JK akataa stendi ya muda!

Huenda kwenye ulaji huu hakuna mtu wake hivyo ameamua kujitoa kimasomaso. Mbona haoni ulaji wa Tanesco, IPTL, Dowans na madudu mengine mengi yenye kila baraka zake? Mbona haoni madudu ya WAMA na uagizaji mafuta nje ambapo kuna mkono wa watu wake wakiongozwa na Rahma Kharoos Kasiga aka Nyumba ndogo ya mkubwa wa inchi? Mambo mengine yanachekesha. Hata hivyo haiko mbaya hizo ndizo sanaa za mkuu mwenyewe. Yeye akifuja pesa ya umma kwa matanuzi ughaibuni si kufuja siyo?

Two wrongs do not make up a right mkuu.
Kwakuwa yeye anafuja ela ya watanzania kwa kusafiri na mambo mengine hiyo haimpi haki na mtu mwingine kufuja pia.
 
raisi kikwete kawaagiza mkuu wa mkoa wa dar na menaja wa tanrods mkoa wampe majibu ndani ya wiki moja ni wapi itajengwa stendi mpya baada ya ile ya ubungo kuhamishwa.
Amekataa wazo lao la kujenga stendi ya muda pale chuo kikuu (udsm) na kuwaambia huko ni kufuja fedha za serekali.
Jk alikuwa anaweka jiwe la msingi ktk mradi wa mabasi yaendao kasi.

kama angekuwa serious tangu ashike madaraka kama alivyofanya jana, labda tungesogea kwa kwenda mbele japo mita moja, sasa kawachekea ndo anakuja kuwapiga mkwara mwishoni. Isije kuwa kanyimwa mgao
 
Siku zote raisi makini, anafanya maamuzi makini. Hongera jakaya.

JK Jana alifanya nijisikie nawezajivuna mbele za watu kuwa Rais wangu anafanya maamuzi mazito na ya busara kwa wakati, 2010 nilikuwa nje ya nchi wenyeji wakapenda kufahamu hbr za Rais wa Tanzania nchi yenye AMANI UTULIVU mwisho wakaniuliza Rais wenu analindwa? nilicheka sana lkn niliwajibu ndiyo...
 
Raisi kikwete kawaagiza mkuu wa mkoa wa dar na menaja wa tanrods mkoa wampe majibu ndani ya wiki moja ni wapi itajengwa stendi mpya baada ya ile ya ubungo kuhamishwa.
Amekataa wazo lao la kujenga stendi ya muda pale chuo kikuu (udsm) na kuwaambia huko ni kufuja fedha za serekali.
Jk alikuwa anaweka jiwe la msingi ktk mradi wa mabasi yaendao kasi.

...Eeh? Nahisi kuna mtu kamuibia Mkulu wetu Password yake!!

:confused2:
 
Siku zote raisi makini, anafanya maamuzi makini. Hongera jakaya.
Tumeliwa..huu si uamuzi makini.....ni maslahi binafsi........" kwa wale msioelewa ni hivi kwamba mapendekezo ya rais na wabunge wa mkoa wa Pwani ni kwamba kituo kipya cha mabasi ya Dar kwa sasa kinatakiwa kiwe mkoa wa Pwani kwa kisingizio cha kupunguza msongamano na kufanya mkoa huo ukue haraka..... (utakumbuka Kikwete ni mzaliwa na mbunge wa Bagamoyo).... Ilikuwa kituo cha Ubungo kipanuliwe kwa kuchuka eka saba, eneo ambalo lipo nyuma ya kituo hicho...na mchakato uliishaanza na wanaoondolewa waliishataarifiwa... Eneo hilo likichukuliwa na kudesign triple loading structure ( jengo lenye level tatu za kupaki mabasi)hakuwakuwepo na haja ya eneo mbadala kuweka kituo bali Ubungo bus terminal itajitosheleza.... Sasa huyu mzee wetu anapolazimisha watafute eneo lingine kubwa kwa Dar ndani ya muda mfupi huo unadhani analenga nini
 
Mkuu binafsi saimini sana unalosema kwani sidhani kama viongozi wetu wanafanya maamuzi kwa kuanaglia wametokea wapi. Ila hebu jiulize ukiipanua ubungo hauoni kuwa unaongeza foleni isiyo ya lazima na msongamano jijini?
Nadhani njia moja wapo ya kupunguza msongamano na foleni ni hayo mabasi makubwa kuyazuia yaishie nje ya mji kabisa, ndio maana hata vipanya (hiace) zilipigwa marufuku zisiingie mjini na kosta zikachukua nafasi yake, lakini baada ya magari kuongezeka na msongamano kuonekana bado unakuwa hizo kosta (na daladala nyingine) zaidi ya 1000 zitaondolewa baada ya mabasi ya kasi kuanza.
Nadhani lengo ni kupunguza msongamano.
 
stendi ya dar inatakiwa kuwa nyuma ya mbezi, otherwise ni kuchochea foleni!

nakubaliana na wewe mkuu,ikiwezekana iwe kibaha maana hata nchi za wenzetu stand za mabasi yatokayo nje ya mji husimama pembezoni ya mji na hapo ndipo mabasi kama daladala hufanya kazi yake
nampongeza mh raisi kwa kukataa stand ya muda
 
sikubaliani na mfano kuwa hata nchi za wenzetu stand ya mabasi huwa nje ya mji, kuna miji mikubwa niliyotembelea ambayo stend kuu ya mabasi na tren/tram ziko at the heart of the city, mfano Helsink. Kinachotusumbuaa sisi ni kuwa myopic juu ya tatizo halisi, tatizo kubwa la folen dar ni kutokuwa na barabara na huduma muhimu kuwa kwenye small central sport. Tuache brabra, angalia, few years ago barabara ya kilwa alikuwa na foleni ya kutisha, baada ya kujengwa double road sasa kwenda mbagala ni few minutes. Inanisikitisha rais anapoingia kwenye upinzani wa mipango ya muda mrefu ambayo imeshatengewa na fedha. Shame.
 
