Kunusuru kudhalilishwa vibaya mno na Dr. Slaa, Jk sasa atakiwa kumfuta kazi Kinana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunusuru kudhalilishwa vibaya mno na Dr. Slaa, Jk sasa atakiwa kumfuta kazi Kinana

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 13, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Katika hali isiyo ya kawaida, Meneja wa kampeni za JK abdulraman Kinana sasa imethibitika ya kuwa ni mzigo mzito katika kampeni ya kuokoa JK kufutwa kazi na waajiri wake ambao ni wapigakura:-


  Utafiti wangu wa kina umebaini yafuatayo:-

  a) Tofauti na mwaka 1995 wakati Kinana alikuwa meneja wa kampeni ya Mkapa ambaye alikuwa anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Bw. Agustine Mrema Nyerere ndiye aliyekuwa mpiga debe nambari one aliyesaidia kuliokoa jahazi lisizame. Ni makosa kwa CCM kudhani Kinana alikuwa na nafasi yoyote katika ushindi wa 1995 kwa CCM na Mkapa.

  CCM sasa hivi haina kiongozi aliyepo madarakani au mstaafu ambaye anakubalika kwa watanzania kwa utashi na hekima ambayo anaweza kubadilisha upepo ambao hivi sasa unaashiria Dr. Slaa na Chadema ndiyo wataunda serikali ijayo.

  CCM ilikosea kufikiria Kinana ndiye aliyewawezesha kushinda uchaguzi wa 1995 na kutegema radi ingelipiga eneo lilelile mara mbili. Ukweli ni kuwa ni Nyerere tu ndiye aliyeiokoa CCM kusarambatishwa na Mrema mwaka 1995.

  b) Tofauti na mwaka 1995 ambapo Kinana alikuwa anasimamia kampeni za Mkapa wakati ule ambapo wapigakura asilimia 42 tu ndiyo walikuwa ni vijana kati ya miaka 18 hadi 45 lakini leo asilimia 66 ni vijana kati ya miaka 18 hadi 45. Hii yaashiria ya kuwa vijana hawa wa kizazi kipya hawana mshikamano wa kihistoria na CCM kutokana na chama hicho kutoa ajira za ngazi za juu ndani ya chama na serikalini kwa wazee huku wakiwatarajia vijana kuendelea tu kuwapigia kura na kuwaweka madarakani wazee.

  Hata uteuzi wa Kinana kuwa meneja wa JK ni thibitisho ya kuwa vijana wamesahaulika ndani ya CCM.

  c) Kinana kutokana na umri wake mkubwa yaani kwenye miaka ya sitini na ushee hivi hana mvuto kwa wapigakura vijana na hivyo kutokuwa na ushawishi kwa vijana ambao ndiyo wenye turufu ya ni nani aibuke kidedea cha Uraisi na chaguzi nyinginezo.

  d) Kinana ana upeo mdogo na hivyo kushindwa kuzisoma alama za wakati. Mfano Kinana amekuwa mstari wa mbele kudai vyama vya upinzani havina sera zenye mashiko bila ya kufafanua za CCM mashiko yake yako wapi?

  Vile vile Kinana ameonyesho udhaifu mkubwa wa kushindwa kuchambua sera za CCM na amekuwa akiishia kusifia Ilani ya uchaguzi ambayo wapigakura hawajapewa hata nakala!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  CCM imetumiwa fedha nyingi sana kununua na kugawa kofia, fulana, kanga na bendera zake bila ya kutumia nguvu zaidi kuzichapisha nakala za Ilani hizo za uchaguzi.

  Utamwona Dr. Bilal akitikisa Ilani ya uchaguzi jukwaani huku wapiga debe wa CCM wakiwa wamevalia sare za CCM lakini hakuna hata mmoja wao akiwa ameshikilia vijitabu vya Ilani hizo.


  d) Kinana kutokuwa mbunifu. Hili limejidhihirisha katika mambo mengi. Mfano ni makosa kwa CCM kuuchukulia umwagaji wa damu kama ni mtaji wa kisiasa. Hii inazidi kuwathibitishia wapigakura CCM ni chama ambacho hakisomi mahitaji ya wapigakura.

