akibandika taarifa zote za ukaguzi. Yaani taarifa kuu kama zinazobandikwa sasa (serikali kuu, serikali za mitaa na Mashirika ya umma). Alifanya zaidi, akibandika taarifa za ukaguzi na hesabu za kila Wizara, shirika la umma na kila halmashauri na mkoa. Hakuishia hapo, alitoa nakala zilizosainiwa kwa mtu yeyote (mtu yeyote) aliyeomba nakala ya ukaguzi ya taasisi yoyote ya umma.

  Kuanzia mwaka 2006, CAG hajabandika taarifa za ukaguzi za taasisi moja moja na alikataa kutoa nakala za taarifa hizo pale zilipoombwa. Madai yake yalikuwa "Ni maagizo kutoka juu". Pia ukifuatilia taarifa hizo kwenye taasisi husika zimezuiwa kwa maelezo hayo hayo.

  Ni vema ikaeleweka kwamba aina ya taarifa anazobandika CAG tangu 2006, hazimuwezeshi mtu kupata picha nzima ya financial management ya taasisi moja moja na hivyo hutaweza kutoa maoni wala kutatua matatizo yaliyopo. Pengine ndiyo maana, kama alivyosema Rais, hati safi zimeongezeka kipindi cha utawala wake, lakini pia amekiri viwango vya ufujaji wa pesa za umma vimepindukia kila ngazi ya serikali.

  Swala la pili, Rais amesema aliagiza mjadala wa wazi wa ripoti za CAG bungeni. Hilo niwaachie mpime wenyewe!

  Nimeona nitoe maoni yangu tu
   
 2. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hayo ni yako,, mh rais ameeleza vzr sana tumemuelewa.
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ni kweli aliwah kusema,siku aliyopokea hzo taarifa IKULU ndo alimwambia CAG apeleke Bungeni zijadiliwe
   
 4. M

  Mkira JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2012
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ila anafanya vizuri hivi tujiulize uhuru anaotoa JK umesaidia sana kufukua mengi kwa kweli japo anachelewa kuchkua hatua.

  LAKINI NIMEANZA KUHISI NA KUONA KUWA TUTAMKUMBUKA SANA KWA UHURU HUU NA STYLE YAKE YA KUWAFUMBUA WATANZANIA, HILO HALITAKUWA NA MJADALA SUBIRINI BAADA YA 2015, TENA IKITOKEA MKAFANYA KOSA CCM AWE MEMBE!!!

  ILA AKIWA SLAA/ZITTO/MKIRA NAO WAENDELEZE UHURU HUO.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Gurudumu, kiongozi wetu ni muongo na hata mara nyingine anasahau kwamba anasema uongo maana amefikia stage ya kujidanganya mwenyewe. Oohhh myyyyy
   
 6. b

  buzz Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  JK kusema kweli katoa uhuru wa kweli wa mambo kuchambuliwa sasa ni wakati wa sisi kutunga sheria mtu apelekwe mahakamani moja kwa moja baada ya hapo lakini yeye kama mkuu wa nchi hawezi kufanya hivyo maana sheria nazo zatungwa na Bunge. Na wabunge ndio wanakuwa wakali bila kujua je rais ana mamlaka ya kumfunga huyo waziri au ana uwezo wa kumtimua tu kazi? Sasa ina sadia nini kama atamtoa uwaziri bila kumwajibisha? Kuna pich napata tunakimbilia kumlaumu tu rais bila kujua mipaka ya utendaji wake.
   
 7. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Ni upepo tu. Utatulia !
   
 8. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nafikiri wachangiaji wengi mmeongozwa na ushabiki zaidi, mwanzisha mada kajaribu kutoa na ushahidi wa hoja zake lakini naona wanaopinga hawaonyeshi popote kuwa hoja za mtoa mada ni za uongo au kutoa uthibisho wa kuona kuwa wao ndio wako sahihi.

  Siamini kuwa hoja zenu zinajengwa katika maneno ya hutuba ya leo tu, maana kwa mtu wa kawaida kama mimi inanipa taabu kuamini kuwa alitaka wabunge waijadili vile ile taarifa. Kama ni kweli leo hii wala Zito asingelikuwa shujaa, hebu support arguements zenu nasi tupate kupima.

  Hapa tena vyombo vya habari vinayo nafasi ya kutuletea kumbukumbu tena, ili tupate kujua mchele ni upi na ngano ni ipi.
   
 9. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mkuu, Public Audit Act imeweka bayana katika kifungu 11(5) kuhusu mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya aliyekula pesa za umma. Paymaster General au Accounting Officer anatakiwa kuchukua hatua kwa mujibu wa mapendekezo ya CAG. Publi Audit Act pia imempa mamlaka CAG katika kifungu 12(c) kushauri Bunge litunge sheria ya kutekeleza mapendekezo yake kumchukulia mwizi hatua pale atakapogundua sheria zilizopo hazikidhi haja

  Kwa ujumla sheria zipo na zina meno, hakujakuwa na nia ya kuwachukulia hatua walioiba pesa na mali za umma. JK anacheza na ukweli kwamba wananchi hawazisomi hizo sheria, hivyo hachukui hatua, kisha anatudanganya
   
 10. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  sisi tunataka tuone watu wakichukuliwa hatua...,hatutaki maneno mengi......,tumeshayasikia sanaaa,...................tumechoka........jamani....!
   