Pale Ubungo ni centre Nzuri sana!! Fikiria kuweka kituo Bunju or Kibamba!! Fikiria kero ya Hao wasafiri Kufika Hapo!! Kwa Ubungo watu wanaweza Kuja na alternative designs na Kujenga Kituo cha Chini na Juu!! Decks!! Pale Ubungo stand Pako so Under utilized!! Hakuna Mpangilio Kabisa!! Wakati nasoma kuna Kitu kinaitwa Spacial Designs!! Na Kazi yake ni Kumaximaze Utilization ya available Space!! Pia kama Treni ya Mwakiembe ipo pale Ubungo itakuwa Busara Mtu anashuka kwenye basi Na Mita Chache anakuta Sehemu Ya kupanda treni na anawahi anakokwenda!! Hao wataalamu wawe Genune wasije Amua Kisiasa!! Au WACHA MBAYA IWE MBAYA TUCHUKUE ARDHI YA KIWANDA CHA URAFIKI NA KUKIGEUZA STEND KUU YA DAR!! Kwani Maeneo yake Yametulia sana kwa Abiria na convinience!! Kwani sidhan Kama TRA Wanapata kodi yoyote kutokana na Haya Magofu ya kuwinda Mufilisi!!

Pia Kule stendi ya ubungo ili ujue Kuna poor planing, siku zote wanasiasa wanasema kituo cha mafuta kiwe Mbali na makazi, ila hapa ubungo Kuna Mkusanyiko Mkubwa na pia ndani yake kuna Hadi Vituo vya mafuta!! Hii yote inadhihirisha Planning Mbovu Tuliyonayo!! Nawaaomba kabla ya kufidia watu pale wafikirie uwezekana wa Kuweka double structute palepale!! Najua wanasiasa wanaweza kuamua lolote kwani wao usafiri wa public Hauwahusu!!
 
sikubaliani na mfano kuwa hata nchi za wenzetu stand ya mabasi huwa nje ya mji, kuna miji mikubwa niliyotembelea ambayo stend kuu ya mabasi na tren/tram ziko at the heart of the city, mfano helsink. Kinachotusumbuaa sisi ni kuwa myopic juu ya tatizo halisi, tatizo kubwa la folen dar ni kutokuwa na barabara na huduma muhimu kuwa kwenye small central sport. Tuache brabra, angalia, few years ago barabara ya kilwa alikuwa na foleni ya kutisha, baada ya kujengwa double road sasa kwenda mbagala ni few minutes. inanisikitisha rais anapoingia kwenye upinzani wa mipango ya muda mrefu ambayo imeshatengewa na fedha. Shame.

hujaeleweka mkuu
hapo ktk red,mh rais hataki kuanzishwa kwa kituo cha muda cha mabasi,kuanzisha kituo hicho ni sawa na kufanya kazi mala 2,yaani leo kituo kisicho cha kudumu na kesho kituo cha kudumu,je hizo pesa za kuanzishia kituo cha muda kwanini zisiunganishwe na pesa za kuanzisha kituo cha kudumu ili tupate kituo chenye ubora wa hali ya juu?
Bado sija kuelewa nini unatetea? Ama nawe ni 10% mnao faidika na hicho kituo cha muda?
 
wewe unadhani sijhaelewa nini?, stand ya muda ililengwa kutumika wakati stand ya ubungo inafanyiwa ukarabati mkubwa(i stand to be corected) ili iweze kukidhi mahitaji, huu ni mpango wa muda mrefu so kila kiongozi anapaswa kuujua, kuibua habari ya kusema litafutwe eneo jingine linalotosheleza mahitaji inamaanisha nini? Ndo maana nikasema "Rais anaingilia ushabiki" anataka stand iende mkoa wa pwani, ethical planners watuambie kunashida gani kuwa na stand ya kisasa katikati ya mji. Personaly nimekutana na chinese firm iliyopendekeza kuwa na flyover juu ya magorofa ya kariakoo ili wale wasiohitaji ku-shop kariakoo wasiguswe ama kuchangia trafic jam ya kitongoji hicho, bado serikali inawapiga danadana. We have a long way to go.
 
Kwa kweli hata mimi namuunga mkono JK maana tulishaambia kuwa eneo litakuwa Mbezi, siyo stendi ya mabasi tu hataSoko kubwa kama la Kariaoo nalo tuliambiwa litajengwa maeneo hayo ya nje ya mji lakini miaka inakatika na hakuna lolote linaloendelea... sijui Mkuu wa Mkoa na huyo mkuu wa Tanroads wanafanya nini...?
 
Back
Top Bottom