  Wenye vurugu kama tulivyoona kule Musoma ni CCM hivyo kuhubiri kwa kulaumu upinzani juu ya umwagaji damu ni kosa kubwa la kisiasa kwa sababu wapigakura yote haya wanayafahamu na kamwe CCM haiwezi kuwahadaa.

  CCM imeshindwa kabisa kujibu hoja za Dr. Slaa juu ya elimu na afya bure. Walichobakia CCM ni kuzibeza hoja hizo nyeti kwa wapigakura kwa kudai ni njozi za kufikirika lakini Dr. Slaa ametaja maeneo ambayo pesa ipo akianzia misamaha ya kodi ya zaidi ya bilioni 700 kwa wachimbaji migodi wakubwa. Dr. Slaa amebainisha ya kuwa elimu bure gharama yake ni trilioni moja. Ukichanganua makadirio ya bajeti ya elimu iliyopo utaona kuna nakisi ndogo tu ya kufanikisha azma yake hiyo.

  La ajabu Kinana ambaye kila siku anaonekana kughafilika kiakili anaendelea kujigamba CCM watashinda kwa zaidi ya asilimia themanini badala ya kujibu hoja za kimsingi za Dr. Slaa kwa nini CCM inaona hizo bilioni 700 hazitoshi au hazipo katika harakati za kusaka fedha ya kutoa elimu na afya bure kwa watanzania wote.

  Nchi nyingi zilizoendelea ni kawaida kabisa kampeni meneja asipofanya kazi yake vizuri huwa mgombea Uraisi anamfuta kazi na ni dhahiri JK yupo kwenye hatihati ya kumkabidhi Dr. Slaa nchi bila ya kutaka mwenyewe au hata CCM yake.

  Jawabu hapa ni kubadilisha uongozi mzima wa timu yake ya kampeni na kuweka vijana wasomi wenye utashi mkubwa wa kisiasa ambao wapigakura wengi watawasikiliza kwa sababu ni wenzao.

  Uamuzi wa kuwaleta wachovu akina Mwinyi, Mkapa, Warioba, Malecela au Sumaye ni uamuzi ambao hauna mashiko hata chembe. Ni uamuzi ambao hauheshimu vijana na wala hautambui ya kuwa hao vigogo ni sehemu ya tatizo wala siyo ufumbuzi wa matatizo ya nchi hii.

  Wengi wao wana kashfa nyingi na watamrahisishia Dr. Slaa ushindi wa kishindo cha Tsunami hapo oktoba 31.

  KWELI NI KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.........KIGUMU HASWAAAAAAAAAAAAA

   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,511
  Trophy Points: 280
  Rusubamayuma.
  Nice analysis, nimekukubali wewe ni kichwa!, kwa kadri idadi ya vichwa humu JF inaongezeka siku hadi siku, ndivyo jf inavyozidi kuwa true and genuine home of great thinkers!.

  Thanks

  Pasco.
   
 3. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Wafa maji hao! watu walishastuka sasa hv hawadanganyiki, mitaa yangu kuna wanazi wa CCM kibao, tena wazee wa zamani haswaa, na wanavaa mashati ya kijani, gari zao wamebandika mabango ya jk-lakini wanasema hawachagui chama wanachagua Dr. Slaa.!!! Imekula kwingine mwaka huu, walizoea inakukla kwetu kila mwaka.:A S 13:
   
 4. m

  mapambano JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM has not worked as one good team since 2005 elections. CCM, hata wangemweka kijana msomi kazi bado ingekua ngumu. Huwezi kufanya kazi nzuri kama hauna timu nzuri, this is not one man's job. Viongozi wa CCM, wanajimaliza wenyewe kwa wenyewe, wameshindwa kufanya kazi kama timu, kila mtu anaangaika kutafuta personal credibility and not party's credibility. CHAMA KIMEINGILIWA...KIKWETE HAUZIKI,MBINAFSI, AMELEWA MADARAKA, MSANII (UWEZO MDOGO) NK. SIKIO LA KUFA...
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Its time to uproot CCM
   
 6. Mantissa

  Mantissa JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2010
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Jamani, tuwahi kupiga kura siku hiyo tumwondoe huyu nduli.
  Kwa pamoja tunaweza.