 11. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mkuu uhuru wa kujadili ripoti za CAG bungeni umetolewa na JK? Mimi nadhani Bunge la mwaka huu halikujadili kwa upana sana ripoti za CAG kama lilivyowahi kufanya miaka ya nyuma. Utagundua kwamba kilichopelekea Sahihi 70 ni Wabunge kuchoka kujadili tu kila mwaka na hatua hazichukuliwi. Nadhani hivyo
   
 12. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Unasema sasa ni wakati wetu kutunga sheria mtu apelekwe mahakamani moja kwa moja - unaishi dunia gani? Unataka kusema Tanzania hakuna sheria zinazohukumu wafujaji na wezi wa mali za umma? Come one, wake up out of your sleep, hapa kunatakiwa vitendo vikali dhidi ya wahalifu hawa na si ungese huu wa Kikwete kujibaraguza kuwa eti awamu yake imeweka uhuru; this is shit.
   
 13. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Dibaji ya CAG inasema hivi:"Kutungwa kwa Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya mwaka 2008 kumeongeza mawanda ya ukaguzi wangu kwa kunipa madaraka ya kufanya kaguzi nyingine zaidi ya ukaguzi wa kawaida wa taarifa za fedha.

  Kwa mujibu wa sheria hii natakiwa kufanya ukaguzi wa ufanisi, utambuzi na mazingira na kaguzi mbalimbali maalum kama zinavyojitokeza.

  Ni matumaini yangu kwamba, kwa kuanzishwa kwa sheria mpya ya Ukaguzi wa Umma, Ofisi yangu itaweza kuimarisha udhibiti wa fedha na kuisaidia Serikali kuimarisha uwajibikaji.

  Sheria hii pia itaniwezesha kuwa huru katika kulithibitishia Bunge masuala yanayohusu uwajibikaji, uwazi na matumizi bora ya rasilimali hasa kuona kwamba rasilimali hizo zimetumika vizuri kwa kuzingatia uchumi,ufanisi na kama ilivyotarajiwa na kupitishwa na Bunge."

  Bado haitoshi? Hivi nyie wenzangu mnaosema enzi za JK ripoti za CAG zilifanywa siri mnakaa dunia ipi? Mbona hata ilikuwa ukienda pale uwanja wa maonesho (Sabasaba) huwa CD za ripoti ya CAG zinatolewa kama njugu? Tatizo lenu, hamtaki kutafuta habari.....hizi ripoti kwa muda mrefu zinapatikana tena kiurahisi kabisa!
   
 14. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Miaka ya nyuma ipi? Toa Reference basi....2008, 2010, 2000, 1993, 1978, or? Unazungumzia zama za Nyerere, Mwinyi au Mkapa?! Mbona kama hujiamini na unachokiongea?!
   
 15. B

  Bob G JF Bronze Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Anajikosha 2, Maneno bila vitendo ni Bure, Ni mtu wa aina gani kila kitu anaamuliwa na watu wengine? Watanzania waleo huwezi kuwadanganya tena! Ni lazima tukiri kwamba rais wetu ni DHAIFU sana na hana sifa ya kuwa Rais, ameifanya nafasi ya urais itamaniwe na watu hata wasio na akili wakijilinganisha na Jk the way anavyoongoza nchi.

  Cheo cha urais kimepoteza HADHI kabisa, amekua kiongozi wa misiba, safari, na mambo madogomadogo ya kufikia hata kuandaliwa party na cloud, amekua kiongozi asie na maamuzi hata asie soma nyakati, IKO HAJA YA KUMFANYIA MAOMBI maana pepo huyu alienae anatuangamiza.
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  May 1, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kama kwa Ahadi za maisha bora kwa kila mtanzania alitudanganya atakuwa alikusudia kutudanganya. Kama kwa Ahadi za maisha bora kwa kila mtanzania alidanganywa ili atudanganye, atakuwa alidanganywa ili atudanganye.
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  May 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu kupeleka bungeni ni suala la kikatiba na lipo wazi kabisa. Alichosisitiza Rais ni kwamba siyo hati ziwekwe mezani tu bali Report ya CAG ipate muda wa kutosha wa kujadiliwa Bungeni.

  Jana nimeulizia Report ya CAG yaani general report iliyojadiliwa bungeni nikaelekezwa niende ofisini ama nimtume mtu akanichukulie bila malipo yoyote.

  Mtoa mada anasema report zinazotangazwa haziwezi kumfanya mtu kutoa ushauri; ni kweli. wanachoweka pale hasa kwenye magazeti ni sehemu tu ya report yaani Opinion ambayo pale utapata kujua tu kama taasisi imepewa hati safi, ya mashaka ama chafu au mkaguzi alishindwa kabisa kutoa hati (disclaimer). Pale kunakuwa hakuna kitu kinachoitwa management letter ambayo ndiyo inaongelea matatizo ama
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  May 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Samahanini wakuu sikuweza kumakizia hiyo post ya hapo juu kwa kuwa MCHINA wangu amekohoa! Lakini nadhani ujumbe umefika.
   
 19. D

  Deo JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Asante saana mkuu.

  Tuseme ukweli, ile hotuba ilituudhi wengi sana. JK ni baba wa uwongo, wateule wake ni cha mtoto.
  Quote yako hapo juu inadhihirisha alivyo ficha ukweli, na uongo wa hotuba yake. Itawezekanaje ateue mafisadi tena kiundugu halafu awathibiti?

  Hotuba yote ni juu ya kazi na ripoti ya CAG ni ya unafiki kana kwamba yeye ni malaika na maagizo yote mema aliyatoa, sasa iweje asichukue hatua miaka yote?

  Lets vote him out, ni janga la taifa
   
 20. Ciphertext

  Ciphertext Senior Member

  #20
  May 1, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani anamkagua CAG? Nani anamonitor utendaji kazi wake?
   
Loading...