JK Ajiandae Kutupiwa Virago na Kusahaulika Mara Moja na Watanzania.

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
WanaJF,
Kwa maoni yangu, tangu uhuru wa nchi hii, watanzania hawajashuhudia uongozi wa nchi ukiyumba na gharama za maisha zikipanda kwa kasi kubwa, kama ilivyo sasa. Kadri siku zinavyokwenda ndivyo gharama zinavyoongezeka. Kwa mfano, kufuatia kupanda kwa bei ya umeme, gharama za bidhaa na huduma mbalimbali nazo zitpanda na mbebaji wa mwisho ni mwananchi.

Ndiyo maana nahisi kwamba baada ya kipindi chake cha uongozi, wananchi watakuwa wamemchoka sana jk. Hivyo, badala ya kuagana nae kwa kushikana mikono ya kwa kheri, kama ilivyofanyika kwa marais wengine, yeye watamtupia virago aende akapumzike kijijini kwake na watamsahau mara moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…