  Mungu ibariki Tz
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mimi kwa kweli natamani siku ya kupiga kura nikalale pale kituoni ili niwe wa kwanza kupiga kura
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,662
  Likes Received: 21,881
  Trophy Points: 280
  Pia jambo la kuipa madaraka makubwa familia yake katika kuendesha kampeni kumemharibia sana Mgombea wa CCM. Wengi wameamua kujiweka pembeni kimoyo ingawa miili yao ipo naye.
   
 9. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  kuwasafisha mafisadi ndiokumetibua mambo kabisa!!!!!
   
 10. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Tatizo nililonalo ni kwamba umewapa CCM ushauri ukubwa sana kiasi kwamba hata kuwaleta hao wastaafu kwenye kampeni sasa watafikiria mara mbilimbili unless wakampigie kampeni kulekule wanakotoka wao.

  Hivi Mwinyi kweli bado ana mvuto kwa waTZ wapiga, Mkapa na maskendo ya EPA sijui atamhutubia nani?? Tingatinga ndiyo choka kabisa, hata kwao wamemkataa. Msekwa yeye kisha soma alama za nyakati. Makamba?? Hahahahaaaaaa!!!!

  Anyway, bring them on!!!
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mazoea yanawaponza!!!!!!!!
   
 12. p

  pierre JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umetoa analysis nzuri mno.Nimeipenda ,sasa mda hautatosha kumpata mwenyekiti mwingine ambaye anaweza kubadili hali ya hewa iliyochafuliwa na kinana.Waache waende kwa wapiga kura na mabango wakifikiri ndio watanzania wa siku zile,watz wa leo hawadanganyiki.
   
 13. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Umenena mkuu huyu ni nduli kabisa tena anaonekana anajiamini kwa sababu ni mwanajeshi lakini anasahau kuwa Tanzania wasomi wote waliomaliza FVI kuanzia 1961 hadi 1994 wote ni wanajeshi wa JKT tunamsubiri 31.oct tuone hizo amri zake kama majeshi yake yatashinda wanajeshi-Raia.Haziibiwi kura mwaka huu
   
 14. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mapambano!

  Unachokisema hapo ni kweli kabisa na kuna huge gap ever since the CCM was born, Wanamtandao jamaniii hawa duuuuh ndipo walipo kileta chama chetu mahali hapa kabisa na ni wabishi kupindukia.

  Ile laaana ya kusema hao ni wazanzibara na sie ni wazanzibari ndi inawala hao wanamtandao kwani kumbuka 2005 uchaguzi wa kumteua mgombea uras CCM ilipitishwa fitna ya kumwaribia Salim Ahamed Salim kuwa yeye anasili ya Uarabuni na mambo chungu mzima kwana kipindi kile wananchi na wana CCM wengi walikuwa wanamwitaji huyo bwana S.A.S, Ila Hao wanamtandao na kiongozi wao EL&RA ndipo wakeneza sumu ya fitna na hapa sasa wametufikisha hapaeleweki kumbe mwenzetu EL anamalengo ya 2015.

  Na kugawanyika kwa CCM ndiko nawambieni kutakuja mafanikio na maendeleo ya haraka kabisa kwa wananchi wa TZ. Tatizo jingine lililoko CCM ni kuwa watu wanadhani CCM ndio Baba na mama yao hapana hicho ni chama cha raia tu kama raia wengine na vyama vingine wanatakiwa kubadilika na kuona alama za nyakati
   
 15. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Thanks
   
 16. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,603
  Likes Received: 4,708
  Trophy Points: 280
  La kuvunda halina ubani, hivi sasa CCM wako maji ya shingo hakuna namna yoyote wanaweza kuepuka kushindwa kwa kishindo, sana sana njia pekee wanayoweza kufanya ni kuiba kura, lanini hii nayo gharama yake ni kubwa. Siku REDET walipotangaza uzushi wao hata wanangu ambao ni wa umri chini ya miaka 14 waliguna na kusema huo ni uongo,sasa hapo NEC itakapomtangaza Mgonjwa wa Taifa kuwa ndiye mshindi wa kishindo kama ambavyo wamepanga kufanya sijui watawabebea watz mbeleko gani.
   
Loading...